AIRTEL 5G ROUTER NI UTAPELI NA WIZI WA MCHANA KWEUPE!
KWA WATEJA WA AIRTEL TANZANIA – ACHENI KUPOTEZA PESA ZENU KWENYE TAKATAKA!
Nimekuwa nikitumia huduma ya Airtel 5G Router (Namba:*** 571 239) kwa miezi kadhaa sasa, nikilipia Tsh 70,000 kila mwezi bila kukosa. Baada ya miezi minne ya hadaa, sasa hivi huduma imekuwa ni kero, dharau, na utapeli uliopitiliza.
HOJA ZANGU ZA MSINGI (MAKAVU LIVE):
MALIPO YA HUDUMA HEWA: Kila mwezi ninatoa 70,000 yangu ya jasho, lakini intaneti haifanyi kazi kabisa! Hata kufungua ukurasa wa YouTube ni muujiza. Je, hii ndio 5G mnayopigia kelele kwenye matangazo au ni usanii?
UHUNI NA UBAGUZI WA KIFAA:
Inakuwaje intaneti kwenye simu inakubali kwa kasi, lakini kwenye Router mliyoniuzia huduma inakuwa mbovu? Huu ni uhuni wa makusudi ili mteja anue vocha ya simu huku mmeshachukua 70,000 ya Router. Huu ni wizi wa kupangwa!
WIZI WA KUTUMIA DHIKI ZA WATEJA: Kuchukua pesa ya mteja bila kumpa huduma inayostahili ni DHULUMA. Mtu anajinyima ili apate huduma, nyie mnaichukua hela kama sadaka. Airtel mna njaa kiasi gani mpaka muishi kwa kutapeli wateja wenu?
ROUTER AU TAKATAKA? Hii router yenu haina maana yoyote ndani ya nyumba yangu zaidi ya kupoteza nafasi. Ni bora nikaivunje niitupe kuliko kuendelea kulipia upuuzi huu.
TAHADHARI KWA WATEJA WENGINE:
Kama unafikiria kununua Airtel 5G Router, KIMBIA! Utapoteza 70,000 yako kila mwezi na utaishia kupata maumivu ya kichwa na shinikizo la damu. Tafuteni mbadala, Airtel wameishiwa na wanatafuta hela za kujiendesha kwa kuibia wateja.
UJUMBE WANGU WA MWISHO KWA AIRTEL:
Msithubutu kunitumia meseji za kijinga za 'Template' (Copy & Paste) za kuomba radhi. Ninataka huduma niliyolipia ifanye kazi SASA HIVI, au rudisheni pesa yangu yote niliyopoteza. Hamuwezi kuendelea kuchukua hela za watu kwa huduma hewa. Mmetuchosha na utapeli wenu wa 5G ya mchongo!
#AirtelTanzania #Airtel5G #Utapeli #Wizi #HudumaMbovu #Tanzania #TCRA #HakiYaMteja
@AirtelTanzania
NIMEMALIZA! [emoji35][emoji35][emoji35]