KERO Air Tanzania imeondoka na abiria wengine, wametuzuia watano, tunaambiwa kuna 'Technical Problem', hii ni sawa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kutakuwa na namna, ila kusema ilizidi uzito sidhani kama ina mashiko.
 
Biashara ya ndege kufanya overbooking ni tabia yao.... Huwa wanategemea kuna watu watachelewa tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kimbembe kinakuja watu wote wanapowahi

Pia overbooking inatakiwa kufanywa sehemu yenye ndege nyingi, ili wote wakiwahi wapelekwe ndege ya baadae
 
Inakera balaa unasikia simama had singida akishuka huyu utakaa πŸ˜€πŸ˜€
 
Wameuza siti yako kwa matajiri wa katoro
 
Kwa kawaida local flights huwa wana-OVERBOOK abiria. Wanachukua booking za abiria kuliko uwezo wa ndege wakitegemea kuna abiria wataahirisha au kuchelewa check in. Hapa airline wananufaika.
Hii ipo sana Nigeria, wao kusimamisha abiria au kupanda ndege na mbuzi siyo jambo geni
 
Watamlipia hiyo ndege nyingine ya kuunganisha aliyoikosa kama ni shirika tofauti?
 
Itakuwa Kuna kigogo kabeba nafasi zenu wanakawa wanatafuta wanyonge wao kuwakandamiza. Poleni
 
Hii ipo sana Nigeria, wao kusimamisha abiria au kupanda ndege na mbuzi siyo jambo geni
Duh Nigeria wako rough ila sio kupanda ndege na mbuzi. Labda Congo DR ndio wanaendesha ndege kama daladala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…