Dada sikujui my dear lakin am sorry kama nitakukwaza. Hii sio hekima kabisa. Nikwambie kitu...wewe ni mzazi. Haibadiliki. Kama mlishakosana wewe na aliekuwa mwenzi wako ni nyinyi wawili..lakin kuna kiumbe cha Mungu mnatakiwa mkilee.
Kupigana block haibadilishi kuwa kuna DNA ya baba wa mtoto kwa mtoto. Ukiona mwenzio kapungukiwa unaloweza kufanya ni kumuombea na wewe kufanya mambo yako kama mama wa mtoto. Sijajua wewe ni dini gani.. lakini katika dini yangu msingi wa dini ni upendo and too bad wengi wetu hatunao.
Upendo haujivuni, hauhesabu mabaya, haukosi kuwa na adabu, hauwazi yaliyo ya kwake. Ukiwa na huu upendo hata mtu akukosee vipi, hutamuwazia mabaya. It doesn't change..he is your kid's father mamy.
Naongea ivi from experience..ya ndani..personal kabisa. Nimeishi na mtu aliekuwa amebeba resentment for years juu ya baby daddy wake, tangia abebe hiyo resentment alipatwa na ugonjwa flani. Na mpaka alipokuja kumsamehe yule mwanaume ndipo na ule ugonjwa umepona.
Fanya kazi, sali sijui swali sana, tafuta maarifa, ufahamu, hekima katika vitabu vya dini kwa namna ya co-parenting, na pia kuwa na mipaka baina yenu. But dont bear grudge...kama nitakuwa nimekukwaza please am sorry madam.