Aina tano za pesa zenye nguvu duniani...WHY

Kitu gani kinafanya pesa iwe na thamani? Hili swali nimejiuliza, mf; Zambia iliongeza thanani ya pesa yake sina uhakika na figure but ni kama elf moja wakaifanya iwe tsh moja. Je ukifanya hivyo hata kwa shilongi utasema pesa yetu inathamani kwa ulinganisho uliofanya?
 
Aliyeanzisha mada halewi sana nini maana ya fedha kuwa na nguvu

Ili fedha iwe na nguvu lazima uangalie je inakubalika kwa matumizi kiasi gani worldwide?

Au kwa lugha rahisi je mzunguko wa fedha ni mkubwa kiasi gani duniani?

Kwa maana hii US dollar ndiyo fedha yenye nguvu zaidi.
 
Serikali kupitia central bank wakiamua kupandisha au kushusha thamani ya fedha wanafanya hivyo purposefully.

Kwa mfano central bank inashusha thamani ya fedha ili kusaidia kuuza zaidi bidhaa nje. Hapa wanunuzi toka nje wanashawishika kwasababu wananunua bei nafuu

Kadhalika central bank ikiongeza thamani ya fedha inasaidia nchi husika kununua bidhaa nje kwa unafuu

Lakini yote hayo kupandisha/kushusha thamani ya fedha kama nilivyosema yanafanyika purposefully na ni kwamuda tu

Ili fedha iwe na thamani isiyoyumba inabidi nchi iwe inauza bidhaa nyingi nje ili ipate fedha za kigeni nyingi zaidi. Na hii ndiyo inaipa nguvu sarafu/fedha ya nchi.

Uarabuni fedha yao inathamani kwasababu wao wanapata fedha za kigeni nyingi kwa kuuza mafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…