Aibu ugenini

Aibu ugenini

BoManganese

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
980
Reaction score
2,679
Habari zenu wanaJF.

Leo imetokea nimekumbuka tukio fulani hivi lililonitia aibu kubwa ugenini kila nikifikiria nachekea na kuhuzunika at the same time.

Ili kuwa ni hivi kipindi hicho nimepata safari ya kwenda kwa ma mkubwa baada ya likizo nakumbuka ilikuwa form 5 kwenda 6. Nilifika ugegeni na kupokelewa vizuri sana na kupewa sifa kedekede kwamba mimi ni kijana mpole na mstaarabu sana.

Pale palikuwa na madogo wengine wa sekondari wawili wa kiume wote sasa baada siku mbili tatu kuzoea mazingira pale nilikuwa sio mtu wa kuzurura kwasababu sikuwa nimeizoea mitaa ya kule.

Sasa siku nikopale mida ya alasiri nikajikuta niko mwenyewe mule ndani nikaona ngoja nicheki CD nione kuna movie gani niangalie nilikuta CD nyingi nikawa nabadili kwa kuwa movie zenyewe zilikuwa za zamani.

Sasa katika kuchekicheki nilikuta CD mbili zimebananishwa katika kasha moja CD moja ilikuwa ni ya movies lakini ile nyingine ilikuwa nyeupe tuu haina jina. Nikaweka hiyo CD nyeupe nijue ina nini aisee kumbe ilikuwa ni porn.

Wakati ile CD inaendelea kuplay sijui ni shetani gani liliniingia nikajikuta nimeduwaa tuu naiangalia. Ujinga nilioufanya ni pale niliposema ngoja nikimbie mara moja jikoni nikanywe maji ili nirudi chap kucheki uhondo.

Niliacha CD inaendelea kuplay pale mi nienda jikoni kwenye fidge sasa wakati nahangaika kumimina fasta fasta mara nasikia sauti kama za watu sebleni. Aisee moyo ulilipuka paaaah nikawa naomba wasiwe watu kweli.

Nikaenda fasta moja kwa moja sebleni ile nimesimama malangoni kutokea jikoni nakutana macho kwa macho na wageni watatu pamoja na ma mkubwa aisee mpaka leo najiuliza wale watu waliingiaje mule ndani bila ya mimi kusikia.

Ma mkumbwa akaenda kuzima ile tv maana bado ilikuwa inaplay watu wanakulana mzigo. Mimi niliwasalimia nikanyoosha moja kwa moja nje nikiwa na aibu kubwa mno pamoja na uoga.

Nilikaa nje mpaka usiku nikifanya mipango ya nauli nisepe maana ilikuwa ni bagamoyo mimi kwetu ilikuwa ni DSM. Kweli nilifanikisha kupata nauli nilipoingia ndani nikamwambia ma mkumbwa mi naomba niende nyumbani nisamehe sana kwa nilicho kifanya nilimwelekeza kuwa zile CD nilizikuta kule kule, japo alinihasa nisiondoke amenisamehe lakini niliforce mpaka nikasepa.

Vipi kwenu wadau tukio gani lilikuaibisha sana ugenini mpaka ukashindwa kukaa huko.
 
Bado sijawahi kupata aibu ugenini..
Labda uniweke mbele ya hadhira niongee tena lugha iwe kiingereza hapo ndo utajua umechagua shetani badala ya malaika.. ila nipe kalamu na karatasi uone navyocheza navyo,hapo sikuaibishi..😜
 
Bado sijawahi kupata aibu ugenini..
Labda uniweke mbele ya hadhira niongee tena lugha iwe kiingereza hapo ndo utajua umechagua shetani badala ya malaika.. ila nipe kalamu na karatasi uone navyocheza navyo,hapo sikuaibishi..[emoji12]
Basi mkuu usiombe maana ni noma sana
 
Wote mnabidi mgawane aibu hiyo kwasababu hiyo CD wewe hukujanayo bali umeikuta humo humo ndani na isitoshe hakukuwa na alama yoyote ya tahadhari juu ya hiyo CD mbaya zaidi ilikuwa pamoja na CD zingine.

Hao na wao ni watu wa porn.
 
Lakini mshikwa na ngozi si ndo mwizi😂😅
 
nitaweka baadae video hapa ni true story alikua anasimulia Mr bean kuna jamaa alienda kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya rafiki yake sasa akabanwa haja kubwa akajiongeza akatafuta choo bila kuuliza wenyeji akafanya yake kumbe ile nyumba ilikua haijafungwa mfumo wa maji[emoji1787]
 
Wote mnabidi mgawane aibu hiyo kwasababu hiyo CD wewe hukujanayo bali umeikuta humo humo ndani na isitoshe hakukuwa na alama yoyote ya tahadhari juu ya hiyo CD mbaya zaidi ilikuwa pamoja na CD zingine.

Hao na wao ni watu wa porn.
Aisee kwakuwa mimi nilijipendekeza kuendelea kuangalia zigo limeniangukia
 
nitaweka baadae video hapa ni true story alikua anasimulia Mr bean kuna jamaa alienda kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya rafiki yake sasa akabanwa haja kubwa akajiongeza akatafuta choo bila kuuliza wenyeji akafanya yake kumbe ile nyumba ilikua haijafungwa mfumo wa maji[emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23]hii nayo balaa
 
Swali, je ulikutwa unaangalia au hakuwepo unaangalia kipindi walipoingia ndani??
Sikukwa pale nacheki ila kwa situation ilivyo kuwa ni wazi kabisa wangejua mi ndio muhusika
 
Back
Top Bottom