Air Tanzania signs deal with Bombardier for 4th Q400 NextGen

Ikifika kwenye 'partnerships' za kibiashara zinazoeleweka KQ sio saizi ya ATCL. Sio hapa Afrika wala kimataifa. Juhudi za ATCL ni za kupongezwa ila ni vitu vya kawaida sana, sio vitu vya kuwafanya mjipige vifua. Kama mnavofanya kwa kuanzisha nyuzi kama hizi kwenye jukwaa la habari na siasa za Kenya. Natumai mods watafanya kweli.
 
Endeleeni komalia kwenye umbea na porojo. Mimi nawapa tawkimu na uhalisia wa mambo kama yalivyo. ATCL haijafikia hata 1/32 ya 'destination' ambazo KQ ilikuwa inatua kote duniani miaka minane iliyopita.
Kama huna porojo ipo wapi order ya ndege 10 za KQ? Ama unasherehekea mawazo ya KQ Wala sio uhalisia? Basi wacha wa Tz pia wa sherehekee mawazo ya Jiwe😁😁😁
 
Praise timu tumechoka jamani.....kwa hiyo uchumi unakua sio .......mnatangaza ajira ya walimu 4,500 wkt kuna uhitaji wa walimu 234,000 nchi nzima nyie mnaakili kweli au mmerogwa. Waalimu zaidi ya 2mil wapo mitaani hawana ajira. Je baado mna uhalali wa kuuliza kwa nn Tz no masikini kwa uwezo wenu mdogo wa kufikiri na kushanhilia vitu vya hovyo namna hii
 
Hii itasaidia sana kutangaza nchi na kuchagiza utalii na uchumi kwa ujumla, hongereni ATC.
 
You are thinking up side down. Unasahau serikali inategemea kodi kwa maendeleo. Kwa ATC kuanzia zilivyoletwa ndege mpya tayari imeshatengeneza kiasi cha bilioni 5 kwa mwezi. Jee huoni hata mchango wake kwenye kodi, kuongeza ajira kwa travel agents, shirika lenyewe kuweza kuajiri wafanyakazi wake wenyewe, kulipa madeni yote ya nyuma kwa kiasi cha asilimia 85 unataka uelezwe nini zaidi???
 
Huu uzi unahusu ATCL, KQ anzishia uzi wao
 
Huu uzi unahusu ATCL, KQ anzishia uzi wao
Acha kukurupuka, uzi huu ulikuwa kule kwenye jukwaa la habari na siasa za Kenya. Alafu uzi ni wako au hata na wewe pia umedandia? Ila haina presha, hutaniona hapa tena, napita tu.
 
Acha kukurupuka, uzi huu ulikuwa kule kwenye jukwaa la habari na siasa za Kenya. Alafu uzi ni wako au hata na wewe pia umedandia? Ila haina presha, hutaniona hapa tena, napita tu.
Anyway, KQ haijaagiza hata ndege moja so you know, acha propaganda, chairman michael wa KQ ameshakanusha huo uzushi.

 
Hiyo press statement ni kituko, yaani unakodisha ndege 20 toka wa mashirika mengine, halafu tena unawakodishia wengine ndege 3, sasa kwanini usikodishe to 17 badala ya 20 kama hizo 3 huzihitaji? Hahaha

Na hadi sasa ndege ambazo imashazilipia na inazimiliki fully ni 3 tu, zingine zote zinaweza kuchukuliwa na wenyewe endapo zitashindwa kulipiwa. Source hiyo hapo chini
https://www.businessdailyafrica.com...r-17-planes/4003102-5009176-ggrdi8/index.html
 
Watumishi wa umma ni mizigo kwa taifa, wafanye kazi na sio kusubiri kubebwa kwa mbeleko.
 
A for effort, F for results.

Reckless effort.

Serikali inachoma hela kuibeba ATC.
Uchawi faida yake nini? Shirika lilipokuwa na lilipo sasa ni vitu viwili tofauti, faida itakuja baadae, kwa sasa wacha tuendelee kubeba watalii, watafidia hasara unayodai tunapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…