Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Siku ya leo, Jaji wa mahakama kuu, Irvin Mgeta, ameandika historia, baada ya kubatilisha hukumu iliyokuwa imetolewa na Hakimu, Thomas Simba, wa mahakama ya Kisutu, hapo mwezi March, 2020, ambapo aliwatia hatiani viongozi hao wa Chadema, kwa Makosa 10 Kati ya 11, waliokuwa wameshitakiwa nayo.
Najiuliza hivi huyo Hakimu Thomas Simba, aliwezaje kuwahukumu akina Mbowe, kulipa faini au kwenda jela miezi 5 wakati walikuwa hawana hatia, kama ambavyo amebaini Jaji wa mahakama kuu, Irvin Mgeta?
Watanzania tunautegemea mhimili wa mahakama ututendee haki bila ukiangalia itikadi zetu za kisiasa, kwa kuwa inafahamika wazi, ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3, kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi
Kwa kutotenda haki kwa mhimili huo , kwa kuwaonea waziwazi wapinzani wa nchi hii, imeleta doa kubwa Sana kuwa mhimili huo wa kutoa haki na wananchi wataanza kukosa imani kuwa mhimili huo unatoa hukumu zake kwa kuwaonea wapinzani.
Imenenwa katika Biblia, katika kitabu cha Mithali sura ya 14:34 kuwa "Haki huinua Taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wote"
Hakimu Simba aliwezsje kuwatia hatiani viongozi hao wa Chadema kwa ajili tu ya kufanya maandamano, ambayo ni halali kwa mujibu wa Katiba yetu, wakimlalamikia Mkurugenzi wa wilaya hiyo ya Kinondoni kwa kutoa viapo vya mawakala wa CCM huku akiwanyima wale wa Chadema?