JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tukio hilo limetokea wakati Manula akiwa ni mmoja wa wachezaji waliotakiwa kuanza katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara Jijini Mwanza.
Aliangukiwa na kioo hicho ambacho kilivunjika baada ya kuegemewa na mashabiki waliokuwa nje ya chumba hicho, Manula amepatiwa matibabu na anaendelea vizuri.
Nafasi yake imechukuliwa na Beno Kakolanya. Kumbuka kuwa zimesalia siku chache kabla ya Simba kucheza dhidi ya Yanga katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam kwenye Uwanja huohuo wa CCM Kirumba.