AIBU: Wachungaji KKKT wampinga Dk Shoo

AIBU: Wachungaji KKKT wampinga Dk Shoo

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Mambo mengine ni kushangaza sana inakuwaje Kanisa lenye waumini wengi kujiendesha kama klabu ya pombe hukuna maelewano ni vurugu, tamaa ya mali hakuna uungu hapo.

Siku chache baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT), Dk Fredrick Shoo kuagiza kiti cha Askofu Dk Edward Mwaikali kurejeshwa Dayosisi ya Konde Tukuyu, wachungaji wa majimbo matano kati ya saba wamepinga maagizo hayo.

Novemba 16, Dk Shoo alifanya ziara mkoani hapa kufuatia mgogoro wa kanisa hilo baada ya waumini kumtuhumu Askofu Dk Mwaikali kuhamishia mali za kanisa na kuzipeleka makao makuu ya Konde jijini Mbeya.

Katika kikao kilichofanyika Tukuyu, kikiwahusisha viongozi wa Serikali, akiwamo Kamanda wa Polisi Mkoa, Urlich Matei na Msajili wa jumuiya za dini kilicholenga kumaliza mgogoro huo, Dk Shoo aliagiza hadi kufikia Novemba 22 kiti cha Askofu kirejeshwe Dayosisi ya Tukuyu, ambapo wachungaji wameweka ngumu wakidai hawakufurahishwa na vitendo vya kiongozi huyo.

Wakizungumza jana jijini hapa kwenye kikao kilichohusisha wachungaji 67 kutoka majimbo matano kati ya saba, walisema hawakubaliani na uamuzi ya Dk Shoo kwa kuwa amelifedhehesha kanisa na viongozi wao.

Nyibuko Mwambola, mchungaji wa jimbo la Mbeya Mashariki alisema hawakubaliani na ubabe, uonevu na unyanyasaji aliofanyiwa Askofu Mwaikali.

Alisema hawakutarajia vyombo vya dola vitumike kuwalazimisha viongozi wa Dayosisi kufika kituo cha Polisi ili kukutana nao kwa mazungumzo badala ya kutumika kwa ofisi ya Dayosisi.

Agosti 22, 2021 waumini wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Tukuyu walifanya vurugu wakipinga Askofu Mwaikali kuhamisha mali za kanisa hilo kuzipeleka makao makuu ya Ruanda Mbeya hadi Jeshi la Polisi lilipoingilia kati.

2946335_1632893095129.png
 
Kkkt shame on you, mnayoyafanya ni ya kishetani na hayana utukufu kwa Mungu. Mtasambaratika kwa kuedekeza ushetani
 
Haki KKKT wanaongoza kwa mihogoro ya hapa na pale jamani, huku kwetu washapiganaga na fyombo fya Dola fikaja.

[emoji849][emoji120]Nasadiki kwa kanisa moja Katoliki Takatifu la Mitume, Naungama na ubatizo mmoja wa maondoleo ya Dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu na uzima wa milele ijayo!.

Sent from
 
Uzi ushaharibiwa hapa.

Wakatoliki bana

ukimaliza hapa kachangie redio Maria
Haki KKKT wanaongoza kwa mihogoro ya hapa na pale jamani, huku kwetu washapiganaga na fyombo fya Dola fikaja.

[emoji849][emoji120]Nasadiki kwa kanisa moja Katoliki Takatifu la Mitume, Naungama na ubatizo mmoja wa maondoleo ya Dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu na uzima wa milele ijayo!.

Sent from
 
Shoo ni mchaga mengine utajaza mwenyewe
Vipi ule mgogoro wa dayosisi ya pare uliishaje? Kkkt ni dhehebu linaloongoza kwa migogoro, bado juzi kati dayosisi ya kaskazini mashariki nako cheche zilifukuta. Tatizo wanakopi sana mambo ya siasa, Mungu ameawaacha wajiamulie wenyewe
 
Mwaikali amewachokoza wanyakyusa hilo bifu haliishi hadi atumbuliwe au ajiuzulu.
Ameingia chakike.
 
Mambo mengine ni kushangaza sana inakuwaje Kanisa lenye waumini wengi kujiendesha kama klabu ya pombe hukuna maelewano ni vurugu, tamaa ya mali hakuna uungu hapo.

Siku chache baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT), Dk Fredrick Shoo kuagiza kiti cha Askofu Dk Edward Mwaikali kurejeshwa Dayosisi ya Konde Tukuyu, wachungaji wa majimbo matano kati ya saba wamepinga maagizo hayo.

Novemba 16, Dk Shoo alifanya ziara mkoani hapa kufuatia mgogoro wa kanisa hilo baada ya waumini kumtuhumu Askofu Dk Mwaikali kuhamishia mali za kanisa na kuzipeleka makao makuu ya Konde jijini Mbeya.

Katika kikao kilichofanyika Tukuyu, kikiwahusisha viongozi wa Serikali, akiwamo Kamanda wa Polisi Mkoa, Urlich Matei na Msajili wa jumuiya za dini kilicholenga kumaliza mgogoro huo, Dk Shoo aliagiza hadi kufikia Novemba 22 kiti cha Askofu kirejeshwe Dayosisi ya Tukuyu, ambapo wachungaji wameweka ngumu wakidai hawakufurahishwa na vitendo vya kiongozi huyo.

Wakizungumza jana jijini hapa kwenye kikao kilichohusisha wachungaji 67 kutoka majimbo matano kati ya saba, walisema hawakubaliani na uamuzi ya Dk Shoo kwa kuwa amelifedhehesha kanisa na viongozi wao.

Nyibuko Mwambola, mchungaji wa jimbo la Mbeya Mashariki alisema hawakubaliani na ubabe, uonevu na unyanyasaji aliofanyiwa Askofu Mwaikali.

Alisema hawakutarajia vyombo vya dola vitumike kuwalazimisha viongozi wa Dayosisi kufika kituo cha Polisi ili kukutana nao kwa mazungumzo badala ya kutumika kwa ofisi ya Dayosisi.

Agosti 22, 2021 waumini wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Tukuyu walifanya vurugu wakipinga Askofu Mwaikali kuhamisha mali za kanisa hilo kuzipeleka makao makuu ya Ruanda Mbeya hadi Jeshi la Polisi lilipoingilia kati.
MIGOGORO NI SEHEMU YA MAISHA YA BINADAMU NA TAASISI. MTU ANAYESHANGAA KUWEPO KWA MIGOGORO ANAPUNGUKIWA UELEWA WA MAMBO. MIGOGORO HATA ENZI YA YESU ILIKUWEPO, NA HATA KUTUNDIKWA KWAKE MSALABANI NI SEHEMU YA MIGOGORO.
 
Aisee mgogoro ya kugombea mali, kanisa linatakiwa kuongozwa kwa Amani,Upendo, Unyenyekevu na hofu ya Mungu utawafindisha nini waumini wenu ikiwa viongozi wanaroho za kishetani kugombeania mali?

Kujibu kwamba hata wakati wa Yesu mgogoro ilikuwepo ni ufinyu wa fikra Yesu alilongoza kanisa kwa amani upendo na unyenyekevu akaacha kilelezo ili wakifuate, pia kuwepo kwa migogoro haihalalishi ns nyie kuwa na migogoro.

Kwanini migogoro yenu inakuwa ni mambo ya mali?
 
Hawa Maaskofu kipindi wakiwa ktk daraja la Uchungaji wanakuwa watumishi na viongozi wa kiroho kwa baadhi balaa huanza baada ya kupanda na kupata daraja la Uaskofu, hugeuka na kuwa watawala na si watumishi tena na maamuzi na mipango yao hujaa siasa siasa.

Sasa kama huyu Askofu sijasikia kama aliomba radhi kwa wakristo na watenda kazi wenzake kwa usumbufu aliouleta kwa kung'ang'ania kuhama, hasa baada ya viongozi wake wa juu kubatilisha maamuzi yake. Biblia inahimiza watu kutafuta amani na utakatifu, hawa viongozi wakubwa kabisa ktk makanisa ndio vinara wa kuanzisha migogoro, chuki, watu wanaongoza zaidi kwa maneno na si kwa matendo. Ndio maana viongozi wa dini wenye ujasiri wa kukemea mambo yasiyofaa yanayofanywa na viongozi wa serikali na kada nyingine wako wachache.
Mungu atuhurumie.
 
Mambo mengine ni kushangaza sana inakuwaje Kanisa lenye waumini wengi kujiendesha kama klabu ya pombe hukuna maelewano ni vurugu, tamaa ya mali hakuna uungu hapo.

Siku chache baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT), Dk Fredrick Shoo kuagiza kiti cha Askofu Dk Edward Mwaikali kurejeshwa Dayosisi ya Konde Tukuyu, wachungaji wa majimbo matano kati ya saba wamepinga maagizo hayo.

Novemba 16, Dk Shoo alifanya ziara mkoani hapa kufuatia mgogoro wa kanisa hilo baada ya waumini kumtuhumu Askofu Dk Mwaikali kuhamishia mali za kanisa na kuzipeleka makao makuu ya Konde jijini Mbeya.

Katika kikao kilichofanyika Tukuyu, kikiwahusisha viongozi wa Serikali, akiwamo Kamanda wa Polisi Mkoa, Urlich Matei na Msajili wa jumuiya za dini kilicholenga kumaliza mgogoro huo, Dk Shoo aliagiza hadi kufikia Novemba 22 kiti cha Askofu kirejeshwe Dayosisi ya Tukuyu, ambapo wachungaji wameweka ngumu wakidai hawakufurahishwa na vitendo vya kiongozi huyo.

Wakizungumza jana jijini hapa kwenye kikao kilichohusisha wachungaji 67 kutoka majimbo matano kati ya saba, walisema hawakubaliani na uamuzi ya Dk Shoo kwa kuwa amelifedhehesha kanisa na viongozi wao.

Nyibuko Mwambola, mchungaji wa jimbo la Mbeya Mashariki alisema hawakubaliani na ubabe, uonevu na unyanyasaji aliofanyiwa Askofu Mwaikali.

Alisema hawakutarajia vyombo vya dola vitumike kuwalazimisha viongozi wa Dayosisi kufika kituo cha Polisi ili kukutana nao kwa mazungumzo badala ya kutumika kwa ofisi ya Dayosisi.

Agosti 22, 2021 waumini wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Tukuyu walifanya vurugu wakipinga Askofu Mwaikali kuhamisha mali za kanisa hilo kuzipeleka makao makuu ya Ruanda Mbeya hadi Jeshi la Polisi lilipoingilia kati.

Pale Nyumba Ya Sara Inapogeuzwa Pango La Wanyang'anyi
 
Back
Top Bottom