Air Tanzania yasimamisha Ndege zote za Airbus A220 kutokana na matatizo ya injini

Katika kitu namsifu Magufuli ni kununua hizo ndege cash. Angechukua kwa kukopeshwa Leo mngetukana matusi yote kuwa kaondoka kaiacha nchi na madeni ya ndege. Ni Kama alijua vile
Huko alikonunua yaani kwa manufacturer alilipa cash lakini huku alikochukua fedha yaani benki ni mkopo hivyo deni lipo pale pale!
 
Kombora la Bashiru! Limetoa nyoka mapangoni. Hauoni matamko na ziara vimefumuka upya?
Wenye makombora inabidi wawe waangalifu tu kwamba Rais aliyepo madarakani sasa hivi hakutokana na uchaguzi; aliwekwa na Mungu baada ya yule aliyetokana na uchaguzi kuwa mmekataa. Mlipomkataa wenu mliyekuwa mmemchagua, Mungu alisikia malalmiko yenu akaamua aweke wa kwake yeye. Huyu sasa inabidi muwe waangalifu sana namna mnavyoenenda naye kwa sababu si nyie mliyemuweka, aliwekwa na Mungu ila kwa kuzingatia Katiba yenu. kwa hiyo kama kuna kitu mlishiriki, basi ni kwenye upande wa Katiba yenu tu kwamba Mungu aliamua kuifuata

Kikubwa ninachotaka kusema hapa ni kwamba Rais aliyepo madarakani hakutokana na uchaguzi bali "state of emergence". Sasa huwezi ukajua kama hiyo "state of emergence". ilishakuwa declared kuwa imeisha au bado ipo, wenye nchi ndiyo wanaojua hiilo

Maana unaweza ukawa unacheza na makombora halafu kumbe nchi bado iko kwenye "state of emergence" huku wewe ukiwa hauna taarifa. Hata hivyo Dr Bashiru ni mwanasiasa; achana na wanasiasa, esppecially kwenye nyakati hizi tunazoelekea elekea kwenye uchaguzi mwingine
 

Hatuwezi kuachana na siasa, si umeona hapa tunajadili Airbus A220 lakini tumeibukia kwenye siasa?
 
Sa itakuwaje njiwa wetu!!
 
Sasa wameziground bila kumtaarifu manufacturer? Wamwambie sasa!
 

inamaana hao ATCL hawakuwa na plan yakujua lini watafikia hizo flight hours ili kuwaweka tayari watalaam, vifaa, fund nk ili kupunguza hiyo downtime.

Kama walikuwa wanajua kuna flight hours ikifika basi tunapaswa kufanya maintenance ya engine kwa nini hawakuingia kwenye service exchange program na kuwa na standby engines tayari Tanzania ambapo time ikifika inapigwa remova, install and test chap na kuresume operation with minimum dowmtime?
 
Manufacturer ndio ameshauri zipark dunia nzima kwa sababu amegundua kuna tatizo la kiufundi ambayo ni fault ya manufacturer mwenyewe?. kama hivi basi manufacturer kwa utaratibu anacover maintenance and repair cost yote mpaka kumaliza tatizo.
ATCL wanaweza kufile claim kwa manufacturer kufidia hasara kipindi chote cha breakdown otherwise manufacturer atafute namna ya kufidia hasara hata kwa kuleta airbus za kukodi during maintenance period.
 
Kama ni manufacturer recommendation kila inapofika flight hours fulani kufanyike repair na maintenance fulani basi ni uzembe wa ATCL kutofanya proper maintenance schedule wa fleet zao.
 
Huko alikonunua yaani kwa manufacturer alilipa cash lakini huku alikochukua fedha yaani benki ni mkopo hivyo deni lipo pale pale!
Sii kila kinachonunuliwa kimechukuliwa mkopo. Sasa tumelipia ndege 5 zingine na hakuna mkopo uliochukuliwa ili kununua hizo ndege.

Nb: mikopo inachukuliwa, Ila sio kweye kila kitu
 
Kuna kitu kinaitwa limited liability, manufacture analipia cost ya fault only, not time, or bussiness uliyopoteza. Na hata ndege ikipata ajali, fidia ni limited kwa $100,000 kwa abiria aliyekufa na mizigo miwili ya cock pit each $100 x 2 jumla $ 200
na mzigo mmoja wa hand luggage $ 50 hivyo total fidia ni $100,250, hata aliyekufa ni bilionea Bill Gates na mzigo wake ulikuwa na diamonds za billions!.
P
 
Hujuma.
 
Watoe ufafanuzi basi,engine ni mbovu,au maintanance costs ni kubwa au kuna hujuma,maana nijuavyo hizi ndege bado ni mpya sana,shida ni nini
Zito aliwahi sikika kuwa ndege zilikuwa za mtumba[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hili lilijulikana mapema kabisa kwamba hili shirika linaenda kufa,hasa baada ya mnunuzi wa hiyo mindege kufariki.

Binafsi namkubali sana Magu kwa mambo mengi ya maendeleo. Nilipingana nae kwenye kulifufua hili shirika kwa ununuzi wa hiyo mindege. Ona sasa sidhani hata kama kuna faida yoyote imepatikana badala ya hasara. Akachukiza kwa kuliua shirika la ndege la wanyonge FAST JET. Tuombe sasa hili shirika la ndege la Fast jet liombe kibali haraka,iwe mbadala wa ATC. Hata hayo mandege wayakope wayarekebishe

Na hapo ujue upo uwezekano mkubwa wa mafisadi kuingilia na kuitafuna shirika,hasa ksbb kwa sasa hakuna msimamizi kwenye mashirika mengi aliyoyasimamia vizuri Magu. Yanafunwa hatari na mchwa kwa sasa. Mama hana habari.
 

kama contract wakati wa purchasing inazungumzia limited liability incase of manufacturer fault/error sina tatizo hapo.

Lakini kuna warrant policy sidhani kama nayenyewe itasimama hapo kwenye limited liability inapotokea manufacturer error within warrant time ( sina uhakika kama hizi airbus zimemaliza warrant au hapana).

USHAURI: ATCL wanapaswa kuwa na service exchange contract na manufacturer wa hizi engine pamoja na airbus incase wanashida kama hizi maana wamemonopolize airline business Tanzania na wanapopata hizi breakdown hali inakuwa worse kwa wasafiri.

Unapokuwa na service exchange programs maana yake unaweza kupewa engine ukaswap haraka uendelee na operations wakati engine iliyotolewa inakwenda kwenye repair na huo muda wa repair wewe unakuwa kazini ( hapa tunapunguza downtime ya ndege na kuwa stable kwenye operation).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…