Aibu ya pombe

Aibu ya pombe

Masunula

Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
98
Reaction score
95
Heri ya krismasi na mwaka mpya,nilikua mnywaji mkubwa wa pombe ila baada ya kushauriwa na kuona inaniletea matatizo nikaamua niiache.

Juzi siku ya boxing day nikatoka na washkaji hadi mtaa wa mbali kidogo ila nafahamika nikasema nikumbushie kidogo pombe.

Matokeo yake nilikunywa kupitiliza nikagombana na kila mtu hata wale wakubwa nnaowaheshimu mbaya zaidi hata kurudi nyumbani nilishindwa nikalala kwenye pagala.Naona aibu kutoka hata nje kwa nilichokifanya.MSAADA Nijinsi gani naweza rejesha heshima yangu na kuiacha pombe kabisa?
 
Back
Top Bottom