Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Mida ya usiku pale kwenye geti la kutokea Tanzania kuingia Rwanda maafisa wetu wa forodha huwa wanafanya uzembe unaohatarisha usalama wa taifa letu kwa wao kwenda majumbani ama nyakati zingine kwenda kuangalia mpira na pengine kwenda bar na mhuri huo hapo juu huachiwa vijana wa ving'amuzi kuutumia kwa kuwagongea madereva ama wenye mizigo kuruhusu kutoka upande wa Tanzania.
Hoja hapa siyo kuharibu kibarua cha mtu bali ni uzalendo.
Iweje afisa forodha azingatie starehe na kumilikisha kijana asiye na sifa kutumia mhuri nyeti namna hiyo?
Binafsi nilipeleka bidhaa zangu huko Rwanda na ajabu tena ikiwa mapema saa 2100 usiku mimi,agent wangu na dereva wangu pia tulikuta afisa mhusika wa zamu hayupo na tukaelezwa mhuri anao yule kijana wa ving'amuzi jambo lililonisononesha sana!
Jamani Watanzania wenzangu hasa mliopewa dhamana mahali fulani tujitahidi tuwe na uzalendo japo kiduchu kwa nchi yetu.