Aibu kwa TRA idara ya forodha Rusumo; Mhuri nyeti huachiwa nyoka (kijana)

Huu muhuri unagongewa kwa madhumuni gani?
 
Huwa sielewi hasa majukumu ya wazee wa vitengo ,yasemekana wapo kila pahala hususani maeneo nyeti. Wanasema utumishi wa umma ni life insurance, ama utake mwenyewe.
 
Kazi hazina mikataba ukiingia ndio milele, hazina target ambayo usipofikia unakua rated as underperformer. Wacha wale kwa urefu wa kamba zao
 
Sawa
Hawa Watumishi Wamevimbiwa
Watapapaswa Muda Siyo Mrefu Sana
 
Hivi tunaweza kuporomoka zaidi ya hivi tulikofikia sasa?

Mbona inatisha sana!
 
namuagiza mkuu wa wilaya awaweke ndani masaa 48
 
Sawa tu kimpango wako Ila if horses were wishes even beggars would ride my friend.

Tafuta hela haya makasiriko yatakuisha utasahau haya mambo ya uzalendo mwitu
 
Sawa tu kimpango wako Ila if horses were wishes even beggars would ride my friend.

Tafuta hela haya makasiriko yatakuisha utasahau haya mambo ya uzalendo mwitu
Mkuu, huu mzaha na mambo kama haya siyo mzuri hata kidogo. Sote tunaumia tu ndani ya taifa letu hili.

Wakati mwingine nadhani ni bora kuyanyamazia mambo kama haya kuliko kuyapa nguvu kwa kuyashabikia kimzaha mzaha hivi.
 
Sawa
Hawa Watumishi Wamevimbiwa
Watapapaswa Muda Siyo Mrefu Sana
Wakututapisha nani...huyu anayetumia masaa 2 kuandika "hints" za hotuba atakayohubia alafu akipewa nafasi anahutubia dk 2 na sekunde saba kwisha! tena points nje kabisa ya mada!
 
Wafanyakazi wa serikali ni janga na wanamkosesha mama tozo, walipoti tuu panapohusika hatuwezi kupoteza tozo kwa walevi kama hao

Hao ndo mama anao wataka maana hawana nidham ya uoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…