Airtel Money huduma mbovu sana, haya mmeondoa kipendele cha kuongea na muhudumu kimya kimya

Airtel Money huduma mbovu sana, haya mmeondoa kipendele cha kuongea na muhudumu kimya kimya

Kuna wakati hawa jamaa siwaelewi kabisa yaani kwenye hii Airtel Money, ukinunua luku wanakuletea tu kuwa malipo yako yamefanyika bila kuleta balance ya akaunti yako baada ya muamala huo kufanyika. Ukitaka kufanya muamala kama salio halitoshi wanakutumia msg salio halitoshi bila kuonyesha salio lililopo.

Sasa ninataka kuongea na muhudumu kipengele cha kuongea na muhudumu kilichokuwa kinapatikana ndani ya namba 100 mmekiondoa kimya kimya bila kutupa taarifa wala njia mbadala, hata kwenye website yenu hamuonyeshi mabadiriko hayo.

Haya wadau napiga namba ngapi kuongea na muhudumu wa airtel kwa anayejua.
Hawa jamaa ni kero sana, hata walipokuwa na option ya kumpata mhudumu ilichukua si chini ya dk 30.

Vv
 
Imenikuta hii leo nimenunua Luku hawajaleta message nikawapigia ni maelezo tu
 
Yaaani UKIPATA SHIDA YOYOTE NA MTANDAO WA Airtel..jisort mwenyewe... Tafuta tawi la karibu upeleke SHIDA yako.

Ukisema eti uwapigie simu...HUTOWAPATA..kwanza hakuna hicho kitu kwenye huduma yao ya wateja ya kupiga 100
 
Back
Top Bottom