Habari ndugu wateja, pole kwa changamoto.
Tumegundua wateja wengi wanaongea utumbo wakitupigia simu, hivyo sasa ukitaka kuongea na sisi lazima ujue lugha ya kiingereza kwa ufasaha. Na kuonesha kuwa tupo siriasi na tunamaanisha katika hilo, tumewaandalia namba yenu maalum ili kuongea na sisi. Piga 101 kisha chagua 1>5>2>2.
Aliyeuliza kuhusu kuangalia salio la vifurushi piga *149*99*10*1#
Aliyeuliza kuhusu message kuchelewa kufika, ni kweli tulikuwa na hilo tatizo lakini mafundi wetu wameshashughulikia. Tulikuwa pia na tatizo la kulemaa kwa mtandao wiki iliyopita ambapo tatizo limeisha. Pia kulikuwa na tatizo la usikivu mbovu wa simu, yaani mtu anakuwa anasikika kama yupo kwenye chungu, nalo linaelekea kuisha kabisa.
Aliyeuliza kutopewa salio akinunua umeme, ndugu mteja unatutega? Ukiambiwa salio halitoshi manake utafute hela uweke! Ukitaka kujua salio tumia menu yetu ya airtel money. Kwani ukinunua umeme kupitia kupitia NMB huwa unapewa salio lililobaki kwenye akaunti yako?
NIMEJIBU KWA NIABA YA AIRTEL