Ajabu: Mbunge Florent Kyombo (CCM), adai Kagera inapakana na Sudan Kusini

Hivi huyo mbunge yupo bunge moja na mh. Rose Tweve!!???
Yaani "pumba" na "mchele" vyote vinakaa jengo moja kweli!!!
 

CHANZO CHA MATATIZO (# code) wanasemaje?
 
Huko bungeni kweli watu waingie kwa interview.

Sasa mtoto wa sekondari akisikia kiongozi wake anaongea na kaingia bungeni wanafunzi watakua na ari ya kusoma kweli

Wapatiwe mitihani kuingia bungeni iwe chini ya mia ikiwezekana matokeo yatangazwe na necta kabisa
 
Kagera na Kilimanjaro tumesoma sana kuliko wengine hao ndo wasomi wetu tangu Uhuru washobokele Wabikwata?
 
Hivi ni viashiria (Indicators) jinsi elimu yetu inavyozidi kushuka ubora.
Ukute huyu amemaliza F4/ F6 na ameenda College.
Kizazi cha sasa kina Low IQ
Kizazi kipi kipo bora mbona wale wazee walienda Madagascar kununua novida na kunywa hadharani hata kabla ya kupimwa bora wangeenda na boat waliwasha ndege kabisa...
 
Huyo Kyombo alihamia CCM akitokea CHADEMA!
Sio kweli! Huyu aligombea Ubunge akitokea kwenye Ukurugenzi wa Wilaya...nadhani Mvomero. Na alianza kugombea 2015...akakosa na ndio wale makada waliopelekwa na JPM kwenye ukurugenzi na ukuu wa wilaya....Hivyo ni CCM toka kitambo sana.
 
Hayo ni matokeo ya kuingiza watu Bungeni kwa nguvu kupitia chaguzi zisizo huru.
 
Mimi nakubaliana na huyo mbunge na sababu zangu ni hizi:
1) Muda anaopewa mbunge kutoa hoja zake unakuwa mdogo, hivyo mambo anayo ongea yana kuwa ni summary ya kitu anachotaka kukielezea. Hivyo anatuachia sisi wasikilizaji kupanua hayo mawazo yake.
2) Katika muingiliano wa biashara - kutoka Tanzania kwenda Sudani ni mkoa wa Kagera uliopakana na Sudani ukipita nchi ya Uganda! Hapa Kupakana sio kutenganishwa na mpaka wa mstari = yaani unene wa msitari! - sasa unene wa mpaka kati ya Kagera na Sudan ni sehemu inayo kaliwa na nchi ya Uganda!
3) hii ni mwendelezo wa 2) juu - Mpaka unaweza ukawa mm au ndogo zaidi, cm, Meter au kilometers nyingi tu lakini baada ya umbali huo kuondolewa, sehemu mbili hizo zinapatikana.
4) Kuliko kumkejeri just jiongeze utaona kiEastAfrika, Kagera inapakana na Sudani kuliko ilivyo Mtwara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…