Hawa Maaskofu kipindi wakiwa ktk daraja la Uchungaji wanakuwa watumishi na viongozi wa kiroho kwa baadhi balaa huanza baada ya kupanda na kupata daraja la Uaskofu, hugeuka na kuwa watawala na si watumishi tena na maamuzi na mipango yao hujaa siasa siasa.
Sasa kama huyu Askofu sijasikia kama aliomba radhi kwa wakristo na watenda kazi wenzake kwa usumbufu aliouleta kwa kung'ang'ania kuhama, hasa baada ya viongozi wake wa juu kubatilisha maamuzi yake. Biblia inahimiza watu kutafuta amani na utakatifu, hawa viongozi wakubwa kabisa ktk makanisa ndio vinara wa kuanzisha migogoro, chuki, watu wanaongoza zaidi kwa maneno na si kwa matendo. Ndio maana viongozi wa dini wenye ujasiri wa kukemea mambo yasiyofaa yanayofanywa na viongozi wa serikali na kada nyingine wako wachache.
Mungu atuhurumie.