Aibu kwa TRA idara ya forodha Rusumo; Mhuri nyeti huachiwa nyoka (kijana)

Aibu kwa TRA idara ya forodha Rusumo; Mhuri nyeti huachiwa nyoka (kijana)


Mida ya usiku pale kwenye geti la kutokea Tanzania kuingia Rwanda maafisa wetu wa forodha huwa wanafanya uzembe unaohatarisha usalama wa taifa letu kwa wao kwenda majumbani ama nyakati zingine kwenda kuangalia mpira na pengine kwenda bar na mhuri huo hapo juu huachiwa vijana wa ving'amuzi kuutumia kwa kuwagongea madereva ama wenye mizigo kuruhusu kutoka upande wa Tanzania.

Hoja hapa siyo kuharibu kibarua cha mtu bali ni uzalendo.

Iweje afisa forodha azingatie starehe na kumilikisha kijana asiye na sifa kutumia mhuri nyeti namna hiyo?

Binafsi nilipeleka bidhaa zangu huko Rwanda na ajabu tena ikiwa mapema saa 2100 usiku mimi,agent wangu na dereva wangu pia tulikuta afisa mhusika wa zamu hayupo na tukaelezwa mhuri anao yule kijana wa ving'amuzi jambo lililonisononesha sana!

Jamani Watanzania wenzangu hasa mliopewa dhamana mahali fulani tujitahidi tuwe na uzalendo japo kiduchu kwa nchi yetu.
Huu muhuri unagongewa kwa madhumuni gani?
 
Huwa sielewi hasa majukumu ya wazee wa vitengo ,yasemekana wapo kila pahala hususani maeneo nyeti. Wanasema utumishi wa umma ni life insurance, ama utake mwenyewe.
 
Kazi hazina mikataba ukiingia ndio milele, hazina target ambayo usipofikia unakua rated as underperformer. Wacha wale kwa urefu wa kamba zao
 
Sawa
Hawa Watumishi Wamevimbiwa
Watapapaswa Muda Siyo Mrefu Sana
 
Nchi ishakufa kaka si mijini tu ila hata vijijini yanayoendelea si Sawa, nimebahatika kuitembelea mbeya vijijini , katika kijiji kinaitwa ISUTO wao wanaita umalila, pale kuna zahanati ya kijiji hivi uliwahi jua kupimwa UKIMWI kwenye hospitali za serikali ni gharama? Basi ni hapa kwenye hiki kijiji watu wanalipishwa sana lakini pia wengi wameathirika na bado hakuna ethics kwa hawa madaktari maana wakikupima kukutangaza ni kawaida.

Oooh Tanzania ya nyerere iko wapi?
Hivi tunaweza kuporomoka zaidi ya hivi tulikofikia sasa?

Mbona inatisha sana!
 
namuagiza mkuu wa wilaya awaweke ndani masaa 48
 
Yanasemwa kimzaha mzaha vile, kumbe ndiyo tabia yenyewe hiyo aliyonayo mtu.

Kuna siku atapatikana mzalendo wa kweli anayejali maslahi ya nchi hii. Watu kama nyinyi mtalia na kusaga meno.

Usiniambie, na wala sitaki kusikia ukimtaja Magufuli kama mfano wa MZALENDO huyo. Yupo, yuko njiani. Mtakoma tu!

'Bondpost', inanilazimu nikukumbuke tokea sasa, kama mmoja wa maadui wa nchi yetu.
Sawa tu kimpango wako Ila if horses were wishes even beggars would ride my friend.

Tafuta hela haya makasiriko yatakuisha utasahau haya mambo ya uzalendo mwitu
 
Sawa tu kimpango wako Ila if horses were wishes even beggars would ride my friend.

Tafuta hela haya makasiriko yatakuisha utasahau haya mambo ya uzalendo mwitu
Mkuu, huu mzaha na mambo kama haya siyo mzuri hata kidogo. Sote tunaumia tu ndani ya taifa letu hili.

Wakati mwingine nadhani ni bora kuyanyamazia mambo kama haya kuliko kuyapa nguvu kwa kuyashabikia kimzaha mzaha hivi.
 
Sawa
Hawa Watumishi Wamevimbiwa
Watapapaswa Muda Siyo Mrefu Sana
Wakututapisha nani...huyu anayetumia masaa 2 kuandika "hints" za hotuba atakayohubia alafu akipewa nafasi anahutubia dk 2 na sekunde saba kwisha! tena points nje kabisa ya mada!
 
Back
Top Bottom