AIR INDIA inauzwa, hasara zimeielemea

AIR INDIA inauzwa, hasara zimeielemea

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Posts
2,507
Reaction score
2,412
air-india-plane_650x400_61474351147.jpg

Wizara ya Anga ya India imetangaza kuweka sokoni umiliki wao wa 76% kwenye Air India baada ya serikali kushindwa kuendelea kuvumilia kula hasara.

Air India wamesema atakaependa kuwachumbia ajue binti anakuja na mtoto wa kulea, utabeba deni la dola bilioni 5.

BBC World News
————————-

Tanzania tuwe makini na shamra shamra za kununua ndege kama zile tulizoziona jana pale JKNA. Matatizo ya mashirika ya ndege yote duniani private and public sio upungufu wa ndege peke yake. Kwa sasa Air Tanzania tayari imeanza kupoteza hela kwa mujibu wa Kamati ya Bunge. Serikali yetu inapopewa tahadhali isikimbilie kushutumu kwamba hatuna uzalendo, bali tunajua, tunatazama na kujifunza yanayotokea duniani kwingine. Nchi hii siku hizi ni ya wasomi wenye exposure pia, sio uninformed peasants peke yao ambao utawanywesha kama dodoki kila unachotaka wewe. Acheni kusomesha vijana basi na mpige marufuku ma vyuo yote! Khaaa!

=====

Air India sale: Who'll buy the debt-laden carrier?
_100618168_airindiaplanein2018.jpg

India's cabinet approved plans to privatise Air India in June last year
India's government has decided to sell a controlling stake in the loss-making national carrier, Air India.

It is putting 76% of the business up for sale in what would be India's most high profile asset sale in decades.

Air India has relied on taxpayer-funded bailouts to stay operational - and the new buyer would take on about $5bn (£3.6bn) of debt.

If privatisation goes ahead, it will be a boost to Prime Minister Narendra Modi's claims to be a reformist leader.

But it is not a done deal. Such plans have been abandoned before, and unions have threatened wide-ranging protests if ministers push ahead this time.

Once the country's only airline, Air India has lost market share to new entrants and suffered from a reputation for poor service and cancelled flights.

It has not turned a profit since 2007 - but with India seeing passenger growth of around 20% per year and analysts saying the Indian market is vastly underserved - it could still be a tempting prospect for would-be buyers.

What's up for sale?
According to documents released by the government, Air India will be put up for sale as four different entities.

  • 76% of the main airline business - made up of Air India, its low-cost arm Air India Express and subsidiary AISATS
  • Alliance Air - the carrier's regional arm
  • Air India Air Transport Services
  • Air India Engineering Services Ltd
Bidders are allowed to make separate offers for the four divisions - or for a combination of them.

Who'll buy it?
International routes are the most lucrative part of the Air India business, with slots at major international airports including London Heathrow and New York JFK.

IndiGo, India's biggest airline, has said that it would like to carve out Air India's international passenger airline operations - to add to the seven international destinations it already flies to.

But that is not an option currently on the table - and Indigo said it would also "evaluate" the option of taking on all of the airline business and see if it was "economically feasible for us to go down that path".

_98659722_gettyimages-863049238.jpg
Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionIndiGo would like to buy Air India's international operations but hasn't ruled out a wider bid.
"At the end of the day, this exercise is not about becoming bigger for the sake of being bigger - it is all about profitable growth," co-founder Rahul Bhatia said.

But he was clear IndiGo was not looking at buying all of Air India's businesses and subsidiaries.

"In our view, that would be a herculean task which would at best be a very challenging proposition and at worst an impossible task, unless an organisation is willing to fund large losses for a very long time," Mr Bhatia said.

Another potential buyer is Vistara - the joint venture airline run between India's Tata Group and Singapore Airlines.

Earlier this month, Singapore Airlines general manager David Lim told the BBC that it was "open" to an Air India bid.

"We haven't closed the doors and when that happens we will look at it", he said

_99458992_043374448-1.jpg

Jet Airways is another potential bidder
Indian rules state that majority ownership of any national airline needs to be with an Indian national. So while international carriers can make a bid - the biggest stake they can hold is 49%.

Jet Airways, another Indian carrier, is also likely to take a serious look at an offer - perhaps in partnership with an international carrier. Media reports suggest Air France and Delta may be interested.

The government has waived some of the criteria for existing Indian airline operators to make bids - relating to net worth and recent profitability - so long as they bid as part of a consortium.

Qatar Airways was another international airline linked with buying a stake in Air India, but it has since denied any interest.

Any caveats?
The eventual buyer of Air India may eventually have to list the airline on the stock exchange - which would be a clear incentive to make it profitable within a fixed time frame.

It is likely that at this point, the government would then sell its remaining 24% in the business.

The buyer will be taking on about $5bn of debt. However, this is only about half of what the airline owes. So in effect the buyer is getting a smaller proportion of the debt than it might expect for a 76% stake - which might make things more appealing.

What's the time line?
Would-be bidders have until 14 May to make initial proposals.

Shortlisted bidders will be informed by 28 May.
 
Mh! Sijui kama watapata mnunuzi hawa. Yaani mnunuzi unanunua na deni la $5 billion! WARIE TU! Na biashara yenyewe ya Ndege ilivyokuwa ngumu duniani sasa hivi watasubiri sana kupata Tajri. Nimepapenda hapo kwenye rangi nyekundu.

Ndege zinailetea nchi heshima!!! Inaelekea India wanataka kuitosa heshima yao!
😱😱😱

air-india-plane_650x400_61474351147.jpg

Mbeba Bendera wa India, Air India, imetangaza kuweka sokoni umiliki wake wa 76% baada ya serikali kushindwa kuendelea kuvumilia kula hasara.

Air India wamesema atakaependa kuwachumbia ajue binti anakuja na mtoto wa kulea, utabeba deni la dola bilioni 5.

BBC World News
————————-

Tanzania tuwe makini na shamra shamra za kununua ndege kama zile tulizoziona jana pale JKNA. Matatizo ya mashirika ya ndege yote duniani private and public sio upungufu wa ndege peke yake. Kwa sasa Air Tanzania tayari imeanza kupoteza hela kwa mujibu wa Kamati ya Bunge. Serikali yetu inapopewa tahadhari isikimbilie kushutumu kwamba hatuna uzalendo, bali tunajua, tunatazama na kujifunza yanayotokea duniani kwingine. Nchi hii siku hizi ni ya wasomi wenye exposure pia, sio uninformed peasants peke yao ambao utawanywesha kama dodoki kila unachotaka wewe. Acheni kusomesha vijana basi na mpige marufuku ma vyuo yote! Khaaa!
 
Nilionya hapa kwamba habari za wanasiasa kuingilia mashirika ya ndege zitafanya mashirika hayo yaendeshwe kisiasa na kwa hasara na hatimaye kufa au kuendelea kwa style ya "bottomless money pit".

Kuna CEO wa Ethiopian Airlines alisema moja ya sababu Ethiopian Airlines ina mafanikio makubwa ni kwamba wanasiasa hawaingilii maamuzi kwa sababu za kisiasa.

Ona hapa Why is Ethiopian Airlines so successful?, 11/08/2017 GMT, Africa Business Report - BBC World News

"The Airline is fully owned by the government of Ethiopia, but fully managed by professional aviation experts..." - Tewolde Gebremariam, Ethiopian Airlines CEO.

Tanzania wanasiasa wataweza kuwaachia professionals waendeshe shirika la usafiri wa ndege?
 
air-india-plane_650x400_61474351147.jpg

Mbeba Bendera wa India, Air India, imetangaza kuweka sokoni umiliki wake wa 76% baada ya serikali kushindwa kuendelea kuvumilia kula hasara.

Air India wamesema atakaependa kuwachumbia ajue binti anakuja na mtoto wa kulea, utabeba deni la dola bilioni 5.

BBC World News
————————-

Tanzania tuwe makini na shamra shamra za kununua ndege kama zile tulizoziona jana pale JKNA. Matatizo ya mashirika ya ndege yote duniani private and public sio upungufu wa ndege peke yake. Kwa sasa Air Tanzania tayari imeanza kupoteza hela kwa mujibu wa Kamati ya Bunge. Serikali yetu inapopewa tahadhali isikimbilie kushutumu kwamba hatuna uzalendo, bali tunajua, tunatazama na kujifunza yanayotokea duniani kwingine. Nchi hii siku hizi ni ya wasomi wenye exposure pia, sio uninformed peasants peke yao ambao utawanywesha kama dodoki kila unachotaka wewe. Acheni kusomesha vijana basi na mpige marufuku ma vyuo yote! Khaaa!

Ujumbe huu umfikie sozinje anayenunua ndege bila hata idhini ya Bunge kwa kisingizio cha uzalendo na kuleta heshima bila ya kufanya upembuzi yakinifu. Haya sasa, kwa kipindi Kifupi tu , bombadia 2 tu zimeshazalisha hasara zaidi ya bilioni 223. Tukifikia umri wa Air India itakuwaje?
 
Nakumbuka wakati kina Zitto Kabwe wanadai tuwe na “flag carrier” nilikuwa nawaambia Flag Carrier maana yake nini? Mbona serikali za Canada, UK, USA, France, Germany, Switzeland, Italia, Australia hawana ndege?
 
Kwa nini mnatoa shutuma badala ya kutoa namna shirika linaweza kujitoa kwenye tatïzo la kuingia hasara!!!? Mnaongea as if ndege ni ya adui yenu!!!! Anyway KUSHINDWA KWA INDIA SI KIGEZO CHA SISI PIA KUSHINDWA
Tatizo lipo kwa wanasiasa kuendesha mashirika kisiasa
 
Ujumbe huu umfikie sozinje anayenunua ndege bila hata idhini ya Bunge kwa kisingizio cha uzalendo na kuleta heshima bila ya kufanya upembuzi yakinifu. Haya sasa, kwa kipindi Kifupi tu , bombadia 2 tu zimeshazalisha hasara zaidi ya bilioni 223. Tukifikia umri wa Air India itakuwaje?
Changamoto kwenye mabadiliko ya kiuchumi ni swala lisilokwepeka, Si lazima kila kitu kuangalizia kwa wenzetu hivyo basi tunaweza kufanikiwa kwa mfumo wetu wenyewe .WATANZANIA MSITAKE MABADILIKO YASOKUA NA MSOTO, YATUPASA TUPATE SHIDA ILI KIZAZI KIJACHO KINUFAIKE SASA SISI TUNATAKA TULIME SHAMBA WAKATI HUOHUO TUVUNE

NB:KUKOSEA SI TATIZO KWANI NI NJIA MOJA NZURI SANA YA KUJIFUNZA
 
Kwa nini mnatoa shutuma badala ya kutoa namna shirika linaweza kujitoa kwenye tatïzo la kuingia hasara!!!? Mnaongea as if ndege ni ya adui yenu!!!! Anyway KUSHINDWA KWA INDIA SI KIGEZO CHA SISI PIA KUSHINDWA
Kweli kushindwa kwa India si kigezo kwa sisi kushindwa.
Ila tayari tuna hasara ya bi.223 tzs. Lakini kupata hasara si kigezo cha kushinda.
 
Tatizo lipo kwa wanasiasa kuendesha mashirika kisiasa

Tanzania wanasiasa wataweza kuwaachia professionals waendeshe shirika la usafiri wa ndege?

Hata kama professionals wangeachiwa ku run kampuni bado sidhani kama ATCL wanaweza kujiendesha. Ingekuwa hivyo serikali zisingejitoa kwenye makampuni kama SWISS AIR, ALITALIA, AIR CANADA, KLM, BRITISH AIRWAYS, LUFTHANSA, AIR FRANCE, QANTAS, na hii ya leo AIR INDIA.

There is a reason why serikali hazimiliki biashara za ndege au biashara period.
 
And what is the reason?
 
Ujumbe huu umfikie sozinje anayenunua ndege bila hata idhini ya Bunge kwa kisingizio cha uzalendo na kuleta heshima bila ya kufanya upembuzi yakinifu. Haya sasa, kwa kipindi Kifupi tu , bombadia 2 tu zimeshazalisha hasara zaidi ya bilioni 223. Tukifikia umri wa Air India itakuwaje?
Bombardier imezalisha hasara ya bilioni 223 ? Yaani hizo pangaboy mbili au tuna Ma Airbus kama 8 hivi zinapiga kazi kimya kimya ?

Hizi habari za hasara hii ziko wapi nikajisomee ?
 
Daah, hizi ndege ni laana au baraka kwetu Watanzania? Naona wapo wanaozishangilia wengine wanazikejeli.
Tunapitia mapito ya pekee sana nafikiri kuliko ilivyowahi kutokea huko tawala za nyuma
 
Biashara ya usafiri wa anga inahitaji abiria wengi na viwanja vingi vya ndege (destinations). Hapa kwetu TZ abiria ni wachache kutokana na wengi kutomudu nauli za ndege. Njia ambazo zinalipa ziko chache sana na ndio zinagombaniwa na kampuni zote. Dar- Mwanza-Dar, Dar -Arusha/Moshi-Dar labda na mbeya na Zanzibar. Njia nyingine huwezi kupeleka ndege kila siku kwa sababu abiria ni wachache au viwanja ni vibovu. Kwa hiyo unahitaji umakini mkubwa kuendesha hii biashara hapa TZ. kuna kipindi precision air walikuwa na ndege 10 lakini walipata hasara na kuzirudisha. Ndege ikikaa chini sana ni hasara kwa sababu unailipia na inaweza kuharibika.
 
Daah, hizi ndege ni laana au baraka kwetu Watanzania? Naona wapo wanaozishangilia wengine wanazikejeli.
Tunapitia mapito ya pekee sana nafikiri kuliko ilivyowahi kutokea huko tawala za nyuma
Waruhusu uchumi uzunguke watu wajiweze kiuchumi wapandaji wawe wengi,watapata faida au wazipeleke ruti za nje,ndani wasafiri wamepungua.Kama wenye mabasi ya mikoani wanayapaki MTU alikuwa anatoa yadi gari NNE Kwa siku Kwa ruti moja leo anatoa gari mbili, hesabu ya daladala Kwa tajiri zimepungua sababu watu usafiri panapokuwa na ulazima.Wao ni nani wapate faida Kwa mazingira hayo hayo.
 
And what is the reason?

Accountability, above all else.

Mimi ni mwajiriwa wa kudumu wa umma, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege, nimeteuliwa na Rais, nina pensheni inaningoja na hakuna popote palipoandikwa kwamba posho, mafao, mshahara na mustakabali wa ajira yangu utategemea business performanceya kampuni, utanieleza nini maisha haya?

Na haya mambo hayajaanza leo, tatizo tunasahau historia yetu. Waajiriwa wa kudumu wa umma wa kina Gibbons Mwaikambo, Mwapachu, Kazaura, Mmari, Janguo waliya run down mashirika ya umma with total impunity mpaka wanastaafu au wanafia ofisini. ATCL is far from a first experiment with state ownership of business conglomerates.
 
Inamaana wahindi sasa n mwiko kutembea kifua mbele, kama watauza heshima ya nchi yao.
 
Back
Top Bottom