Aishi Manula akatwa na kioo mkononi muda mfupi kabla ya mechi dhidi ya Geita Gold

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kipa wa Simba, Aishi Manula amepata majeraha ya kukatwa na kioo kwenye mkono akiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa timu hiyo dhidi ya Geita Gold, leo Mei 22, 2022.

Tukio hilo limetokea wakati Manula akiwa ni mmoja wa wachezaji waliotakiwa kuanza katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara Jijini Mwanza.

Aliangukiwa na kioo hicho ambacho kilivunjika baada ya kuegemewa na mashabiki waliokuwa nje ya chumba hicho, Manula amepatiwa matibabu na anaendelea vizuri.

Nafasi yake imechukuliwa na Beno Kakolanya. Kumbuka kuwa zimesalia siku chache kabla ya Simba kucheza dhidi ya Yanga katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam kwenye Uwanja huohuo wa CCM Kirumba.
 
Sasa kuumia kwake na kuihusisha Yanga unatakusemaje??!!--- au hapo kuna mkono wa kamati ya ufundi ya Yanga??!!
 
Tarehe 28 mbali hiyo chupa ilikuwa imkate mchana wa tarehe hiyo.
 
Ni yule alikuwa akikodolea kwa matamanio makalio mapana ya makonda?
 
Sasa kuumia kwake na kuihusisha Yanga unatakusemaje??!!--- au hapo kuna mkono wa kamati ya ufundi ya Yanga??!!
Ile Alphard nyeusi iliyowabeba Manara, Mayele na wengine kwenda kwa mganga mtaa wa Ipogo......
 
Sisi Tunamuombea Yeye Na Chama Wapone Haraka Na Ikiwezekana Wacheze Tar 28...Hatutaki Visingizio Vya Flani Hakuwepo Tukishawapasua...Na Ikiwezekana Pia Morrison Arudishwe.
 
Yanga tunamtaka uyo uyo Manula maana ni pazia na yale mashuti ya Ambundo kaona azuge kuumia mapema
 
Danganya totooooo.
Wazee wa moto bhana.
 
Hii imenikumbusha wakati wa vita vya Kagera, kuna askari walikuwa wanajipiga risasi mkononi ili warudishwe kutoka frontline, they were many.
 
mpeni mkataba mpya acheni kusinizia upuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…