Alvin_255
JF-Expert Member
- Oct 26, 2015
- 246
- 503
Kanisa Lina Aina ya watu ambao hawako katika MISHENI Sawa. Kuna Baadhi ya wahusika uwepo wao Kanisani ni kukamilisha ajenda zao ZINGINE...
Katika Historia ya Makanisa Maandiko Matakatifu (Ufunuo 3:14-15) yanaeleza kuwa tupo Kanisa la mwisho ambalo ni Kanisa la Laodakia na tabia za Kanisa la Laodakia zinaelezwa kuwa ni....
"Nayajua matendo yako ya kuwa hu baridi wala Moto; Heri kama ungekuwa baridi au Moto!.."
MAKALA hiii itakupatia Baadhi ya Aina ya watu na tabia zao Kanisani, Lakini pia itakuwezesha kujitafakari mwenyewe....
1. Soldier.
Hawa ni Askari wa MUNGU. Wamejitoa kikamilifu katika kumtumikia MUNGU. Wamebarikiwa Sana na MUNGU Kwa sababu ya utiifu na uaminifu wao. Wana msimamo mkuu katika kuifanya kazi ya MUNGU. Wanaahika maono na kuyafanya yawe. Wanatumia muda wao mwingi, pesa, rasilimali, na talanta kuendeleza misheni na maono ya kanisa. Hufanya Maombi ya kina kuhusu maendeleo ya Kanisa.
2. A prostitute.
Amebarikiwa na Talanta ndani Yake Lakini mwelekeo wa Talanta yake humuongoza katika
kutafuna tunda lililokatazwa.
A prostitute wa kiume anaonekana Mwinjlisti, Mwalimu wa Neno la MUNGU, Mwalimu wa kwaya, Mpiga kinanda gitaa au Ngoma, Mwonekano wa nje ni serious mtu wa kiroho Lakini dhamira yake ni kumtafuna Salome muimbishaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu....
Mara tuu anapomaliza kumtafuna Salome, anatoweka kwenye hewa nyembamba na kuanza misheni kama hiyo mahali pengine. Hii ndio sababu utakuta Kanisa lina wanawake wengi wasio na hatia wanaolea watoto peke yao, kwasababu tuu waliingia katika mtego wa Church boy...
3. Forced Lover.
Anaenda kanisani kukidhi matakwa ya mchumba wake, Wengi ni wanaume. Matamanio ya kila mwanaume ni kuoa Mwanamke mwenye Hofu ya MUNGU ili aipate heshima anayoitafuta. Sababu hii humfanya kufake pindi tuu anapokutana na Yule anayehisi kuwa ni sahihi kwake.
Atajifanya kuwa ni KIJANA wa kiroho mzuri zaidi, Kwa kuficha tabia zale zote zisizofaa ili ampate Binti mlokole. Lakini Baada ya misheni yake kukamilika(Kufungua Ndoa) Hurudi katika tabia zale halisi....
4. Fame seekers.
Katika kundi hili, kuna wanasiasa utawaona Kanisani ili kupata Mafanikio Yao ya kisiasa. Na tunaelekea uchaguzi utawaona walivyo wakiroho na walivyo watoaji...
Tunapoelekea uchanguzi watasoma Biblia Kwa bidii zote ili waonekane Wana Hofu ya MUNGU. Watajitahidi kuenenda kama wanafunzi wa YESU. Lakini, unafiki wao niwa muda mfupi Kabla ya kurudi kwenye maisha Yao halisi Baada ya uchaguzi kuisha...
5. Lover hunters.
Hawa wanatofauti kidogo na Church boy Hawa wanatafuta upendo wa dhati na wanaamini msichana wa kanisa au mvulana wa kanisa anaweza kuwa chaguo Bora katika maisha ya Ndoa...
Anakuwa mshiriki wa kanisa mara tu anapomwona msichana mrembo Kanisani tena mwenye tabia njema...
Hujitolea katika Kazi ngumu za Kanisani ili kukuvuta moyo wa msichana huyo na anapofaulu hutulia katika maisha ya Ndoa.
6. Music lovers.
Hawa huwenda Kanisani kwasababu tuu wanapenda Aina ya nyimbo zinazoimbwa..
Utawasikia wakisema; " Napenda Sana nyimbo za Kanisa katoliki au za kisabato, wanaimba wametulia". Au Utawaona wakijiunga katika vikundi vya kusifu na kuabudu au kujifunza Kupiga kinanda, gitaa, Ngoma wakishapata Ujuzi wanageukia katika mziki wa kidunia...
7. Confused believers.
Wanaenda kanisani kimazoea, na kushiriki katika shughuli zote za kanisa lakini hawana uhakika wa kwa nini wanaenda kanisani....
Ukiwauliza kwanini unaenda Kanisani, watakujibu kwasababu; nimekulia katika familia ambayo wanaenda Kanisani...
Mara nyingi zaidi kundi hili ni vigumu zaidi kuwaona wamepiga hatua yoyote ya kiroho. Utawaona wamebeba Biblia Lakini ukiwaambia wakwambie Hata mafungu mawili waliyokariri katika Biblia hawana majibu.
8. Personal advertiser.
Ni Aina ya waumini wanaojitokeza kuonyesha Mafanikio makubwa na madogo waliyoyapata Kanisani.
Wanapokuwa kanisani mara nyingi zaidi matamanio Yao ni kutaka watambuliwe na kila muumini, mchungaji au Padri kuwa ni familia
yenye Mafanikio makubwa.
Hupenda kila muumini awazingatie na kuwaona wao ni special Sana. Kwa sababu ya Mafanikio Yao hutengeneza urafiki wa Karibu zaidi na watumishi wa MUNGU.
9. Seekers wealth.
Wanajua MUNGU ndiye mtoaji na utume wao kanisani ni kumuomba MUNGU ili awabariki kwa mambo ya duniani. Utajiri ndio lengo lao pekee. Wanawinda utajiri kwa njia zozote kupitia mahubiri ya pokea Muujiza..
Wanafunga na kuomba ili kupokea muujiza. Wengine huanzisha makanisa na kujiita watumishi wa MUNGU ili kukamua waamini walio katika mazingira magumu. Mahubiri Yao kila KUKICHA ni pokea Mafanikio, pokea utajiri, pokea Mali, Pokea Muujiza wako nasi kuwaongoza watu katika kumjua MUNGU....
Muumini Seekers wealth anaamini utajiri katika Pokea Muujiza nasio Mchakato wa kazi, bidii na consistency...
10. Prisoner mentality.
Aina hii ya waumini huwaona viongozi wao wa kidini kuwa ndio kila kitu kwao. Huwaambii chochote kuhusu kiongozi wao dini.
Kwao kiongozi wao wa dini ndio MUNGU wao. Chochote atakachowaambia watafanya Hata kama hakina ukweli katika Maandiko Matakatifu. Kwasababu ya utumwa wa Fikra walionao huamini kila kisemwacho na viongozi wao wa dini bila kukipima katika Maandiko Matakatifu....
"Afya yako ya akili, Kipaumbele chetu"