Mkuu
SemperFI , asante sana kwa story hii, kwanza, ukiondoa gazeti la the Citizen na Mwananchi, hakuna media ya Tanzania ina vichwa vya kuandika kitu kama hii!.
Humo kuna vitu Matinde hakusema ambavyo vinaligharimu taifa kwa ujuha tuu wa viongozi wetu, kununua ndege kwa cash kama unavyonunua nazi sokoni, wamama wa uswahilini wakinunua nazi wana ipasua pale pale kwa mnunuzi ili ikiwa mbovu inakuwa replaced, ukinunua nazi, ukaenda nayo nyumbani, ikotokea ni mbovu, imekula kwako!.
Manunuzi yote ya mitambo zikiwemo ndege hufanywa by order na kulipiwa by hire purchase, ili kutumika kama warranty na guarantee ya manufactures liability on defects, ukitokea kuna uharibifu wowote uliotokana na manufactures defect, ni manufacture ana gharimia. Ukinunua kwa cash, likitokea la kutokea, utajibeba!, hivyo ule ujinga wa kununua midege sokoni kama unanunua nazi, unai cost ATC na kutu cost Watanzania kwa ujuha tuu!.
Ujinga mwingine ni umiliki wa ndege kwa TGFA, halafu ATC inakodisha!. TGFA ni 100% government, ATCL ni 100% government, ATCL inakodisha ndege za TGFA, wakati wote midege hii iko grounded, yeye TGFA, anakula tuu kodi yake ya ukodishaji, ATCL inalipia midege iliyosimama, hivyo kwenye hesabu za ATCL kunaonekana ina operates on loss!.
Taarifa ya CAG ya mwaka huu imeonyesha ATC inaendeshwa kwa hasara na mpaka sasa deni la TGFA ni dola $132.77 milioni!. Halafu serikali inachota dola $194 milioni toka mfuku mkuu wa hazina kui bail out ATCL!, huu ni nini kama sio ujinga?!. Mama Samia asiukubali ujinga huu uendelee!. Mkataba wa ATC wa ukodishaji ndege za TGFA uvunjwe!, ATCL izitumie ndege bure, zikiwa kwenye operations na kuzalisha faida ndipo TGFA agaiwe faida, siku ndege ziko grounded hazizalishi kitu kama sasa, hizo Airbus, TGFA isilipwe chochote!.
Najua lengo la kuziweka ndege chini ya umiliki wa TGFA ni ku mitigate zisikamatwe na wadeni wa ATCL, nashauri, serikali yetu, lipeni madeni ya nchi, kuzuia ndege zetu kushikiliwa, kisha ipeni ATCL hiyo midege ili ATCL iwe huru kufanya chochote.
Ila pia tukubali tukatae ATCL bado kuna issues, mengine tusiseme kwa uzalendo, ila tusiendekeze ujinga kwa jina la uzalendo!.
P