Aisee kumiliki gari kumbe gharama hivi? Nimetumia 505,000/= kufanya service!!

Aisee kumiliki gari kumbe gharama hivi? Nimetumia 505,000/= kufanya service!!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila kajitahidi, mwanaume wa dar huwa hawagusagi hivyo vitu, grisi? Hell no
Kwamba kajifunza kitu😂😂😂
 
Juzi fundi aliniuliza mara ya mwisho kufanya service gari langu. Nikamwambia mie tangu niagize nikaanza kutembea nayo sijawahi kufanya intensive service mpaka ipate tatizo ndio naileta kwako.

Akashangaa sana. Akasema kawaida unaponunua gari either kwa mtu au kutoka nje, kabla hujaanza kuzurura nalo lifanyie service kwanza. Bila kujali aliyekuaa nalo alifanyia service lini. Labda hiyo gari iwe brand new.

Basi nikamwambia kesho (ambayo ishakua jana) nitaileta tuifanyie service. Kesho yake mapema tu nikatoa gari nje, nikafungua boneti, cheki oil na maji kwenye rejeta. Maji nikaongeza kidogo.

Nikatimba kwa fundi wangu mzuri pale Sinza Palestina. Tukaanza kazi. Uzuri step zote nilikuepo. Fundi ana vijana wake wawili. Namie nikawa pemben nawapiga tafu.

Wanafungua hiki, wananiambia kazi yake na kama kiko sawa wanasema kiko sawa. Wanafungua kile, kama hakiko sawa wanasema boss inabidi tubadilishe hiki, kimeisha sana.

Anyway, jioni nakuja kupewa mchanganuo wa gharama aisee nikasema "Bhagoshaaaaa mweeeee".

Ukiona mtu anaendesha gari kali barabarani kila siku mwamkie " shikamoo". Kumiliki gari inabidi ujipange aisee. Unakuta kampira au kachuma kadogo tu kanauzwa 65,000/=. Au kale kamkanda ka kwenye Steering wheel kana bei kubwa hadi nikashangaa!

Mchanganuo wake:
Vifaa, Fluids = 405,000
Ufundi = 100,000
Tip = 0
Jumla = 505,000

Fundi alisema gharama za vifaa hatuwezi ku-negotiate maana tumevinunua namie nikiwa nashuhudia. Gharama za Ufundi ndio tunaweza ongea.

Hata hivo kutokana na nilivokua nawaona vijana wakizama chini ya uvungu wa gari, wanamwagikiwa na oil, wanachafuka kinoma, wanafungua nati zingine zimekazwa kinoma, sikuona haja ya kugalaliza hela ya Ufundi.

Labda tu, safari hii sijampa fundi ile "Tip" ambayo nishagamzoesha.

ADDITIVE POINT:
Kitendo cha mie kuwasaidia mafundi wakati wanafanya service ya babywoka yangu imenifanya nijifunze vitu vingi sana kuhusu gari. Yaani hapa nilipo naweza kufungua boneti nikakuelezea kazi ya kila kidude, kila waya, kila pipe, kila chuma.

Matatito mengine madogo madogo nitakua nayamaliza mwenyewe home. Uzuri Toolbox ninayo.

Sio unakua kama Extrovert hata Fog Light ikiungua lazima aende garage pale Majengo Moshi.

Yaani mtu kama mng'ato anamiliki gari kali, lakin yeye anachojua ni kuwasha na kuondoka tu. Hata ukimuuliza hivi ukipiga honi ikawa hailii hatua ya kwanza utafanyeje, hajui!!!

View attachment 1578413
Umepigwa kwenye oil sill Ni elf tano
 
Mafundi hawana maana kmmmk, siku ambayo walininunulisha Oil ya litre 1 sh.15,000 wakati inauzwa 10K niliacha mchezo nao.

Wafungue kifaa kibovu wanipe naenda na Boda boda mwenyewe dukani 🤣🤣🤣! Tena sio duka la hapo gereji
Hiyo ndio kabali yao,jamaa hawanaga huruma aisee 😀
 
Mafundi hawana maana kmmmk, siku ambayo walininunulisha Oil ya litre 1 sh.15,000 wakati inauzwa 10K niliacha mchezo nao.

Wafungue kifaa kibovu wanipe naenda na Boda boda mwenyewe dukani [emoji1787][emoji1787][emoji1787]! Tena sio duka la hapo gereji
Ukiwaachia gari kwenda kufata spare dukani wanatoa kifaa kizima, then wanakuchomekea kifaa kibovu, ukirudi unakutana na stori mpya tena

Mimi nawaitaga nyumbani na ni baada ya kufanya whole check up ya gari youtube, then namwambia tatizo..
 
Kwamba kajifunza kitu[emoji23][emoji23][emoji23]
Nayo sio mbaya

Mwenzio mwaka mpya nataka kuagiza gari mpya, but be4 this, hii miezi miwili iliyobaki nataka nikae na rafiki yangu pale NIT, anipige brush kuhusu kifaa cha gari kikiharibika, huu mtumba mpya ukiingia bongo nakuwa expert sikanyagi kwa fundi tena, zaidi ya kufungua nut na kupachika kifaa kipya
 
Hayo ndiyo matatizo ya kuendesha gari huku ikiwa unahitaji service na mwisho wa siku utatumia pesa nyingi kwasabb gari sikuzote kitu kimoja kikiharibika basi na kingine kitafuata,
Hivyo vitu ulivyoorodhesha ni Ile Hali ya kukaa na ugonjwa Kwa muda mrefu matokeo yake ndiyo hayo unakuja kutumia pesa nyingi
 
Nayo sio mbaya

Mwenzio mwaka mpya nataka kuagiza gari mpya, but be4 this, hii miezi miwili iliyobaki nataka nikae na rafiki yangu pale NIT, anipige brush kuhusu kifaa cha gari kikiharibika, huu mtumba mpya ukiingia bongo nakuwa expert sikanyagi kwa fundi tena, zaidi ya kufungua nut na kupachika kifaa kipya
Miezi miwili utakuwa umejua kitu gani?
Wenzio wanasugua garage miaka 5 na bado wanachemka..
 
Mlolongo nakumbuka ulinifata inbox ukihitaji gari nakumbuka nilikutumia picha zake ukasema gari Yangu ni Carina ti ni ya kizamani,sasa sijui umepigwa gari tena ambayo umeanza kutumia pesa kiasi hicho...
Mkuu hiyo gari yako umenunua ya Aina gani?
 
Back
Top Bottom