Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Nina hakika kuwa njia sahihi kwa CUF CHADEMA +ACT ni kutumia mahakama zetu JIMBO KWA JIMBO kwa kesi zenye ushahidi wa election irregularities hata ziwe 250 na nina hakika kwa quality ya WANASHERIA mliopo kwenye vyama na supporters wa haki mtashinda walau kesi 30.

Waacheni walioshinda waende BUNGENI kama ALAMA YA KIHISTORIA na muwape support katika kujenga hoja maana wao watakuwa na immunity na ninyi mtapigana underground kwa maana philosophically .....there is a victory of GOOD over evil OF JUSTICE over injustiuces and of the TRUTH over falsehood
 
Maendeleo hayana chama! Mbunge Mteule anapigania wananchi pamoja na maisha yake.
Jimbo lake litakosa maendeleo afanye kama walivyofanya akina mtulia aunge juhudi uchaguzi urudiwe jimboni kwake ccm itamteua kugombea bila kushindanishwa. Namkumbusha yeye ni gunzi ktk mabetri
 
Kama uchaguzi hautarudiwa sioni mantiki ya yeye kukubali wazo la kukataa ubunge, kawakilishe wananchi wako...huku tukiipambania demokrasia...ana familia na maisha ya kuishi licha ya gharama alizotumia
Wazo la kukataa lilikuwa la kijinga sana sijui ni nani aliye toa wazo kama ni Mbowe basi ni msiba mzito , wananchi ni zaid ya chama
 
..100%.

..anaweza ku-protest mambo ya hovyo akiwa ndani ya bunge.

..na usije ukashangaa ccm wakawa wanamhitaji huyu dada kuwasilisha mawazo mbadala.

..kuwepo kwake bungeni hakumzuii kushiriki harakati za chama chake kupinga dhuluma.

Shida ni kuwa kwa vyovyote vile ataonekana anatumika. Chochote atakachofanikiwa kupeleka kwenye jimbo lake itaonekana kama ni shukrani kwa kutofautiana na msimamo wa chama chake.

Ingawa ataweza kweli kujitahidi ku-protest lakini atageuziwa kibao kuwa kuwepo kwake ni ishara tosha kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na wazi.

Hilo la kutumika kama conduit ya wabunge wa Chama Tawala kuwasilisha mawazo mbadala ni kibaya zaidi maana atakuwa anasaidia kuficha nyufa katika Chama hicho. Inatakiwa kama kuna mbunge ana mawazo mbadala asimame na ayatoe mwenyewe, sio ajifiche nyuma ya gauni la huyu dada. Huo utakuwa unafik wa hali ya juu.

Kwa vile chama chake kimetangaza kutotambua uhalali wa uchaguzi wote basi kwa vyovyote hakitampa ushirikiano katika harakati zake zozote. Itafika wakati atakuwa hana jinsi bali kuhamia upande wa pili.

Mwisho, kazi ya mbunge sio tu kuwakilisha wananchi wa jimbo lake bali pia kusimamia serikali kwa kutoa msimamo mbadala kwa masuala yote yatakayowasilishwa na serikali ikiwa pamoja na bajeti. Akiwa peke yake au wawili sijui atawezaje kuchambua bajeti ya serikali na wizara yake na misuada kibao ya sheria itakayowasilishwa bila kupata msaada wa chama chake. Na atapata wapi uhalila wa kusimama bungeni na kuyawasilisha kama ndio msimamo wa chama chake?

Huyu dada kweli amewekwa mahali pabaya na chochote atakachofanya ataonekana msaliti. Akikubali kuapishwa ataonekana msaliti kwa chama chake na akikataa ataonekana amewasiliti wale waliompigania ili atangazwe kuwa ameshinda. Ushauri wangu kwake ni kuwa aombe ushauri wa waliompigania, na kama watamwambia akubali kuapishwa, atakuwa na nguvu zaidi ya kuwaambia viongozi wake katika chama kuwa ni utashi wa wanachama wao wa Nkasi na sio wa kwake yeye. Wakimkatalia, basi afanye maamuzi magumu mapema ya kuhamia upande wa pili. Bila shaka atashinda uchaguzi wa marudio maana atakuwa ameondoka na wale wa chama chake cha sasa waliompigia kura.

Amandla...
 
Safi sana, Mungu akubariki, ...
Kumbe mmeshaona tatizo la bunge la chama kimoja 100% Hii karata ilichangwa vibaya, ilibidi muachie kama watano hivi ili wavutane wenyewe. Bakini wenyewe mjadili vizuri maendeleo bila hawa wanaorudisha nyuma maendeleo.
 
Shida ni kuwa kwa vyovyote vile ataonekana anatumika. Chochote atakachofanikiwa kupeleka kwenye jimbo lake itaonekana kama ni shukrani kwa kutofautiana na msimamo wa chama chake.

Ingawa ataweza kweli kujitahidi ku-protest lakini atageuziwa kibao kuwa kuwepo kwake ni ishara tosha kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na wazi.

Hilo la kutumika kama conduit ya wabunge wa Chama Tawala kuwasilisha mawazo mbadala ni kibaya zaidi maana atakuwa anasaidia kuficha nyufa katika Chama hicho. Inatakiwa kama kuna mbunge ana mawazo mbadala asimame na ayatoe mwenyewe, sio ajifiche nyuma ya gauni la huyu dada. Huo utakuwa unafik wa hali ya juu.

Kwa vile chama chake kimetangaza kutotambua uhalali wa uchaguzi wote basi kwa vyovyote hakitampa ushirikiano katika harakati zake zozote. Itafika wakati atakuwa hana jinsi bali kuhamia upande wa pili.

Mwisho, kazi ya mbunge sio tu kuwakilisha wananchi wa jimbo lake bali pia kusimamia serikali kwa kutoa msimamo mbadala kwa masuala yote yatakayowasilishwa na serikali ikiwa pamoja na bajeti. Akiwa peke yake au wawili sijui atawezaje kuchambua bajeti ya serikali na wizara yake na misuada kibao ya sheria itakayowasilishwa bila kupata msaada wa chama chake. Na atapata wapi uhalila wa kusimama bungeni na kuyawasilisha kama ndio msimamo wa chama chake?

Huyu dada kweli amewekwa mahali pabaya na chochote atakachofanya ataonekana msaliti. Akikubali kuapishwa ataonekana msaliti kwa chama chake na akikataa ataonekana amewasiliti wale waliompigania ili atangazwe kuwa ameshinda. Ushauri wangu kwake ni kuwa aombe ushauri wa waliompigania, na kama watamwambia akubali kuapishwa, atakuwa na nguvu zaidi ya kuwaambia viongozi wake katika chama kuwa ni utashi wa wanachama wao wa Nkasi na sio wa kwake yeye. Wakimkatalia, basi afanye maamuzi magumu mapema ya kuhamia upande wa pili. Bila shaka atashinda uchaguzi wa marudio maana atakuwa ameondoka na wale wa chama chake cha sasa waliompigia kura.

Amandla...

..nakubaliana na hapo unaposema kwamba awashirikishe WANANCHI waliompigania mpaka akawa mbunge.
 
Sasa huyo mmoja ndio atabadilisha picha halisi ya hilo Bunge?

Kumbe nafsi zinawsuta kuona mmebaki peke yenu!!
Wanapata taabu sana. Watakosa wa kuwarushia ngumi. Sasa mmoja atatosha kurusha mipasho. Pia wa kumrushia mipasho anafaa awe anajibu, sasa sidhani kama huyu ni wale wa kujibu. Tunalisubiri hilo bunge, tena liwe live maana wale wa kuwarudisha nyuma kwenye maendeleo hawapo Bungeni.
 
Kawaza mbali na kaamua maamuzi mazuri sana.
Ukweli umetumwa kazi na watu wa Nkasi Kaskazini hayo mengine ni ubabaishaji nenda ukapige kazi.
Ukifanya utani ubunge utausikia kwenye redio.
 
..nakubaliana na hapo unaposema kwamba awashirikishe WANANCHI waliompigania mpaka akawa mbunge.
Kwa hiyo unaamini kuwa ataweza kuwakilisha kikamilifu kambi ya upinzani? Yeye na yule dada wa Mtwara? Na kama hataweza, hatakuwa na tofauti na wabunge wa Chama tawala ambao kazi yao kubwa ni kuwakilisha majimbo yao na sio kuisimamia serikali.

Binafsi, sioni namna ambayo Chadema watakubali awawakilishe hasa ukiangalia wakati huu ambao viongozi wao ( Mbowe, Lema, Boniface, Makamba, wale wa Bavicha na wafuasi wao kibao) wakiwa wako ndani na wanakabiliwa na mashtaka makubwa ya jinai. Hawataeleweka.

Amandla....
 
Hana sehemu ya kuponea zaidi ya ubunge na CCM wamemchagua huyu wakijua hata elimu yake ni haba sana mwaka jana alikuwa form four resetter kwahiyo wanajua hatawasumbua.
Huyu dada hana CV hata ya mistari sita.
 
Kwa hiyo unaamini kuwa ataweza kuwakilisha kikamilifu kambi ya upinzani? Yeye na yule dada wa Mtwara? Na kama hataweza, hatakuwa na tofauti na wabunge wa Chama tawala ambao kazi yao kubwa ni kuwakilisha majimbo yao na sio kuisimamia serikali. Binafsi, sioni namna ambayo Chadema watakubali awawakilishe hasa ukiangalia wakati huu ambao viongozi wao ( Mbowe, Lema, Boniface, Makamba, wale wa Bavicha na wafuasi wao kibao) wakiwa wako ndani na wanakabiliwa na mashtaka makubwa ya jinai. Hawataeleweka.

Amandla....

..hana historia ya kuwa mpambanaji kiasi cha kutegemewa awe jeshi la mtu mmoja ndani ya bunge.

..chadema wasitengeneze mgogoro naye ambao utaondoa focus na attention ktk kupinga dhuluma iliyotokea wakati wa uchaguzi.

..hataeleweka kwa kipindi kifupi, lakini vilevile anaweza kufunikwa na kusaulika kwa haraka ndani ya bunge. ila atasaidia kuwaweka pamoja wanachama wa chadema ktk eneo anakotoka.
 
Kama Zitto na Mbowe wangeshinda/wangeachiwa kupenya Ubunge, most likely wangeingia bungeni kwa kisingizio cha “kwenda kupigania haki kwa maslahi mapana ya Nchi”

Aida kwenda Bungeni haitoondoa ukweli kwamba CCM na NEC yao wamenajisi uchaguzi huu.
 
..hana historia ya kuwa mpambanaji kiasi cha kutegemewa awe jeshi la mtu mmoja ndani ya bunge.

..chadema wasitengeneze mgogoro naye ambao utaondoa focus na attention ktk kupinga dhuluma iliyotokea wakati wa uchaguzi.

..hataeleweka kwa kipindi kifupi, lakini vilevile anaweza kufunikwa na kusaulika kwa haraka ndani ya bunge. ila atasaidia kuwaweka pamoja wanachama wa chadema ktk eneo anakotoka.

Kwa hiyo basically Chadema wamuache afanye atakachoamua bila kusisitiza one way or the other.

Kama ameweza kupambana mpaka akatangazwa ( kama haikuwa ni token tu) anaweza kuwashangaza watu kwa kugeuka mpambanaji mzuri nje ya kivuli cha wakina Mdee.

Aachwe akaape tu. Kama unavyosema waliompigania wata appreciate hiyo gesture. Na kama kuna mtu kutoka Chama Tawala atajaribu kumtumia kama conduit awataje waziwazi.

Better still, anaweza kugeuza kibao na kusema yuko pale under protest kwa hiyo anawakilisha jimbo lake na sio chama chake. Kwa mntik hiyo, hata akipewa u KUB akatae.

Amandla...
 
Hana sehemu ya kuponea zaidi ya ubunge na CCM wamemchagua huyu wakijua hata elimu yake ni haba sana mwaka jana alikuwa form four resetter kwahiyo wanajua hatawasumbua.
Huyu dada hana CV hata ya mistari sita.
Duuuuu.. Ahamie tu huko kwao wa kijani, aungane nao waimbe mapambio pamoja.
 
Kwa hiyo basically Chadema wamuache afanye atakachoamua bila kusisitiza one way or the other.

Kama ameweza kupambana mpaka akatangazwa ( kama haikuwa ni token tu) anaweza kuwashangaza watu kwa kugeuka mpambanaji mzuri nje ya kivuli cha wakina Mdee.

Aachwe akaape tu. Kama unavyosema waliompigania wata appreciate hiyo gesture. Na kama kuna mtu kutoka Chama Tawala atajaribu kumtumia kama conduit awataje waziwazi.

Amandla...

..it is a very tricky situation.

..Chadema wakianza kugombana naye, Ccm hawatapoteza muda kumchukua na kumtumia dhidi ya Chadema.

..Ndio maana napendekeza Chadema waende naye taratibu na waepushe migogoro naye.
 
Sasa huyo mmoja ndio atabadilisha picha halisi ya hilo Bunge?

Kumbe nafsi zinawsuta kuona mmebaki peke yenu!!
Hivi mnashindwa hata kuuliza muelimishwe. Nani amekwambia cdm wana mbunge mmoja?

Ipo hivi, hata Chadema wasingeshinda jimbo lolote, kwa kufikisha 18% ni zaidi ya 5% ya kula zote, tayari wana wabunge wa kuteuliwa. Kwa haraka haraka, chadema watakuwa na wabunge zaidi ya 10 wa kuteuliwa + na huyo mmoja.

ACT wana wabunge kama wanne tu wa kuchaguliwa na CUF wana wabunge 3. So hizo akili zenu kuwa hakutakuwa na wabunge wa upinzani ni utopolo mtupu. Kinacho piganiwa kwa sasa ni maslahi ya kina Mbowe tu.
 
Uyo jamaa kiongozi wa ACT alitaka kumwaga mboga na ugali kwaujumla jamaa wakamuwai kwa kumpiga bega aache.
 
Back
Top Bottom