Air Tanzania ingeshusha viwango vya nauli, tungesafirisha Watanzania wengi ndani na nje ya nchi

Mimi nililipa, 42500, 66000, 94000 na 154000 one way
Hizi ni bei rafiki sana.

Wateja wetu wengi hutuomba tuwafikishie malalamiko yao katika idara husika na kututaka tukahoji; hayo mashirika mengine yaliwezaje hadi ATC lishindwe kuweka bei hizi?

Kupitia uzi huu watayaona pia. Tunatazamia kheri.
 
Kwa sasa hata ukiliombea shirika la ATCL life ni ngumu kwani idadi ya abiria kwa kila route sio ndogo. Mapendekezo yangu;
1. Kama mtanzania naungana na wote tunaotaka nauli zipungue. Inawezekana na itasaidia shirika letu kuwa na abiria wengi zaidi.
2. Route za southern corridor zirejeshwe, kama vile mtwara, songea na iringa. Maana viwanja vimeshakarabatiwa.
3. Tukimaster route zote za ndani twende route za nje kama london, guanhzou nk.
 
Umeiweka vizuri sana mdau
 
Ghar
Gharama za undeshaji lazima uzingatiwe, tuko kwenye uchumi wa kati wananchi wengi wana uwezo wa kupanda Ndege.
 
Hivi ukisafiri na ndege ukapanda izo place mfano business, economy ndege ikianguka ci mnakufa wote?
Tofauti ya madaraja (classes) katika Ndege ni ubora wa huduma anazopatiwa mteja kulingana na hadhi ya daraja husika.

Kuna daraja la uchumi (economy class), daraja la biashara (business class) na daraja la kwanza (first class).

Ajali na matokeo yake ni suala lingine.

Asante.
 
Ungeweka figures ingependeza zaidi. Compare & contrast!
Ukipitia uzi vizuri, utaona bei mbalimbali zimetajwa sambamba na shuhuda.

Habari njema ni kwamba maoni na taarifa zinazoandikwa kwenye uzi huu tayari zimefika mezani kwa ofisi kuu ya ATCL.

Yote yanayoandikwa hapa yanafuatiliwa ili kufanyiwa kazi haraka mwaka huu.

Asante.
 
Yaani bei ni shida jamani tena sasa hivi naona zimeongezeka zaidi, maana juzi tu hapa nimefanya booking sema sikulipia , baada ya siku kadhaa nakuja kufanya tena booking ya siku nyingine naona bei zimeongezeka, hata ukitafuta za siku za mbeleni huko.
 
Pole sana kajojo. Tuliwasiliana na menejiment ya #AirTanzania na viongozi wa idara wakasema watakuwa wanapitia uzi huu mara kwa mara. Bila shaka wataona malalamiko haya na kuyafanyia kazi.
 
siku hzi hakuna za kukata mapemaaaaaaa kabla ya chrismass??maisha haya tunateseka na mengi jamani
 
Pole sana kajojo. Tuliwasiliana na menejiment ya #AirTanzania na viongozi wa idara wakasema watakuwa wanapitia uzi huu mara kwa mara. Bila shaka wataona malalamiko haya na kuyafanyia kazi.
ishu watende haki mambo ya kupitia uzi kila siku sio suluhisho ishu ni bei imekuwa shida !!!!!swala la kusema ndege ni zetu mbna gharama ni kubwa sana pia
 
yote ya yote ataalamu wa mambo ya auditing wanakwambia bado kampuni nyingi za ndege zinajiendesha kiahasara sana..wengi wao wanahemea juuujuu
 
Dar-Dodoma nilipe sijui 325,000 wallah nitakufa. Shabiby na Kibinyiko zile za Alfajili ni Tshs 20,000/= halafu unapita Pwani Kibaha, Morogoro kisha Dodoma. Upo angani unapita wapi. Sikataki kupanda mwewe ila kwa route za humu ndani hapa kbs biashara ya kupunguziana K-Vant na mbuzi choma. Pandeni tu. Wengine tutakufa na IT na Mafusso kwa route za ndani. Ama magari ya Magazeti yale ya Posta.
 
Ajabu ni rahisi kupanda ndege congo kuliko Tanzania, Alaumiwe aliewatoa fastjet angani tulijua ATCL ni shirika letu la kizalendo litajopanga kibiashara kwa huduma nzuri na bei rafiki lakini kubaki peke yao imekua mzigo kwao, wajitafakari bila hivo naona Baada ya Rais Magufuli na shirika litakufa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…