Aibu kubwa kwa Mahakama. Mkuu wa Wilaya apiga marufuku maamuzi ya Mahakama kuheshimiwa, ajipa mamlaka (video)

Aibu kubwa kwa Mahakama. Mkuu wa Wilaya apiga marufuku maamuzi ya Mahakama kuheshimiwa, ajipa mamlaka (video)

nzagambadume

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
2,430
Reaction score
5,779
Jaji Mkuu wa awamu ya tano, you will go down as the worst Chief Justice in history.

Mwenzako IGP jeshi lake linadhalilishwa hadi na vijikatibu kata vya Ccm wanatoa amri kwa mapolisi.

Huko Handeni Godwin Gondwe na yeye anavaa sare ya JWTZ, ma doctor nao wanakaripiwa na kufukuzwa kazi na makatibu wa shina wa CCM . Ni tafrani tupu, sasa jionee maajabu ya video hapa.

Ama kwa hakika tumepatikana, misingi ya nchi inavunjwa vunjwa mbele yetu tukiona ukilalamika unasikia eti hauoni ndege and fly-overs?

Kama ni hivyo kina Mandela wangekausha tu maana makaburu yalinunua ndege na kujenga miundombinu zaidi ya Chattleville.

Walahi hawa vifutu wanaojimwambafai walishajua baba yao anapenda watu wa aina gani.

Huu ni ujinga sasa nchi imekuwa ya kipuuzi kwelikweli.

 
Jaji mkuu wa awamu ya tano you will go down as the worst chief justice in history,mwenzako IGP jeshi lake linadahlilishwa hadi na vijikatibu kata vya ccm wanatoa amri kwa mapolisi
Huko Handeni Godwin gondwe na yeye anavaa sare ya JWTZ, ma doctor nao wanakaripiwa na kufukuzwa kazi na makatibu wa shina wa ccm nio tafrani tupu
sasa jionee maajabu ya video hapa,ama kw ahakika tumepatikana aiseee,misingi ya nchi inavunjwa vunjwa mbele yetu tukiona ukilalamika unasikia eti hauoni ndege an dflyovers, kama ni hivyo kina mandela wamgekeausha tu maana makaburu yalinunua ndege na kujenga miundombinu zaidi ya chattleville
walahi hawa VIFUTU WANAOJIMWAMBAFAI walishajua baba yao anapenda watu wa aina gani,huu ni ujinga sasa nchi imekuwa ya kipuuzi kwelikweli

Mbowe hajambo!
 
Mwakani syo mabali
usishangae keshapokea simu ya pongezi kutoka barack obama road huku akiambiwa wewe chapa kazi nasema chapa kazi,instituitions za nchi zimekufa kabisa,Rais anagawa hela kama oioi na kuamua wapi atoe wapi akatae halafu eti wanasema kuna mihimili mitatu,my foot.
 
Mbowe hajambo!
cha kufurahisha ni kwamba kila comment ikipinga upuuzi mna associate na cdm which means inawasumbua akili,maana hadi leo watu wamezima simu na kufunga offisi wakiwakimbia wagombea wa cdm wasirudishe fomu halafu utasikia eti upinzani umekufa mara nyokonyoko ccm ni ya kisayansi
 
Halafu mnaamini kuwa nchi hii kwenye mazingira ya sasa kuna mtu mwenye akili ya kawaida atawekeza pesa zake?
 
Hawa wanatakiwa kwanza kabisa kufundishwa kuwa nchi hii inatawaliwa kwa misingi ya KATIBA!! Katika katika kuna separation of powers kati ya BUNGE, MAHAKAMA na SERIKALI KUU. Kila muhimili una mamalaka yake yanayotakiwa kutoingiliwa na muhimili mwingine na hiyo ndio inafanikisha CHECKS AND BALANCES kati yao!

Sasa wanateuliwa hawa viazi hawajui hata kuwa kuna katiba matokeo yake ndio hayo matamshi ya kiwenda wazimu yanayoitia aibu serikali na chama tawala.
 
Hii ni aibu halafu hadi sasa hivi jaji mkuu kakaaa kimya tu kuna siku majaji watakuwa wana report hadi kwa makatibu wa shina wa ccm , UJINGANA UBWEGE HUU, LI NCHI LIMEKUWA LA HOVYO KWELI
 
Kesho kutwa akipata matatizo anakimbilia mahakamani huko huko
 
Back
Top Bottom