Air Tanzania yasimamisha Ndege zote za Airbus A220 kutokana na matatizo ya injini


..hii biashara haipaswi kufanywa na nchi masikini kama Tanzania.

..nchi tajiri zenye uwezo wa kumiliki mamia ya ndege ndio zinaweza kumiliki shirika la ndege na kupata faida.

..kwa afrika ni ethiopia peke yake ndio anaendesha shirika la ndege kwa faida, na wenyewe wana bahati kwasababu shirika lao lilianzishwa zamani sana mwaka 1945.
 
Watoe ufafanuzi basi,engine ni mbovu,au maintanance costs ni kubwa au kuna hujuma,maana nijuavyo hizi ndege bado ni mpya sana,shida ni nini
Kuna jambo nyuma ya pazia , tumekua kama mbuzi wanaovunja nyumba yao. Hii nchi ni vyetu tuithamini na watu na vitu vilivyomo. Hakuna Tanzania nyingine. Hata tukiihujumu tunajihumu wenyewe
 
Kulikuwa na A220 moja ambayo bado ipo operational hata jana ilikuwepo mwanza nayo imekuwa grounded? kinachoshangaza hata zile airbus mbili zilizopokelewa znz last year nazo zipo grounded,5H-TCL na 5H-TCM sasa tuelezwe ni manufacturer's defect au ni hours za engines or what.P&W.pia kiuhalisia mashirika kama yetu yangejikita kwenye fleet za Boeing na Q400 tu,hizi ndege toleo jipya zitatusumbua, boeing 737 hata (Fundi wa Ilala anatengeneza (joke) .Swala hili la kuground ndege litaleta crisiss sana maana q400 haziwezi kufidia deficit husika
 
Now days Technologies mbalimbali zina kuwa na so many bugs kabla azijawa OK and 100% OK. Ziwe simu (iphone 14 mfano) ndege kama zile Max (mojawapo ya Eithopia airline ilioanguka na kuuwa watu- mpaka leo Boing wamestopisha model ya max zaidi ya 1000 kuruka duniani kote) kinachotakiwa ni kutokimbilia nunua haya ma high tech gadgets wakati tu zikitoka mpaka bugs zote ziwe cleared
 
Hili unalosema wwe lipo kwenye Mkataba wa manunuzi ya hizo Ndege!? Au ndiyo limejulikana Sasa!!??
 
Mafisadi wameisha andaa mpango kazi (ila nasikia Rostam kanunua ndege zake hataki ushindani kabisa 😭😭😭pole sana tanganyika yangu
Unasikia lakini hujui lolote, Rostam ameinunuwa kampuni ya coastal aviation, ni vile vindege vya kuruka na kutuwa mbugani au Zanzibar, Mafia na sehemu nyingine au kukodi mtu binafsi ikupeleke sehemu.

Rostam hayupo kwenye ushindani wa biashara ya ndege msimpakazie kila ujinga wenu.

Biashara ya charter plan ni maalum kwa sehemu ambazo ndege kubwa haziwezi kutuwa au hakuna route kabisa.

Mshindani wa ATCL ni Precision tu baada ya Magufuli kuiuwa Fast jet kwa chuki zake za kishamba.
 
Uko sahihi. Ethiopia Airlines wana Fleet ya Engines ambazo hutumika during such emergencies. Hawakodi.
 
Si kwamba Ethiopia INA bahati, Bali Ethiopia haijawahi kutawaliwa, siyo koloni la nchi yeyote ile.
 
ℍ𝕚𝕝𝕚 𝕝𝕚 𝕓𝕚𝕒𝕤𝕙𝕒𝕣𝕒 𝕝𝕚𝕟𝕒𝕥𝕦𝕥𝕚𝕒 𝕙𝕒𝕤𝕒𝕣𝕒 𝕥𝕦...𝕟𝕒 𝕓𝕒𝕕𝕠 𝕄𝕒𝕫𝕒 𝕜𝕒𝕒𝕘𝕚𝕫𝕒 𝕟𝕪𝕚𝕟𝕘𝕚𝕟𝕖 5.

ℕ𝕕𝕖𝕘𝕖 𝕤𝕚𝕠 𝕍𝕚𝕥𝕫 𝕛𝕒𝕞𝕒𝕟
 
Hili unalosema wwe lipo kwenye Mkataba wa manunuzi ya hizo Ndege!? Au ndiyo limejulikana Sasa!!??
Lazima liwepo ili usije ukarusha Ndege beyond estimated safe hours. Ukidharau ni tatizo lako. Tatizo kubwa Manufacturers wa Ndege huwa hawana stock ya Engines. Kumbuka kuwa Ndege zinatengenezwa kwa order. Lakini kuna Makampuni ambayo yanafanya Biashara ya Leasing ya Ndege na Engines. Ni utaratibu wa kawaida kabisa katika Aviation Industry.
 
Hizi engine za Pratty and Whitney zenye gearbox zilishalalamikiwa kuwa na matatizo. India waliamua kuwa ili ndege za aina hii ziweze kuruka angalau ziwe na engine moja ambayo iko modified.
Mimi naishauri serikali iwawezeshe Air tz kununua engine tatu angalau kila ndege moja iwe na engine moja mpya maisha yaendelee. Otherwise hazitopaki milele. If something has to be done, it has to be done now...
 
nahisi wanataka kuuwa shirikir ili Matajiri waingize ndege.AZZIZ nasikia anataka kuanzisha shirika lake
 
Engine options ni swala la airbus na sio air Tanzania ,
To the best of my knowledge a220 , ilikuja na engine options mbili , zote kutoka PW
 
Kwa kuwa tatizo ni engine , pratt and whitney nd wanatakiwa kulipa fidia
Kuna makala imeandikwa na mwandishi flani wa London anaikandia sana ATCL
 
Figisu sana hii nchi. Lengo wanataka ziharibike zaidi
 
Kampuni iliyowauzia hizo ndege itawafidia hasara hii?
Andiko limesema nn kuhusu suala la manufacturer kufidia hasara, umesoma news report yote mwanzo mpaka mwisho ???
 
Andiko limesema nn kuhusu suala la kufidiwa hasara, umesoma news report yote ukaielewa ???
Kwanza asante kwa kuitikia wito...nimekupenda zaidu😄

Maandiko ni mengi mno.
Kuna Andiko limeandikwa na mwandishi flani London linasema huu ni mwendelezo wa uzembe wa ATCL na upigaji.

Lakini kuna mahala wanasema ni kweli injini ziliwahi kusumbua hasa shirika la ndege za Korea, Misri na baadhi za nchi chache lakini sio tatizo kubwa kuifanya ATCL ione kuwa injini hizo sio salama.

Mambo ni mengi buana aaah
 

Lakini si umeona mashirika mengine ya ndege yanayotumia hizo injini na yenyewe yametakuwa kufanya hivyo? Au ni Mimi lugha inanipiga chenga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…