Aisome RAS wa Tanga

Aisome RAS wa Tanga

Tumbu

Senior Member
Joined
May 27, 2021
Posts
109
Reaction score
96
Wiki mbili zilizopita iliripotiwa habari ya uvunjwaji wa kanuni katika matumizi ya fedha kwa manaibu makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) wa wilaya za Tanga na Mkinga.

Wahusika hao wamekuwa wakisainiana hela bila kushirikisha watumishi wengine ndani ya ofisi hizo jambo ambalo ni kinyume cha taratibu. Tena eti watu hao bdio wanaoangalia nidhamu ya watumishi wenzao. Hao wanaweza kutenda haki?

Baadae TSC makao makuu waliwaleta watu hao kufuatilia watu wao kufanya ufuatiliaji. Wajumbe hao hawajafuatilia upotevu wa fedha na taratibu kutofuatwa. Wamefika Tanga na kuwabana watumishi kwamba kwanini wanatoa siri za ofisi. Je hiyo nayo ni siri ya ofisi?

RAS kuwa makini na wafujaji hao na wavunja kanuni kwani wanaweza kushawishi watu wanaokuja kuwachunguza. Watajivisha ukada na hatimaye usipokua makini unaonekana umepwaya.

Waangalie sana watu wa Tanga
 
Mkuu kwani mchakato wote wa uchunguzi uliushuhudia wakati unafanyika na hao wajumbe kutoka makao makuu? Na je, ripoti yao umeiona? Nionavyo mimi hao wajumbe hawawezi kutoka DOM na kuja Tanga kufanya hicho ulichokisema.
 
Hizo ni issue za kimkoa,huu ni mtandao wa kimataifa, embu jiratibu
 
Mkuu kwani mchakato wote wa uchunguzi uliushuhudia wakati unafanyika na hao wajumbe kutoka makao makuu? Na je, ripoti yao umeiona? Nionavyo mimi hao wajumbe hawawezi kutoka DOM na kuja Tanga kufanya hicho ulichokisema.
Walioingia wanadai wamelazimika wakubali kumsafisha huyo mama ambaye ni naibu katibu kwani eti wao nimakada na wanazo ndoto za kugombea nafasi mbalimbali kwenye siasa.
Sasa sijui wanataka kugombea kwasababu zipi wakati hata hela waliyotakiwa kusaini imeliwa bila kushirikishwa na wanamsafisha mtu wakiwa shingo upande.
Ninarudia kusema tunaisubiri ripoti ya makao makuu tuone je watawabeba hapo wavunja utaratibu au watasimama kwenye ukweli?
 
Yes, kusubiri ripoti ndiyo jambo la msingi.Ninawafahamu baadhi ya watumishi wa pale TSC makao makuu, ni watu makini sana katika utendaji wao wa kazi.Natarajia kuona haki inatendeka ktk Jambo hilo.
 
Yes, kusubiri ripoti ndiyo jambo la msingi.Ninawafahamu baadhi ya watumishi wa pale TSC makao makuu, ni watu makini sana katika utendaji wao wa kazi.Natarajia kuona haki inatendeka ktk Jambo hilo.
Kumbuka pia hao TSC makao makuu ni binadamu na wana njaa na tamaa.
Utakapojua kama walimu wanamatatizo ni namna watakavyo washuhulikia hao wezi wao walio waweka
Wamekua wakiiba muda mrefu kumbe halafu hao makao makuu hawajui wala hawaelewi. Hawapo makini na maslahi ya umma zaidi ya matumbo yao
 
Huyo RAS wa Tanga amelala bado maana nimeona uzi mwanajukwaa ameandika akisema yupo mwalimu mmoja ameshtakiwa kesi ya uhujumu uchumi lakini bado ni Afisaelimu kata eti.
Huyo RAS Tanga wanahasara
 
Back
Top Bottom