Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Ujenzi wa mji wa serikali mkoani Dodoma unaendelea, na hivi sasa mtandao wa barabara za lami katika mji huu ni kama umekamilika na umebadilisha kabisa muonekano au mandhari ya huu mji.
Hata hivyo, aina ya magorofa kwa kila wizara ndio yataamua muonekano wa jumla wa huu mji..Yale majengo ya mwanzo ya kufanan kwa kila wizara, kwa hakika hayakuwa ya kuvutia, ila baada ya mtandao wa barabara za lami katika mji huu kufikia hatua ya kukamilika, taswira ya huu mji sasa imebadilka na umeanza kuvutia. Hofu yangu sasa ni aina ya magorofa kwa kila wizara kwani ndio yataamua huu mji uonekane vipi.
Sijui wamepanga kujenga magorofa ya aina gani kwa kila wizara, ila binafsi naona itakuwa bora/itapendeza kama kila wizara itakuwa na ramani yake kuliko kuwa na majengo uniform kama ilivyo sasa kwa yale majengo yaliyopo kwa kila wizara.
Eneo la mji wa serikali ni kubwa mno na nitakuwa wa mwisho kuamini kama uniformity katika ujenzi wa magorofa katika eneo hili utavutia.
Kama majengo yatakuwa ya kuvutia, basi hata yakifanana mji mzima, inaweza isiwe tatizo sana, ila ikitokea hayavuti, na mji mzima yakawa ndio hayo, basi mji huu utakuwa umeharibiwa.
Pia ikiwezekana, wizara moja iwe ni gorofa tatu, nyingine nne na nyingine tano,n.k mradi tu kuwe na tofauti na hapo ndio tutweza kuwa na mji katika eneo hili.
Najua mpaka sasa michoro kwa kila wizara iko teyari, hivyo hakuna kitachobadilika ila hii haituzui kusema.
Mji kwa sasa unapendeza, ila ujenzi wa hayo magorofa ndio utaamua kila kitu hapo baadae juu ya muonekano mzima wa huu mji.
Msije mkatujengea mji wa serikali ukawa kama yale ya magorofa ya Jeshi yaliyoko jirani pale Ihumwa.
Michoro kama hii inapendeza machoni, ila inaweza kuku-deceive na utakuja kugundua when it comes to reality baada ya ujenzi kukamilika.