Aina gani ya friji ni nzuri?

Go for LG utaja nishukuru, pamoja na kwamba ni ghali lkn hakika wana chombo, mi nlinunua langu size ya kati tokea 2016 mpaka leo na sijawahi kujuta, ni energy efficient, hakuna kuweka mabonge ya barafu kule juu, inagandisha chap pia, lkn kwa muonekano ni Urembo ndani
 
WestPoint is the best.
 
hivi tofauti ya fridge na freezer ni nini?
 
Nina von ina miaka mi 5 sasa na ipo vizuri
 
Ninatumia boss wapo vzuri sana! Aigandishi mabarafu upande wa freezer, inatumia umeme kidgo sana na haina kelele
 
Nilienda kariakoo kununua friji nikaacha friji jipya kampuni ya boss lenye lita 100 kwa 360,000 nikaenda kununua la mtumba lenye lita 168 kwa bei hiyo hiyo kampuni ya whirlpool nimekaa nalo mwaka mmoja tu sasa hivi linawaka haligandishi halipoozi hata uliwashe masaa 24 yani ni bora ukanunua jipya ukaja kulibikiri mwenyewe hata kama ni chinese brand
 
Tafuta LG au Fresh Tech
 
Ina maana deep freezer ndogo la og Bei gani ?
 
Njoo tukujulishe
Friji ni Westpoint, Samsung, lg , sharp , hisense make sure uko kwa authorised dealer, ila zote hizo ni global brand so bei yake ni kisu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…