mtunzasiri
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 1,446
- 988
Nimeshangazwa kidogo na huduma za mtandao wa Aitel nimekuwa nautumia kwa kitambo kidogo hatimae nikaibiwa simu nikabaki na laini yangu niliosajiri kihalali ikiwa pamoja nakuitumia kwa Aitel money sasa tangu niibiwe inafikia miezi miwili sijapata simu tatizo limekuja baada ya kununua simu na kuweka laini yangu ili nitumie nakutana na ujumbe kwamba laini yangu imezui kupiga simu, nikashauriwa nipige namba 100 kwa maelezo simu ndo haitoki, nikaenda quarity center kuona kama kuna huduma kwa mteja lakini nikajibiwa kuwa laini yangu kama sijatumia zaidi ya miezi miwili inarudishwa dukani na kuuzwa tena kumbuka pia kuwa niliweka salio na likaingia sasa wanazuiaje laini nilonunua kwa pesa yangu na kuisajiri kama halali yangu? je hawa ile sheria ya tra inayozuia kumuwekea mteja masharti haiwahusu?? na kama laini yangu ina aitel money nazo wanapeleka wapi wakati wanaiuza laini yangu?? anaejua kuhusu haya tujuzane...