KERO Air Tanzania imeondoka na abiria wengine, wametuzuia watano, tunaambiwa kuna 'Technical Problem', hii ni sawa?

KERO Air Tanzania imeondoka na abiria wengine, wametuzuia watano, tunaambiwa kuna 'Technical Problem', hii ni sawa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kutakuwa na namna, ila kusema ilizidi uzito sidhani kama ina mashiko.
 
Biashara ya ndege kufanya overbooking ni tabia yao.... Huwa wanategemea kuna watu watachelewa tu 😂😂😂 kimbembe kinakuja watu wote wanapowahi

Pia overbooking inatakiwa kufanywa sehemu yenye ndege nyingi, ili wote wakiwahi wapelekwe ndege ya baadae
 
Hahaha! Unanikumbusha mambo ya zamani ya kwenye treni na mabasi, makondakta wanapambanisha tiketi, yaani siti moja inakatiwa hata kwa abiria watatu halafu mnakuja kugombana ndani ya safari.

Sasa itakuwa kwenye ndege haiwezekani abiria kusimama, ingekuwa inawezekana wangekuwa wanawasondeka kwa sababu sisi WaTZ tumeamua kuishi mfumo wetu wa maisha!
Inakera balaa unasikia simama had singida akishuka huyu utakaa 😀😀
 
Kwa kawaida local flights huwa wana-OVERBOOK abiria. Wanachukua booking za abiria kuliko uwezo wa ndege wakitegemea kuna abiria wataahirisha au kuchelewa check in. Hapa airline wananufaika.
Hii ipo sana Nigeria, wao kusimamisha abiria au kupanda ndege na mbuzi siyo jambo geni
 
Kwa kawaida local flights huwa wana-OVERBOOK abiria. Wanachukua booking za abiria kuliko uwezo wa ndege wakitegemea kuna abiria wataahirisha au kuchelewa check in. Hapa airline wananufaika. Kama itatokea abiria wote kufika airport ndio inatokea kama hivi. Kwahio mleta mada hizi local flights jitahidi uwe unawahi ku check in.
Watamlipia hiyo ndege nyingine ya kuunganisha aliyoikosa kama ni shirika tofauti?
 
Itakuwa Kuna kigogo kabeba nafasi zenu wanakawa wanatafuta wanyonge wao kuwakandamiza. Poleni
 
Hii ipo sana Nigeria, wao kusimamisha abiria au kupanda ndege na mbuzi siyo jambo geni
Duh Nigeria wako rough ila sio kupanda ndege na mbuzi. Labda Congo DR ndio wanaendesha ndege kama daladala.
 
Back
Top Bottom