Aibu kuu kwa nchi yangu Tanzania huko Saudi Arabia: Bondia apigwa kipigo cha mbwa koko

Aibu kuu kwa nchi yangu Tanzania huko Saudi Arabia: Bondia apigwa kipigo cha mbwa koko

Leo kuna pambano kati ya antony Joshua na andy Luiz, sasa kwenye Yale mapambano ya utangulizi wamepigana watanzania wawili,Mohammed na said wote wamepigwa ila kipigo cha huyu said ilikua balaa,kapigwa right jeb moja hatari sana,ilibidi madaktari wamuwai,pambano lilikua la round nne, dogo rounds ya kwanza tu kala jeb moja matata sana... Cha kusikitisha dgo aliemchapa anamiaka 19 tu wakati jamaa ana 32
Inaonekana umeanza kuangalia ngumi hivi karibuni.

Mtu kupigwa round ya kwanza ni kitu cha kawaida sana katika ngumi
Wanaomjua MIKE TYSON wanaelewa.
 
Ni hujuma tu unapelekaje mabondia km hao
Kwa kweli hata mimi nimeshuhudia,afadhali yule wa kwanza kidooogo alionyesha upinzani. Huyu wa pili sijui Saidi na body yake ilivyojazia nikajua atamchakaza vibaya dogo aitwaye Pacheco kutoka Texas, USA lakini kumbe mawazo yangu yakawa kinyume Bw Saidi raundi ya kwanza tu hakufurukuta, alilamba sakafu na kusababisha apatiwe first aid hali ilikuwa tete sana.

Ni aibu sana tunafahamu kule Saudi Arabia kuna Watanzania wengi wanaishi huko bila shaka watakuwa wamejisikia vibaya. Mapromota angalieni mabondia wenye viwango ili kuondoa aibu kama hii siku za usoni.
 
Jaman hiz ngumi ziacheni ziitwe ngumi

Sikuzote mtu kujitutumua ulingoni inategemea umekutana na mpinzan wa aina gan.
Ukikutana na mtabe anae kuzid ujanja lazma ukae.
Ndo mana mwakinyo ilibid AJ ametumia teknik kumshinda chibonge. Angeenda kichwa kichwa angevunjwa taya.
 
Huyo Mohammed wakati anaingia alikuwa na mbwembwe nyingi nikamwambia wife kwa mbwembwe zile Kama anaenda ngomani lazima achezee kichapo hakuamini kilichomkuta Mtanzania mwenzetu kutoka Darisalama.Shukrani za pekee ziende kwa refa.
 
Hahaha mleta uzi yaan kwamba Watz wenzetu huko wanataka kuuwa huko alaf si hatuna habari.
Mkuu, tumezoea kuwa na mapokezi ya kitaifa kwa mabondia wanaoshinda nje, hadi ikulu. Sasa mara hii tutakuwa na mazishi ya kitaifa
 
Back
Top Bottom