Aisee! Mastaa hawa 10 walishikwa mkono wakajibeba kabisa...

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
Imekuwa ni kawaida katika siasa, biashara, michezo, muziki, filamu na mitindo, kila anayefanya vizuri upande huo, kuna mtu alimshika mkono au kumvutia kufanya mojawapo kati ya hayo machache.

Je, kwenye muziki wa Bongofleva hali ipoje? Wasanii wamekuwa wakishirikishwa kwenye nyimbo kila siku, lakini kuna wale ambao kufanya hivyo kulipelekea kuleta au kutengeneza majina mapya na baadaye kuwa makubwa kwenye muziki huo. Karibu.

1. Ben Pol > Darassa
Hakuna ubishi kuwa wimbo ‘Sikati Tamaa’ ambao Darassa alimshirikisha Ben Pol ndio uliomtoa mwenyewe kimuziki, licha ya huko nyuma kurekodi nyimbo kibao.

Baada ya miaka zaidi ya mitano Darassa alimshirikisha tena mkali huyu wa RnB katika wimbo uitwao ‘Muziki’ ambao ulipelekea jina la Darassa kuwa kubwa maradufu.

2. Alikiba > Ommy Dimpoz
Wawili hawa walikutana G Records na Prodyuza KTG akawatengenezea mdundo wa wimbo ‘Nai Nai’ ambao Ommy Dimpoz alimshirikisha Alikiba, baada ya hapo jina la Ommy likawa maarufu kila kona.

Na baada ya miaka mingi walitoa wimbo mwingine uitwao ‘Kajiandaye’, huku Alikiba akija kumsainisha Ommy Dimpoz ndani ya Rockstar Africa wakati akiwa kiongozi katika lebo hiyo.

3. Belle 9 > Young Killer
Ngoma yake iitwayo ‘Dear Gambe’ aliyomshirikisha Belle 9 ndiyo ilimtoa na kumpa tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2013 kipengele cha msanii bora chipukizi kwa wakati huo.

Kabla ya wimbo huo, Young Killer ambaye alikuwa akisifika kwa uwezo wa kuandika mistari kwenzi na kuichana, tayari alikuwa amesharekodi baadhi ya nyimbo na Maprodyuza kama D Classic na Duke Tachez.

4. Mwana FA > Maua Sama
Mwimbaji Maua Sama mwenye sauti ya kipekee alikuwa amesharekodi wimbo wake ‘So Crazy’ na Prodyuza mwingine huko Moshi, lakini hakufanya vizuri.

Alipokuja kukutana na Mwana FA wakaifanya upya ngoma hiyo chini ya Prodyuza Marco Chali, na ndio ikawa tiketi ya Maua Sama kusikika kwenye Bongofleva hadi sasa.

5. Belle 9 > Shetta
Wimbo ‘Nimechokwa’ ndio uliomtoa Shetta kimuziki, ni wazi sauti ya Belle 9 kama msanii mkubwa kwa wakati huo ilipelekea wengi kuipenda ngoma hiyo. Kutokana na mafanikio yake, haikuwa ajabu Shetta kuendelea kufanya kolabo na wakali wa kuimba kama Dully Sykes, Tundaman, Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Jux n.k na kuzifanya nyimbo zake kuwa kubwa.

6. Jux >Mabeste
Rapa huyu mwenye swaga za muziki wa Genge kutoka Kenya, alitambua sauti ya Jux inafaa katika wimbo wake ‘Baadaye Sana’ ambao ulipokelewa kwa mikono miwili kwenye Bongofleva.

Kolabo hiyo ilirekodiwa na marehemu Prodyuza Pancho chini ya B’Hits Music Group ambapo kwa wakati huo Jux na wenzake kutoka kundi la Wakacha nyimbo zao nyingi walirekodia hapo.

7. Rich Mavoko > Stamina
Rapa huyu anayetamba na kundi Rostam kwa sasa, alimshirikisha Rich Mavoko katika wimbo wake uitwao ‘Kabwela’ na ndipo akatoka kimuziki ingawa alikuwa ameurekodi awali zaidi ya mara tatu.

Kufanya vizuri kwa wimbo huo kulipelekea Stamina kuona umuhimu wa kuchanganya Hip Hop na RnB, ndipo akamshirikisha Jux katika wimbo ‘Alisema’ ambao nao ulifanya vizuri zaidi.

8. Rama Dee > Nikki wa Pili
Tayari Nikki wa Pili alikuwa ameshasikika kwenye wimbo ‘Niaje Nivipi’ alioshirikishwa na kaka yake, Joh Makini aliyekuwa akitamba wakati huo na kundi la River Camp Soldiers.

Ila bado Nikki alikuwa hajasikika yeye binafsi, ndipo alipotoa ngoma yake iitwayo ‘Good Boy’ akimshirikisha mkali wa RnB, Rama Dee ambayo ilimtambulisha na kumuongezea mashabiki.

9. Tundaman > Dogo Janja
Kilikuwa ni kipaji kipya ndani ya Tip Top Connection kwa wakati huo, ambapo Dogo Janja alikuwa chalii mdogo tena mwanafunzi wa shule ya msingi ila mwenye uwezo mkubwa wa kuchana.

Alimshirikisha Tundaman kwenye wimbo wake ‘Anajua’ ambao alikuwepo pia na Madee, ndio ulimtambulisha kwenye muziki wa Bongofleva na mengine yakabaki kuwa historia.

10. Ommy Dimpoz > Vanessa Mdee
Ingwa tayari Vanessa alikuwa ameshasikika kwenye baadhi ya ngoma kama ‘Money’ yake AY na ‘Press Play’ ya DJ Choka, bado mashabiki wengi walikuwa hawajamuelewa sana.

Hakuna ubishi kuwa wimbo ‘You and Me’ alioshirikishwa na Ommy Dimpoz ulimpa jina kubwa kwenye muziki wa Bongofleva, ndipo akaja kutoa wimbo wa kwanza alioupa jina la ‘Closer’.

©Mwananchi
 
Aisee Mabeste sijui alifail wapi maana jamaa nilikuwa nakubali sana anavyochana. Napenda sana ile Ngoma yake aliyomshirikisha tena Jux inayoitwa - Sirudi tena.

Nilikuwa napenda uandishi wake wa kuchanganya kingereza na kiswahili. RIP Pancho Latino, jamaa alikuwa mkali ila mziki haukumlipa kwa kiasi anachostahili.
 
Vijana wa Arusha siku hizi wamepatwa na pepo la umarioo. Wanapenda sana kitonga.

Mabeste ana kipaji ila alivyokuja kumuona yule, akapunguza juhudi akabaki kulelewa kwasababu demu mwenyewe alikuwa fighter.
 
Vijana wa Arusha siku hizi wamepatwa na pepo la umarioo. Wanapenda sana kitonga.

Mabeste ana kipaji ila alivyokuja kumuona yule, akapunguza juhudi akabaki kulelewa kwasababu demu mwenyewe alikuwa fighter.
Hivi mkuu ni nini kilitokea mpaka akina mabeste, na akina vanessa wakaondoka bhits na baada ya hapo mabeste ndiyo akawa basi tena
 
Hivi mkuu ni nini kilitokea mpaka akina mabeste, na akina vanessa wakaondoka bhits na baada ya hapo mabeste ndiyo akawa basi tena
Sijui exactly, ila nahisi itakuwa ni baada ya HarmyB kupandisha bei ya kurekodi.

Kumbuka seke seke la AY na FA baada ya HarmyB kutoka alipwe 2M kwa wimbo.
 
Sijui exactly, ila nahisi itakuwa ni baada ya HarmyB kupandisha bei ya kurekodi.

Kumbuka seke seke la AY na FA baada ya HarmyB kutoka alipwe 2M kwa wimbo.
Oh, kweli nimekumbuka. Studio uwa zinapanda na kushuka naona sasa anayevuma s2kizzy
 
Oh, kweli nimekumbuka. Studio uwa zinapanda na kushuka naona sasa anayevuma s2kizzy
S2kizzy mwenyewe anafanya kazi sehemu moja tu siku hizi.

Mara nyingi studio ndio zinabebwa na wasanii na ndio maana wasanii hasa wakubwa wana kiburi, studio nyingi wanarekodi bure.

Producer akiwadai pesa wanahama.

Weusi walihama The Industry wakaenda kwa Luffa.

Alikiba alihama Combination akaenda kwa Moco Genius.

Diamond alikuwa anafanya kazi na Sheddy clever, tangu ampige chini nae kapotea. Kuna kipindi alitaka kusimamia wasanii chini studio yake lakini mpaka leo bila bila.

Lamar yupo na studio yake hata haina kazi.

Kazi ya production bongo bado hailipi wala kuheshimika. Producers wanaishi kwa hisani ya msanii.

Bora hata maDJ wameanza kujiongeza.
 
Kweli kabisa na nadhani jina la s2kizzy linabebwa na kufanya kazi na diamond. Niliona ana wasanii wake sijui wa pluto republic ila sidhani kama sokoni wanafamya vizuri.
Weusi hata bhits waliwahi kuwepo.
The industry nadhani wamebaki zaidi kujitengenezea nyimbo zao sijasikia msanii mkubwa hivi karibuni kagonga nyimbo pale.
Sema maisha ya uproducer bongo ni mafupi sana mtu akihit ajiandae kwa mambo mengine
 
Vanessa Mdee alikuwa anakimbizana na Diamond Platnumz hadi pale aliponogewa na nyama ya mnigeria ndio ukawa mwisho wa habari yake
Baada ya kumfanyia figisu mpaka kaamua apumzike kimziki
 
Mkuu nyimbo zake za hivi karibuni km qualify na back off mbn ziko vizuri sn
 
Hili Pepo la wasanii kuwakimbia maproduzer na wengine kuanzisha productions zao wenyewe linahamia taratibu Kwa music video directors..mambo yanaanza kwenda mrama mdogomdogo,soon mambo yatakuwa mabaya sn Kwa bahadhi ya directors
 
Kuna moja nimeiona juzi nmependa sema nahs hapati airtime ya kutosha au muda wake ushaisha au hana ukarbu na wale waliokuwa wanazipga kwenye media
Wimbo wa back off,aliyekuwa mkewe alienda kumshitaki usipigwe maredioni unamdhalilisha..aliimba baada ya mkewe kutembea na Yule dogo aliyekuwa mshikaji wake na kumpora na kukimbia nae kabisa Hadi mimba akapata huko nje

Nadhani hiyo Nayo ni sababu ya kutosikika,Ila mm ninao kwenye device yangu,ni mkali sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…