TANZIA Aisha Madinda afariki dunia

TANZIA Aisha Madinda afariki dunia

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,785
IMG_7994.jpg

Aisha Madinda wakati wa Uhai wake


Aliyekuwa Mnenguaji na Muimbaji wa Bandi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda amefariki dunia hivi punde Jijini Dar es salaam. Habari imethibitishwa na mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta Asha Baraka. Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.

" Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea". Amesema Asha Baraka

Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina

Kwa taarifa niliyoipata muda huu toka Clouds Fm. Amefikishwa Mwananyamala Hosp, akiwa tayari keshapinda.
madinda.jpg
 
R.I.P Aisha
Hivi ndo yule mnenguaji au?maana Aisha madinda na asha baraka majina yao huwa yananichanganya
 
Imeandikwa kila nafsi itaonja mauti. na kwa hakika umauti ni mawaidha tosha kwa wenye kuamini.maisha ya duniani ni mafupi sana ila wanadamu tunajisahau sana na maisha haya ya mpito. anza leo kumuabudu Muumba wako usisubiri kesho huenda sasa hivi ndio ikawa pumzi yako ya mwisho.
 
Back
Top Bottom