Aibu! John Heche adai mkuu wa wilaya Nyamagana anachangisha 10k kila mzazi kujenga madarasa

Inakuwa ni kumhadaa Raisi wetu mpendwa.

Maisha yenyewe yamekuwa magumu sana kutokana na Covid19, na kupanda kwa Mafuta, huu sio muda muafaka wa kubebesha Wazazi mzigo wa ziada.

Kwanini wasisubiri tutoke kwenye huu "mkwamo"wa kiuchumi?.

Mimi huwa namwelewa sana Mama Samia Suluhu wasimuangushe bhana.

Mungu mjaalie Rais wetu mpendwa.
 
Tozo huko nyamagana zinafanya kazi gani mkuu au zinajaza mafuta ya ma vx ya watawala wa nyamagana?

maana sehemu nyingine madarasa hadi 1000 yashajengwa na tozo na wanaofundisha ni misukule sababu hamna ajira mpya za walimu
Unamaanisha mke wa Heche anayefundisha ni msukule?
 
Unamaanisha mke wa Heche anayefundisha ni msukule?
Hayo madarasa mapya na zahanati tunazidanganywa zimejengwa na tozo zinahudumiwa na vibwengo?
Au wanuka jasho walioko ajirani wanajigawa mara mbili?
Maana mitakwimu mikuuuubwa kama mlima halafu hakuna matangazo ya ajira mpya za walimu,manesi na madr,nchi ka kingese sana hili
 
Kwa hiyo unadhani hajui kinachoendelea?
Kama aliweza kuwakumbusha wafanyabiashara kupandisha bidhaa bei nini kinakufanya uhisi anajali maumivu ya watu?
 
Kwa hiyo unadhani hajui kinachoendelea?
Kama aliweza kuwakumbusha wafanyabiashara kupandisha bidhaa bei nini kinakufanya uhisi anajali maumivu ya watu?
Alisema kuwa vitu vitapanda kwa jinsi hali ilivyo lakini aliongelea uhalisia kuliko angenyamaza vitu vikaendelea kupanda na yeye kimya tu nadhani angeshambuliwa sana.
 
Lisu yuko bize na amsterdam.

Ufipa inanuka kisamvu
okay umesikika, haya sasa sisi tuna focus na wilaya ya nyamagana kutopewa pesa za TOZO kujenga madarasa hadi wazazi wanalazimishwa kutoa 10k
 
anzishia mada ya lissu na amsterdam hapa issue ni mchango wa lazima wa madarasa kwa amri ya mkuu wa wilaya wakati tunaambiwa TOZO ndizo zinajenga madarasa
Kwanini usiende Jijini Mwanza ukajionea kama kuna hiyo michango ya lazima? Ipo siku utaambiwa mimi ni babaako na utakubali!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…