Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Uwakilishi bubu una faida gani? Atasikilizwa na nani bungeni akiwa peke yake? Hatakuwa na uwezo wa kupinga lolote lile liletwalo bungeni, sioni faida yeyote ile zaidi ya mafao tu!
uwakilishi bubu kivipi?walivyokuwa wengi walisikilizwa?suala la mafao na fursa zinazojitokeza kwa nafasi aliyoipata ndio sababu kubwa wanasiasa wote wanasukumwa kugombea nafasi mbali mbali, kisha yanafuatia waslahi ya wanaowakilishwa...haikumake difference walivyokuwa wengi
 
Uchaguzi ungekuwa huru na haki,sehemu nyingi CCM wangelambishwa mchanga kama jimboni kwa Aida.
 
Huyo dada kwangu akienda bungeni ni sawa, na akiamua kusimamia msimamo wa chama ni sawa. Cha muhimu akiwa bungeni asigeuzwe kondoo wa kutii mambo ya ccm. Tena kuna uwezekano wa kuwashinda kwa hoja hao viazi wengi wa ccm.
 
Uchaguzi ulikuwa huru na haki, tumuunge mkono mbakaji mkuu atakapoanza kumbaka mwananchi mmoja mmoja.
 
..huyu dada aende bungeni.

..yeye na wananchi waliomchagua wameutolea jasho ushindi huo.

..kushiriki kwake bungeni hakuondoi ukweli kuhusu dhuluma kubwa iliyotokea ktk uchaguzi mkuu.
👍👍
 
Uwakilishi bubu una faida gani? Atasikilizwa na nani bungeni akiwa peke yake? Hatakuwa na uwezo wa kupinga lolote lile liletwalo bungeni, sioni faida yeyote ile zaidi ya mafao tu!
Haaaa! Kumbe Mjengoni mnaendaga kupinga tuu, na wala siyo kuisimamia serikali na kuwawakilisha wananchi wa majimbo yenu? Hapa ndipo maana halisi ya JPM ya "CONNECTION" inatiki!
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote

Kwakweli wamuache naye akale maisha maana hata akijiuzulu hakuna itakacho badilika. Ingekuwa wamepita viongozi je wangejiuzuru? Jibu ni hapana, hivyo mama naye acha akale mema ya nchi.
 
We are here supporting u mpambanaji.. Thanks kwa kuwatendea haki wapiga kura wako. Achana na kina salum mwalim ambao kisa wamekosa wanataka mkose wote
 
Sasa huyo mmoja ndio atabadilisha picha halisi ya hilo Bunge?

Kumbe nafsi zinawsuta kuona mmebaki peke yenu!!
Bora kabisa ata mlivyopata hivyo viti viwili tu.
Bunge lililopita mmetusumbua sana kuitisha uchaguzi kila mara sababu tu ya kukosa kwenu msimamo na kuishia kuunga juhudi.
Kwa sasa walau nchi italuia.
 
Huyo dada kwangu akienda bungeni ni sawa, na akiamua kusimamia msimamo wa chama ni sawa. Cha muhimu akiwa bungeni asigeuzwe kondoo wa kutii mambo ya ccm. Tena kuna uwezekano wa kuwashinda kwa hoja hao viazi wengi wa ccm.

..100%.

..anaweza ku-protest mambo ya hovyo akiwa ndani ya bunge.

..na usije ukashangaa ccm wakawa wanamhitaji huyu dada kuwasilisha mawazo mbadala.

..kuwepo kwake bungeni hakumzuii kushiriki harakati za chama chake kupinga dhuluma.
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote

Watu wanafikiri definition ya democrasia ni mpaka chadema wachaguliwe
 
Huyu dada aende bungeni yeye na wananchi waliomchagua wameutolea jasho ushindi huo.

Kushiriki kwake bungeni hakuondoi ukweli kuhusu dhuluma kubwa iliyotokea ktk uchaguzi mkuu.
Tatizo ni Mbowe anaona mshahara wa mtu mmoja haumtoshi alizoea kuwakamua mabillion Sasa akichukua laki 5 toka huyu mbunge mmoja haitoshi ndo maana anatapatapa eti uchaguzi urudiwe.
 
Tatizo ni Mbowe anaona mshahara wa mtu mmoja haumtoshi alizoea kuwakamua mabillion Sasa akichukua laki 5 toka huyu mbunge mmoja haitoshi ndo maana anatapatapa eti uchaguzi urudiwe.

..sidhani kama ni kweli.

..Haiwezekani kumchangisha mbunge mmoja.

..Kwa hiyo akienda bungeni, au asipokwenda bungeni, hakuna tofauti yoyote ktk mfuko wa michango wa chama.
 
Back
Top Bottom