Sasa wewe na ufipa mna tofauti gani? Nani kakuambia sija-research? Usibadilishe mjadala kuufanya personal. Mimi ninataka mazuri kwa Air Tanzania sio mambo nusu nusu kama wanavyofanya sasa hivi. Kila awamu kampuni inafeli kwasababu ya mawazo ya kijinga. Wewe unatetea waende Zimbabwe unajua wanaotoka Zimbabwe kuja bongo kabla ya Zimbabwe walikua wapi? Walikua Sauzi sasa kwanini tusiwachukue kutoka sauzi moja kwa moja mpaka tusubiri wafike Zimbabwe? Plus, sauzi imeendelea kiviwanda maana yake tutapata wafanyabiashara wengi wakusafiri sauzi kuja bongo na bongo kwenda sauzi tofauti na kutegemea watalii wa Victoria falls peke yake. Tumia akili unapojenga hoja, usiwe uadhihaki watu tu, mimi naipenda Tanzania na naitakia mema Air Tanzania