Aibu: Ziara ya Waziri Mkuu Tunduma yageuka Mkutano wa Kampeni, Silinde na Mwambe wahutubia

Aibu: Ziara ya Waziri Mkuu Tunduma yageuka Mkutano wa Kampeni, Silinde na Mwambe wahutubia

Hapo ndipo CCM Mpya waelewe gharama za kuendekeza utashi wa mtu mmoja bila kuwashirikisha wananchi wanataka nini ktk maeneo yao yawe Maendeleo ya Vitu au Maendeleo ya Watu lazima kuwa msikivu kwa wabunge na wananchi hitaji lao lenye kipaumbele ni lipi badala ya kuwaburuza.
Tegemeo la ccm ni polisi pekee
 
Yaani katika wabunge waliounga juhudi kifala ni Lijualikali na Silinde,mbwembwe nyingi utafikiri wameahidiwa uzima wa milele,naamini wakiwa wametulia wanajuta sana kwa maamuzi waliyoyafanya ila hawana namna inabidi wakaze uzi tu.
Aibu kubwa sana !
 
Muda utawashitaki yaani walivyo wepesi bila polisi hakuna CCM imara
 
Tunaposema CCM imekufa huwa hatubahatishi, Mh Kasimu Majaliwa ambaye yuko Tunduma kwa kinachoitwa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya Mji wa Tunduma, hatimaye ametimiza kile kilichompeleka hasa ambacho ni kutafuta uwanja wa Msaliti Silinde kuhutubia baada ya kubainika kwamba, kwa sasa Silinde hana uwezo wa kukusanya hata watu 50 kwenye mkutano wa hadhara.

Hii yaweza kuwa aibu kwa mtu mzito kama Waziri Mkuu kutengeneza ziara ya kinafiki ili kuwapa uwanja wa kuhutubia wasaliti waliohama vyama vyao baada ya kununuliwa. Kama Silinde aliwadanganya kwamba yeye ni maarufu hadi mkamlipa pesa ya uchakavu kuna haja gani tena ya kutumia ziara za kiserikali ili kumbeba?

Juzi Mwakajoka amehutubia mwenyewe bila mamluki yeyote, kwanini Silinde naye asifanye hivyo ?
Mmmh! sisi wengine tusio na mavyama vyama sijui tuwe tunajificha wapi! Huyo mtu mmemfukuza wenyewe kwenye chama chenu na mkatangaza wenyewe kwenye vyombo vya habari kwa majigambo. Sasa kaamua kujiunga na CCM kuendelea na taaluma yake ya siasa halafu wewe unatuletea story za ooh kanunuliwa! Kivipi?? Kama kwamba kila mtu atakayesoma uzi wako ni mjinga wa kufikiri kiasi hicho. I mean, seriously???
 
Chadema kwa kulialia , subiri kiama chenu mwaka huu yani tulivyopania!

Ni kweli nyinyi tume ya uchaguzi na vyombo vya dola mmepania sana, na mwenyekiti wenu kwa kofia ya urais ameshatoa maagizo kabisa mtangazwe washindi.
 
Humphrey Polepole alikuwapo juzi Tunduma lakini aliona dhahiri mkoa wa Songwe mambo magumu akakimbia. Sera za Maendeleo ya Vitu ya Dar es Salaam aliyosema Polepole kusuhu flyover , madaraja ya baharini, ndege na meli haziuziki Tunduma. Tunduma wanataka Maendeleo ya Watu .

Kwa kwa watu wa Tunduma ndio nguzo ya taifa tunawafahamu hao hakuna mchezo safi sana fukuza polepole na ujinga wake
 
Ni kweli nyinyi tume ya uchaguzi na vyombo vya dola mmepania sana, na mwenyekiti wenu kwa kofia ya urais ameshatoa maagizo kabisa mtangazwe washindi.
Mkuu hicho kitu kitapasua hii nchi mwaka huu , polisi wamechoka sana kutumika
 
6 Julai 2020
Tunduma, Tanzania

Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa afika Tunduma
Waziri Shonza aelezea hali ya kisiasa ilivyo Momba ambapo upinzani wanashikilia hatamu za uongozi kwa ridhaa ya wananchi

Source : Jay TV
 
6 Julai 2020
Tunduma, Tanzania

Majaliwa: maendeleo yapo kwenye vidole vyenu
ashangazwa na umati wa watu katika mkutano wao na kuwaomba watumie vidole vyao vizuri. Maana katika ziara zake zote hajapata kuona umati mkubwa Tanzania ukijitokeza kama katika mkutano wa Tunduma.

Waziri Mkuu azungumzia hospitali kubwa inayojengwa kwa awamu kwa gharama ya bajeti ya Tshs. 15.0 bilioni

Source : Jay TV
 
5 Julai 2020

CCM NYANDA ZA JUU KUSINI : Tumechoka kuongozwa na upinzani

Source : MbeyaYetuOnlineTV
 
Tunduma na Mbeya mjini mtake msitake,Mtaongozwa na CCM
 
6 Julai 2020
Tunduma, Tanzania

Majaliwa: maendeleo yapo kwenye vidole vyenu
ashangazwa na umati wa watu katika mkutano wao na kuwaomba watumie vidole vyao vizuri. Maana katika ziara zake zote hajapata kuona umati mkubwa Tanzania ukijitokeza kama katika mkutano wa Tunduma.

Waziri Mkuu azungumzia hospitali kubwa inayojengwa kwa awamu kwa gharama ya bajeti ya Tshs. 15.0 bilioni

Source : Jay TV

Hatimaye Majaliwa naye aanza siasa za kishamba
 
Julai 2020
Tunduma, Tanzania

MWAKAJOKA Atikisa Tunduma
"Mkutano wa kuwashukuru Wananchi "CHADEMA Tutashinda Uchaguzi Majimbo Yote 2020 .

Mfano Chipaka tenki la maji na matenki mengine yatasambaza huduma ya maji safi kwa wote.

Elimu mji wa Tunduma imezidi kuboreshwa

Mbunge wenu mimi Mwakajoka nimetambuliwa ktk hansard ya bunge kama mchangiaji bora aliyeshika namba 7 ktk bunge la Muungano wa Tanzania kuwatetea wakulima, wafugaji, wavuvi na watumishi wa umma siyo Tunduma tu bali pia kuwatetea waTanzania wote. Kiasi Spika Job Ndugai akawa anaomba nipunguze mbinyo kuibana serikali lakini mimi kama Mwakajoka nilikuwa sielewi wala kuchoka kulibana bunge la Ndugai na serikali ya CCM Mpya.

Michezo ni afya na ajira mfano Mwakajoka Cup imesaidia kutoa burudani na kutoa vijana 3 waliochaguliwa kwenda under 17 timu ya taifa ya Tanzania ya soka.

Mfuko wa jimbo 95 milioni kila kata imenufaika kufuatana na mahitaji ya kila sehemu.

Vituo vya Afya pia vimeboreshwa kutoa huduma kwa Mama na Mtoto pia vijana na kina baba.
Source : JAY TV

Tuseme tu ukweli, Tunduma watu wanajitambua sana. CCM na Silinde wana wakati mgumu sana!
 
L
Humphrey Polepole alikuwapo juzi Tunduma lakini aliona dhahiri mkoa wa Songwe mambo magumu akakimbia. Sera za Maendeleo ya Vitu ya Dar es Salaam aliyosema Polepole kusuhu flyover , madaraja ya baharini, ndege na meli haziuziki Tunduma. Tunduma wanataka Maendeleo ya Watu .

L

Hapo bavicha matimbo joto, wanapishana tu vichakani kwa mhalo😅😅😅😅😅
 
Tuseme tu ukweli, Tunduma watu wanajitambua sana. CCM na Silinde wana wakati mgumu sana!

Umati huo wa wanaTunduma unawatizama tu hao viongozi makada wa CCM Mpya wa kuletwa na CCM kuongoza wilaya na mikoa RC , DC, RAS , DAS , DED wakiwasanifu lakini siku ya kupiga kura wanafanya kweli kwa kuchagua upinzani.

Pia Majaliwa ameonesha kutowaamini hata wanaCCM makundi ambao wanawapigia kura zao za siri kuchagua upinzani Oktoba 2020.
 
Majaliwa anajidhalilisha sana na michezo hii ya kishamba!
 
Back
Top Bottom