Air Tanzania yapandisha nauli zake

Air Tanzania yapandisha nauli zake

Mkuu

Mkuu nimechek nao ATC hiyo promo class wameipa validity ya mwezi sahivi na hizo changes wamefanya leo. Kama unaendelea kubisha fanya booking ya over 31dayz ukipata pungufu ya laki 4 natoa hii thread leo leo kabla ya saa sita
upo sawa mkuu naona na kilo wamepunguza mpaka kilo 15
 
ATCIL io ni kampuni inajihusisha na nn? Hii mada inahusisha ATCL io yako ifungulie thread yake tutakuja kuchangia huko.
Haichukui hata uzito wa gramu moja ya kutumia akili yako kuelewa nilichoandika. Wewe na wenzako wa ATCL ni mzigo kwa Taifa. Akili na ubunifu hamna.Mna-survive kwa machungu na jasho la Watanzania kwa kubebwa na mtu asiye na vision Wala uelewa wa biashara ya usafiri wa anga.
 
Hilo shirika la ATCL alina mda mrefu kwenye biashara kwasababu aliendani na hari halisi ya uchumi wa wananchi, Mtu aende Mbeya kuenda na kurudi kwa 520k kufanya nini kuna biashara gani huku ya kurudisha hiyo gharama. Watabaki na abiria watchache sana ili route zita anza kufa automatically
Umechangia vizuri ila huo uandishi ni shiiida
 
Habari za leo wanajanvi.... tokea jana ndege yetu penda Air Tanzania nauli zake zimepanda kwa asilimia kubwa sana kutoka zile za awali.

Nimejaribu kununua tiket online kama kawaida yangu lakini bei niliyokutana nayo tofauti na sikuzote.

Nikaona isiwe taabu nikaenda ofisi zao za town, kufika pale wakanambia nauli ni kweli zimepanda.

Kwenda Mwanza na kurudi nilishazoea kupata bei nafuu ya laki 365,000 lakini jana nikakutana na kitu cha laki 420,000.

Kuna haja ya mamlaka husika kupitia tena hivi viwango vya nauli, vina tuumiza sana sisi wananchi.
Mtaelewa tu.

Ni hivi, ATCL imewekwa kimkakati kuua upinzani wa kibiashara uliokuwa unasababisha bei kuwa nzuri.

Upinzani unavyozidi kufa, ndivyo nauli za ATCL zitakavyozidi kupanda. Kwa sababu.

1. ATCL itazidi kuelekea kwenye monopoly. A monopoly industry company inajipangia bei yenyewe bila kuogopa upinzani.

2. ATCL inaendeshwa kisiasa, si kibiashara. Maamuzi makubwa yanatoka kwa wanasiasa, hususan Magufuli. Hapo kampuni kupata hasara ninjambo rahisi sana. Ikioata hasara itafidia vioi? Kwa kuongeza nauli.

Jiandae hata hiyo nauli mpya kuongezeka zaidi.

Tulipokuwa tunakemea ATCL kuendeshwa kisiasa wengi walikuwa hawaelewi. Walikuwa wanamsifia Magufuli.

Uzuri wa uchumi ni kwamba, in the long run, haufichi siri.
 
Habari za leo wanajanvi.... tokea jana ndege yetu penda Air Tanzania nauli zake zimepanda kwa asilimia kubwa sana kutoka zile za awali.

Nimejaribu kununua tiket online kama kawaida yangu lakini bei niliyokutana nayo tofauti na sikuzote.

Nikaona isiwe taabu nikaenda ofisi zao za town, kufika pale wakanambia nauli ni kweli zimepanda.

Kwenda Mwanza na kurudi nilishazoea kupata bei nafuu ya laki 365,000 lakini jana nikakutana na kitu cha laki 420,000.

Kuna haja ya mamlaka husika kupitia tena hivi viwango vya nauli, vina tuumiza sana sisi wananchi.
naona ombi lako wamelisikia wamerudisha fare za zamani.
 
Back
Top Bottom