Airtel mtandao wa ovyo sana, mawingu kidogo tu hakuna huduma

Airtel mtandao wa ovyo sana, mawingu kidogo tu hakuna huduma

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Hata kama wamepata balozi mzuri wa kuwatangazia matangazo yao tatizo sio matangazo bali ni huduma.

Airtel money changamoto,kama una haraka huwezi kutoa pesa fasta ukaondoka.

Kupiga simu,wanatoa dk nyingi sana za kuwasiliana lakini unaweza kutumia dk mpaka 5 hamuelewani mnabaki kuulizana sikusikii vizuri... network inasumbua huku dk zikikata tu.
Sms unaweza kutuma asubuhi ikafika jioni.

Kwa mujibu wa TCRA takwimu za mwaka jana ni mtandao wa pili kwa watumiaji wengi nyuma ya Vodacom. Ni mtandao wa hovyo sana wasipobadilika naiona kabisa Halotel ikiipiku.
 
Unatumia simu gani, maana kuna wakati nilikuwa nawalaumu tigo kumbe simu yangu ya Tecno C9 ndiyo kimeo. Baada ya kuachana nayo Tigo hawasumbui, so simu pia ni tatizo
 
Unatumia simu gani, maana kuna wakati nilikuwa nawalaumu tigo kumbe simu yangu ya Tecno C9 ndiyo kimeo. Baada ya kuachana nayo Tigo hawasumbui, so simu pia ni tatizo
Asee...afu ndio hiyo hiyo ninayo
 
Mwenye data za tccl atuambie maana vifurushi viko juu hii mitandao mingine na speed zao ni mwendo wa konokono
 
Aisee nina line ya Airtel toka miaka ile wanaita celtel mara ikaja zain na sasa airtel hawajawahi kuniangusha hawa jamaa.
 
Aisee nina line ya Airtel toka miaka ile wanaita celtel mara ikaja zain na sasa airtel hawajawahi kuniangusha hawa jamaa.
Unaweza kudownload file ya 1Gb kwa mud gani?
 
Back
Top Bottom