AIBU: Mchekeshaji Said Said aaibika baada ya kuzuiwa na walinzi wa Rais, kisa zawadi ya Cheni

AIBU: Mchekeshaji Said Said aaibika baada ya kuzuiwa na walinzi wa Rais, kisa zawadi ya Cheni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Said Said aondoka kwa aibu baada ya kuzuiwa na Walinzi wa Rais Samia alipotaka kumkabidhi Kitu kutoka mfukoni mwake baada ya ku-perform kwenye Samia Kalamu Awards.

Wadau mbalimbali wa Sanaa ya Uchekeshaji wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu tukio hili

IMG_4722.jpeg
IMG_4719.jpeg
 
Said Said aondoka kwa aibu baada ya kuzuiwa na Walinzi wa Rais Samia alipotaka kumkabidhi Kitu kutoka mfukoni mwake baada ya ku-perform kwenye Samia Kalamu Awards.

View attachment 3325883

Umeandika as if Said alikunyang'anya demu wako....Mbona sijaona cha ajabu hapo chochote zaidi ya protokali? huwezi kumkabidhi kitu prezdent kutoka mfukoni mwako bila ya walinzi kukichukua wao kwanza ,hapo ni elimu tu wasanii wapewe kuhusu itifaki.
 
Nimekiona hicho kitoto Said Said kipuuzi sana hakijui kua kuna wakati wa utani utani na kuna wakati wa kua serious kidogo. Jana kilitakiwa kijikite na ucheshi mbali na mama lakini chenyewe hovyoo wala hakikusoma wakati, kimeboa sana sana sidhani kama kitakuja ipata hio nafasi tena.
 
Hawa Comediana hasa huyo Said Said hafai kabisaaa kabisaaaaa kuitwa katika events za Mh. Rais…!!

Wanao andaa events za Mh. Rais wasirudie tena kosa kama hilo, huyu kijana hajui mambo anayoongea, wala hachekeshi, anatia aibu na ni kukosa adabu kabisa, nimekereka kiukweli, asialikwe tena..

Leonardo is the best Comedian kualikwa na yule kijana wa Mbeya, mweusi, sijui anaitwa nani, pia akina Mpoki na Joti ndio wanafaa sana kualikwa..!!

Huyo mtoto Said Said hafai kabisa
 
Inaelekea huyu dogo kupiga picha na Rais iliwaumiza watu wengi sana.

Watanzania wana wivu, chuki na roho mbaya sana.
​
Dogo bado hajakomaa kiakili Raisi ni Kiongozi mkuu wa Nchi huwezi mletea mzaha kama ule lazma uweke Mpaka na kumtofautisha na mtu mwengine wa kawaida

Hakuna sehemu yoyote huyu dogo amemkosea Rais heshima, tatizo la watanzania wengi ni uelewa mdogo na uchawa kwa wingi.

Mnashindwa hata kuelewa vitu vidogo kama pale juu kijana alipanda kuchekesha?
​
 
Back
Top Bottom