Aibu tupu!! Vyuo vya Tanzania mtu anasoma masomo ya biashara miaka mitatu na kulipa almost milioni 5 lakini hajui hata kufungua biashara

Hii nchi ukiwa msomi inabidi ujiandae kuonekana hujui mambo. Mifumo ya Elimu ipo more theoretically.
 
Ni kwamba la saba lazima awe na confidence kwa sababu hana chaguo .
 
Tofautisha masomo ya biashara (commerce and Business Administration) na mafunzo ya Ujasiliamali (Entrepreneurship). Commerce and Business Administration wanasoma maeneo kama uhasibu, Masoko, Uendeshaji wa Bima (Insurance), Uendeshaji wa Benki (Banking), Usimamizi wa Fedha (Finance). Mtu akimaliza digrii ya biashara pekee siyo lazima akupe njia za ujasiliamali. Vyoo vingi vya Marekani hue eka digrii ndogo (Minor degree) ya ujasiriamali kuwasaidia graduate kuanzisha biashara zao katika mazingira ya kisasa. Kwenye kodi za ujasiliamali Ngoako wanakofundisha sheria na taratibu za kuanzisha biashara, njia za kutafuta mitaji na mbinu za kujijingea soko. Hizi digrii ndogo za ujasiliamali zinatolewa kwa mtu yoyote anayetaka: engineering, medicine, commerce, law, agriculture, education n. k.
 
Watu kibao wanaosoma Us na ulaya wakirudi bongo huwa wana anzisha biashara zao, wapo wengi wanaoacha hata ajira, Elimu za wezetu zinafungua sana vichwa + exposure. Mfano moja wapo ni Mengi alikuwa na ajira safi sana akiwa mtu wa kwanza kupata cpa hapa nchini lakini baada ya muda akaingia kwenye business.
 
Hawamalizi masomo ya biashara tu na kuanzisha biashara. Wengine kufanya kazi katika makampuni ya huko na kujipatia knowledge na experience ya kuanzisha na kuendesha biashara. Ikiwa angalia hao unawatumia kama case study yako wanatoka kwenye background mbalimbali siyo tu kuwa walisoma commerce. Wengine hawa kwenda college kabisa Bali walikuwa wakifanya kazi katika kampuni walikojipatia ujuzi wa biashara
 
Nyie si mlisema elimu ya makaratasi haifanyi kazi mtaani, Kulikoni tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…