Wakuu jana mida ya saa tatu usiku nilikuwa na salio la mb20 katika bundle yangu ya mb400 nikawa nadowaload kitu cha mb 300 lakini chaajabu nikadownload hadi mwisho, ni nilipo jaribu kuangalia salio nikapata ujembe usemao "Samahani,huduma haipatikani kwa sasa kwa sababu tunaboresha mitambo yetu.Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.Asante".
Nikazima pc na baadae kama saa 7 hivi nikawasha ili nitumie zile mb200 za ofa ya usiku ikakataa kuconnect yaani haina salio
Leo asubuhi najaribu ku activate kifurushi cha mb400 kwa kutuma neno INTERNET kwenda 15444 lakini napokea ujumbe ufuatao " Neno ulilotuma sio sahihi, Tafadhali chagua kati ya :- 10MB,25MB,50MB,150MB,250MB,500MB,1GB,2GB,5GB,15GB,30GB,SIKU,WIKI,MWEZI ama SALIO kwenda 15444.Asante.
Nimechek na website yao bado wanamaelezo ya bundle za zamani
Inakuwaje hapa wadau