Aina za ujasiriamali zinazoweza kumtoa kijana kimaisha

Aina za ujasiriamali zinazoweza kumtoa kijana kimaisha

Unakosea boss kitu kimoja...kuna kitu kinaitwa batch...ukianza mwanzo utasubiri kwanza wakue au wazaliane baadae utaanza kuwa na batch tofauti ambayo itakuruhusu ww kuuza kila siku...hili litakuwa sawa pale tu unapoweka effort zako zote huko na sio bra bra ....kwaiyo utakuwa na watoto...wakatikati na wakiotayr kuuzwa...ww umeangalia pale unapoanza
 
Watu wanataka pesa za kila siku hata kama ni ndogo ila awe na uhakika kila siku anapata pesa ya kuhudumia maisha yake na familia.

hizo biashara ulizotaja zinawafaa wastaafu au watu ambao tayari wameshazipata...

Biashara hizo zipo ktk kundi la (biashara ongeza kipato)

Wakati unasubiri sungura azae,nguruwe azae,kuku wakue (hapo kati kati unakua unafanya nini?)

Biashara ni nzuri sana hizo ila yapasa uwe una plan na backup ya pesa ili hiyo miradi iweze kukua na kukupa matokeo chanya.
Wewe jamaa inahitajika uwe Consultant officer wa business, mkuu tafuta mtaji uwe unatoa elimu kwa wajasiriamali na vikundi mbalimbali hii itasaidia wengi na itakuongezea kipato na kujulikana.
Mtaji naozungumzia ni wa kujitangaza na kugather watu wanaohitaji ushauri.
 
1. ufugaji wa kuku. Ufugaji wa kuku wa kienyeji ama kuku wa kisasa. Faida zake zinatokana na uuzaji wa mayai, nyama ya kuku, kuku wenyewe, vifaranga, mbolea n.k

_ Ndege wengine wenye faida kama za kuku ni kanga, bata wa aina tofauti, njiwa, kware n.k

2. Ufugaji wa mbuzi. Mbuzi faida zake zinakuja kwenye nyama, maziwa, mbolea,pembe na kwato huzalisha gundi,
_pia unaweza fuga kondoo ama ngombe

3. Ufugaji wa sungura. Faida za sungura hazitofautiani na faida za mbuzi lakini sungura huzaa watoto wengi na ni rahisi kumfuga kwenye eneo dogo

_Mkojo wa sungura ni mzuri sana kwa mbolea

4. Ufugaji wa ngurue. Hii ndio biashara inayochipukia kwa sasa. Pia ngurue huzaa watoto wengi kwa mpigo, faida zake nyingine ni kama zile za mbuzi

5. Ufugaji wa nyuki. Ufugaji wa nyuki ni mrahisi tu ukiwa na eneo la kutosha faida za nyuki ni asali hii hutumika kama kiungo kwenye vyakula lakini pia hutumika kama dawa na hata kuoshea vidonda kwa watu wenye ugonjwa wa sukari, uchavushaji ni faida nyingine kubwa ya nyuki, masega ya nyuki hutumika kutengenezea mishumaa

6. Ufugaji wa samaki. Samaki wana source kubwa ya protein ambayo hutumika kwa ukuaji, mafuta ya samaki pia watu wanasema ni dawa, lakini pia kipato kutokana na samaki, kuna samaki wa mapambo pia
7 ufugaji wa mbwa. Kufuga mbwa kama biashara tutajipatia kipato lakini pia mbwa hutumika kwa ulinzi nyumbani
8.kilimo cha mazao tofauti kwaajili ya chakula na biashara hii ni njia nyingine ya kujipatia kipato
mkuu ni frash kidogo kwenye ufugaji wa samaki.
 
Hapana nakupinga mkuu CONTROLA.
Kuna binti anafuga kuku wa nyama lakini ilifika wakati akakata tamaa kwawababu ya bei ndogo sokoni(kwa walanguzi).akapata wazo la kununua freezer kubwa ya kugandisha,kuku wakikua anachinja wote anatunza kwenye freezer anatoa kuku kwenye freezer anakaanga na anauza mwenyewe kidogo kidogo,wakati huo bandani anavifaranga wapya wanakua,mpaka akawa maarufu kiasi mpaka akawa anapokea oder kubwa ya nyama za kuku kwenye sherehe n,k.
Kumbuka kunamsemo usemao safari moja huanzisha nyingine,kikubwa kuwa mbunifu mambo mengine yanajiseti yenyewe kama ukiwa mbinifu kama ulivyo wewe CONTROLA
Mkuu huyo binti sidhani kama tunamuweka ktk kundi la wenye shida hapa town.

Jiulize Bei ya hilo freezer alilonunua ni sh ngapi, usifkiri n kale ka freezer kadogo...

Jiulize hela ya kulisha hao kuku mpaka anawatoa anawachinja anawatunza ni amekua ametumia kiasi gani?

Jiulize gharama anazokua anatumia kuwasha freezer ON 24hrs ili kuku wasiharibike anakua ametumia UMEME wa UNIT ngapi?

Tunaongelea freezer ulaji wake waumeme tunaufananisha na gari kama Premio/Alphard na wenzao kwenye mafuta.

freezer linabugia UNIT halionji onji kama Fridge, sasa mwenzako analiwasha 24hrs halizimwi.

Hizo ni cost za juu juu tunazoziona sisi wapga story hapa,kuna zile hidden cost ambazo hatuzijui Mkuuu mtu anaefuga kuku usimchukulie kisport sport sio mwenzako kbsa.

Ni mjasiriamali ndio hatukatai Hata MO dewj nae ni mjasiriamali ila huwezi nifananisha mimi controla na Mo au bakhressa never...

Huyo dada ana ligi zake ila sio ligi za wajasiriamali wauza mahindi/mishkaki/wamama ntilie wanaouza wali wao kwenye ndooo,nk nk

Huyo ana backup ya pesa somewhere sio eti ndio anataftia hapo Maisha atoke,no way.
 
Watu wanataka pesa za kila siku hata kama ni ndogo ila awe na uhakika kila siku anapata pesa ya kuhudumia maisha yake na familia.

hizo biashara ulizotaja zinawafaa wastaafu au watu ambao tayari wameshazipata...

Biashara hizo zipo ktk kundi la (biashara ongeza kipato)

Wakati unasubiri sungura azae,nguruwe azae,kuku wakue (hapo kati kati unakua unafanya nini?)

Biashara ni nzuri sana hizo ila yapasa uwe una plan na backup ya pesa ili hiyo miradi iweze kukua na kukupa matokeo chanya.
Summary ya maelezo yako ni kwamba biashara hizo zinahitaji pesa ya kutumia wakati zikisubiriwa. Huo ndio mtaji, japo benki hazina nafasi ya kutoa mitaji kwa biashara zinazo anza, kwao ni risky. Wanatoa mitaji kuendeleza biashara.
 
Samahani mkuu nje ya mada kidogo naomba kuuliza, hivi mtu alie Fundi mfano welding, Carpenter, mechanical, Mason, nk. Wanaweza kufanya ufundi wao Kama biashara?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ngazi ya chini huwa ni mafundi na si wafanya biashara. Wanasubiri oda za wateja. Wakipata mtaji mkubwa huwa wafanya biashara, wanatengeneza bidhaa na kusubiri wateja. Workshop zao zinaweza kuwa eneo moja na show room, au vinaweza kuwa maeneo tofauti.
 
Mkuu huyo binti sidhani kama tunamuweka ktk kundi la wenye shida hapa town.

Jiulize Bei ya hilo freezer alilonunua ni sh ngapi, usifkiri n kale ka freezer kadogo...

Jiulize hela ya kulisha hao kuku mpaka anawatoa anawachinja anawatunza ni amekua ametumia kiasi gani?

Jiulize gharama anazokua anatumia kuwasha freezer ON 24hrs ili kuku wasiharibike anakua ametumia UMEME wa UNIT ngapi?

Tunaongelea freezer ulaji wake waumeme tunaufananisha na gari kama Premio/Alphard na wenzao kwenye mafuta.

freezer linabugia UNIT halionji onji kama Fridge, sasa mwenzako analiwasha 24hrs halizimwi.

Hizo ni cost za juu juu tunazoziona sisi wapga story hapa,kuna zile hidden cost ambazo hatuzijui Mkuuu mtu anaefuga kuku usimchukulie kisport sport sio mwenzako kbsa.

Ni mjasiriamali ndio hatukatai Hata MO dewj nae ni mjasiriamali ila huwezi nifananisha mimi controla na Mo au bakhressa never...

Huyo dada ana ligi zake ila sio ligi za wajasiriamali wauza mahindi/mishkaki/wamama ntilie wanaouza wali wao kwenye ndooo,nk nk

Huyo ana backup ya pesa somewhere sio eti ndio anataftia hapo Maisha atoke,no way.
Nimekupata vema mkuu CONTROLA
 
Ukiona biashara hafanyi mo,bakharesa, au wahindi,au waarabu au wachaga, au wakinga.......achana nazo hazina faida.....wapi umeona wachaga wanafuga sungura au kuku,wapi umeona wahindi wanauza mkojo WA sungura.....mwenye akili amenielewaaaa
_[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom