Aida Kenani: CHADEMA inaonewa sana, kama haumuitaki ifuteni tu

Aida Kenani: CHADEMA inaonewa sana, kama haumuitaki ifuteni tu

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Aliyekuwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA, Aida Kenan asema kama vya vyama vya upinzani havitakiwi nchini ni bora kuvifuta vyote ili watu wasiendelee kuuawa na kuumizwa na kibaki chama tawala tu.

 
Yes Afrika tumeuana sana kwa sababu ya maigizo ya demokrasia. Bora turudi chama kimoja tupinduane tu kijeshi ndio tunachoweza na pengine tungeheshimiana kuliko hivi sasa ambapo upande mmoja ndio una bunduki unaamua kuua wenzao wasio na bunduki kisa tu ni chama mbadala.

Imagine watu 10,000 wameuwawa ili tu mtu mmoja akae ikulu!! Hivi waafrika tuna laana gani
 
Nchi ikishaongozwa na kilaza mambo mengi ya hovyo hufanyika, haishangazi.. rais aliyefeli matokeo ya form 4 kwa kuambulia D moja tuu huwezi tegemea miujiza yoyote kutoka kwake!.
 
CCM hawajawahi kuwa tayari kwa siasa za vyama vingi. Marekebisho ya sheria na katiba yamefanywa kwa kuzingatia ni lazima CCM iendelee kubaki madarakani.

Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ipo kuhakikisha vyama vya upinzani havipati haki sawa na CCM.
 
Huyu Kenani sijawahi kumfuatilia sana ila toka nimeanza kumsikia kuna kitu kinamkataa ila bado sijajua ni nini.

Kauli kama "tumefungiwa tumekubali" ina maana gani? Mwisho katika mahojiano haya ukisikia anavyomuongelea Samia, kuna kitu utajiuliza kama fikra zako bado zinachaji.

Wamepita wengi wa aina hii CHADEMA, kuweni macho.
 
Nchi ikishaongozwa na kilaza mambo mengi ya hovyo hufanyika, haishangazi.. rais aliyefeli matokeo ya form 4 kwa kuambulia D moja tuu huwezi tegemea miujiza yoyote kutoka kwake!.
Bora aliyefeli form 4 lkn kwa sasa wenye vyeti wote wako chini kuliko mliosoma lkn hamna uwezo wa kumtoa Madarakani
 
Back
Top Bottom