DOKEZO Aibu UDSM kiajiri wahitimu isiwalipe

DOKEZO Aibu UDSM kiajiri wahitimu isiwalipe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Vumilieni, mambo ya utumishi yana taratibu zake. Mtalipwa pamoja na malimbikizo
 
Katika miaka ya hivi karibuni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa kikichukua wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma wahitimu kubaki kusaidia shughuli za kitaaluma (TAs).

Cha kusikitisha vijana Hawa Chuo huwatekeza bila mikataba wala malipo. Kwa mfano, vijana wengi waliohitimu mwaka 2024 na kubakishwa kwa madhumuni hayo wanaendelea na kazi kwa miezi mitatu (3) sasa bila kupewa mikataba ya kazi wala kulipwa chochote.

Hivi, UDSM inafikiri wanaishije vijana Hawa? Mnawaingiza katika matatizo makubwa ya maisha na pia kutowalipa wala kuwapa mikataba ni ukiukwaji wa sheria ya Kazi na Mahusiano kazini.

UDSM Angalieni hili muwasaidie Hawa vijana
Mleta mada hukustahili kupewa nafasi UDSM hujui kutunza siri unakuja kujianika humu kuwa umepata nafasi UDSM na hujalipwa miezi mitatu

Anyway kama ulibebwa huyo aliyekubeba umeshamuumiza hata kama humjui yuko behind the scenes

Wabebaji muwe makini watu mnaowabeba yaweza wagharimu

Nadhani naeleweka code gani nimetumia humu kuhusiana na hili kwa wajua codes
 
Hajuiq siri za ofisi ni rahisi sana kukamatwa .
 
Pole kwa Wahanga, naamini waliaopo kwenye nafasi za maamuzi watafanya jambo ili kuhakikisha kwamba Wahusika wanapata stahiki zao za msingi.

Sina uhakika kwa kada zingine, ila kwa kada ya uhandisi, kubakiza wahitimu waliofanya vizuri na kuwaendeleza kimasomo ili waje kuwa Wakufunzi ni kuangamiza elimu yetu na kuzalisha wahitimu wasio na maarifa yanayohitajika kwenye soko la ajira. Ufaulu pekee tu isiwe kigezo, kama chuo kinaona kinamhitaji mhitimu fulani kutokana na ufaulu wake, ni vyema ikaingia naye makubaliano akafanye kazi (huku akipewa na mafunzo hitajika) kwenye mazingira yenye ujuzi sawa na ile course anayohitajika kuja kufundisha, baada ya miaka mitano ndo wamrudishe kuja kufundisha.

Vinginevyo wataishia tu kukaririsha wanafanzi mambo.
 
Wewe nakutambua vizuri na ulibakizwa kama TA 2024, kwa kuja kulalamika uongo hapa, umejiponza.
Akishalipwa kama kuna mkataba wa kulipana miezi yake ofis ya ajira UDSM imwambie kwa heri ya kuonana awasalimie huko aendako sababu ofisi ya UDSM haina mkataba naye wa ajira anajitolea tu
 
Tatizo hamna mkataba hata wao wanaumiza kichwa mtalipwaje...vumilieni vibali vya kuajiri vikitoka mtakula shavu, maana ni scholarship after scholarship leo ulaya mwakani America halafu haya mnasahau mnaamza kututafunia vitoto vyetu vinavyotegemea boom.
So chuo kikuu cha Dar kinafanyisha watu kazi KIHUNI? Sekta binafsi ikifanya hivo, vyombo vya kisheria vinapiga kelele, ajabu watu wazima na akili zetu kabisa tunaunga mkono jambo OVU kama hili kufanywa na taasisi ambayo ilitakiwa kua mfano wa kila kitu; poor us
 
Kwanini asiache hiyo kazi akatafute yenye malipo ? Tuanzie hapo.
 
Itakuwa alibakishwa kwa upendeleo. Ndio maana analalamika mtandaoni.

Graduates wenye gpa kubwa za halali huwa wanagombaniwa na PWC, KPMG ama EY . kama Udsm ikiwataka wabaki huwa inawapa mkataba wa ajira moja kwa moja na kuanza kuwalipa mishahara. Hakunaga mambo ya kujitolea
 
Kwanini usiseme ni wewe useme madogo mkuu be free funguka usaidiwe

Kingine kwanini usiwaulizw waliokubakiza hapo uendelee na kazi za chuo wana lengo gani na je kuhusu malipo yapoje?
Unalazimisha iwe Mimi, Mimi ni GenX na ninaosema ni GenZ
 
Katika miaka ya hivi karibuni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa kikichukua wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma wahitimu kubaki kusaidia shughuli za kitaaluma (TAs).

Cha kusikitisha vijana Hawa Chuo huwatekeza bila mikataba wala malipo. Kwa mfano, vijana wengi waliohitimu mwaka 2024 na kubakishwa kwa madhumuni hayo wanaendelea na kazi kwa miezi mitatu (3) sasa bila kupewa mikataba ya kazi wala kulipwa chochote.

Hivi, UDSM inafikiri wanaishije vijana Hawa? Mnawaingiza katika matatizo makubwa ya maisha na pia kutowalipa wala kuwapa mikataba ni ukiukwaji wa sheria ya Kazi na Mahusiano kazini.

UDSM Angalieni hili muwasaidie Hawa vijana
Ndugu Mtoa Mada,

Hebu fuatilia vizuri. Ninachofahamu ni kwamba utaratibu wa kubakiza wahitimu waliofanya vizuri ulishaachwa katika vyuo vya umma.

Siku hizi ajira zote za vyuo vikuu vya umma zinatangazwa kwa uwazi na Mtanzania yeyote mwenye sifa anaomba. Baada ya maombi kupokelewa panakuwa na usaili jumuishi. Mpaka wawakilishi wa Wizara huwa wanakuja.

Wale wanaobahatika kuajiriwa majina yao hupelekwa Utumishi kwa hatua zinazofuata -- kama mtumishi mwingine yeyote wa serikali. Mishahara huanza kutoka muda wowote ndani ya miezi mitatu.

Kama kuna mtu amebakizwa UDSM kwa utaratibu wa zamani hebu mwambie afuatilie vizuri ajue amebakizwa kivipi. Pengine amebakizwa kama research assistant chini ya mradi fulani.
 
Kwanini asiache hiyo kazi akatafute yenye malipo ? Tuanzie hapo.
Unaielewa hoja yangu kaka? Siwatetei waliozurumiwa, narudia tu just in case hujanielewa, "Kitendo cha kuajiri watu bila mkataba na kimefanywa na taasisi inayo heshimika kama UD ni kibaya na kashfa kubwa" uhuni kama huo ufanywe na sekta binafsi, sio taasisi za serikali na hasa chuo kikuu cha Dar, zamani UD ilijulikana kama the home of intellectuals, bahati mbaya sana sasa hvi ndio kina ongoza kutoa machawa wengi zaidi. Ujumbe wangu upo pale kwenye alama hizi " "
 
Back
Top Bottom