JumaKilumbi
JF-Expert Member
- Sep 7, 2022
- 432
- 507
AJABU YA UTEUZI WA WAZIRI MKUU UINGEREZA 🇬🇧
Na JumaKilumbi,
05.09.2022
Uingereza ni nchi ya kidemokrasia, Demokrasia iliyokomaa hasa, ila ina Malkia mwenye mamlaka ambayo huizidi katiba kwa sehemu.
Kuna mengi ya kuuliza kuhusu ‘Demokrasia’ yao ila leo tuzungumze kuhusu kupatikana kwa Waziri Mkuu wao.
WAZIRI MKUU NI NANI HASA?
Ni kiongozi wa Serikali mwenye mamlaka ya teuzi zote za juu; Teuzi za mabalozi, Teuzi za Baraza la mawaziri na Teuzi za maafisa wa Jeshi.
Pia ana mamlaka juu ya Utungaji wa sheria Utungaji wa sera na Utumaji Majeshi nje.
Muhimu ya yote ana sikio la Malkia, aweza mshauri kitu Malkia naye akafuata, kama vile Kuvunja Bunge!
WAINGEREZA HAWACHAGUI WAZIRI MKUU WAO
Tofauti na Tanzania 🇹🇿 ambapo huku kila baada ya miaka mitano tunapiga kura kumchagua kiongozi wa serikali, Rais, wao humchagua mtu mmoja tu, Mbunge.
Hao Wabunge wakienda Bungeni hujitazama, Chama kipi kitakuwa na Wabunge wengi?
Kama ni Labor basi Malkia atamteua kiongozi wa chama cha Labour kuwa Waziri Mkuu, na kama ni Conservative vivyo hivyo.
Kwahiyo WAINGEREZA HAWCHAGUI WAZIRI MKUU!
SAKATA LA KUANGUKA KWA BORIS JOHNSON!
NB: Boris Johnson - BJ
Alipoulizwa BJ akadai hajui chochote kuhusu tabia za Mnadhimu Pincher, lakini watu wakazidi kusema kuwa BJ alikuwa anajua fika.
Baadae BJ alikiri kuwa alikua anajua tabia ya mnadhimu wake na akaomba radhi kumteua. Hili likamtafuna polepole.
👉 Mwezi may 2020 walifanya ‘party’ kwenye bustani iliyopo Downing street (makazi ya Waziri Mkuu) na BJ alikuwepo.
👉 Mwezi Juni 2020 BJ alienda kwenye sherehe ya ‘birthday’ yake, ambapo ilisemekana kanuni za ‘Lockdown’ zilivunjwa.
Yote ilikuwa siri lakini Novemba 2021 gazeti la ‘Daily Mirror’ likaripoti matukio haya, ripoti nyingi zaidi zikafuata ila alipoulizwa BJ alisema kanuni za ‘social distancing’ zilifuatwa! Na uongozi wa Makazi ya ‘Downing Street’ (makazi na ofisi za Waziri Mkuu) walisema hakukuwa na ‘party’ yoyote.
Wiki moja baadae Video ikasambaa mtandaoni kumuonesha mkuu wa kitengo cha habari na mwenzie wakifanya mzaha kuhusu kanuni za ‘lockdown’. Shughuli ikaanzia hapo, Bunge likaunda kamati kuchunguza nini hasa kilitokea.
Miezi ikapita Januari 2022 ripoti ikatoka ikieleza kinaga ubaga kuwa sheria za ‘lockdown’ zilivunjwa kwenye ‘party’ ya mwezi mei 2020. BJ akajitokeza kukiri kuwani kweli alienda kwenye ‘party’ na kuomba radhi.
Iliposambaa ile video ya mkuu wa kitengo cha habari BJ aliunda chombo cha kuchunguza ambacho kilitoa ripoti mwezi mei 2022 ambayo ilieleza kuwa Watu walilewa sana kwenye ‘party’ hiyo na wengine walifanya vitendo vya dharau kwa wafanyakazi za usafi na ulinzi jengoni hapo.
Mzozo ukazuka mitandaoni watu wakiulizana kama BJ alikutana na babae Evegny bwana Alexander Lebedev aliyekuwa afisa wa KGB. Kama walikutana je walijadili nini? BJ hakutoa siri kwa jasusi huyo? Maafisa wengine walikuwepo?
Maswali yalikuwa ni mengi ila majibu hayakueleweka.
Tangu 2018 hilo lilibaki kuwa kitendawili, mwezi Juni 2022 BJ aliwekwa kikaangoni na kamati ya Bunge iliyolivalia njuga skendo hiyo. Baada ya kuulizwa kama walikutana na jasusi huyo alikubali kuwa alikutana nae.
Alipoulizwa kama walijadili masuala ya usalama ya NATO na lile suala la mauaji ya majasusi wa Urusi BJ alisema “kwa nijuavyo hakuna masuala ya kiserikali yalijadiliwa”
Hilo likaisha hivyo lakini vichwani mwa watu bado maswali yalikuwa ni mengi.
ATHARI ZA SKENDO
Baada ya mambo kuwa dhahiri BJ akapoteza uungwaji wa wananchi wengi, Wabunge wa Upinzani na chama chake wakataka ajiuzulu. Wakafikia kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae, BJ akashinda kura hiyo.
Lakini tarehe 7 Julai 2022 BJ akatangaza kujiuzulu nafasi ya Kiongozi wa chama chake cha ‘Conservative’ na Uwaziri Mkuu, lakini ataendelea kuwa Waziri Mkuu mpaka atakapopatikana mrithi wake.
KILICHOFUATA…
Basi chama chenye serikali kiliendesha mchakato wa kupiga kura kumchagua Kiongozi mpya wa chama hicho, ambaye moja kwa moja ndiye atakaekuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.
Mchakato ulimalizika kwa Bi. Liz Truss kushinda nafasi hiyo na 6.09.2022 alienda Scotland kwenye kasri la Balmoral alipokuwa Malkia Elizabeth II kuagizwa kuunda serikali, Maana Malkia ndiye humtafuta mtu wa kuunda serikali.
KWAHIYO WAZIRI MKUU ANAPATIKANAJE?
Malkia ndiye anateua Waziri Mkuu, na moja ya sifa za mtu huyo ni awe na wafuasi wengi Bungeni, kwa kesi hii mtu toka chama cha Conservative ndiye mwenye wafuasi wengi Bungeni. Hivyo Mchakato wa wanachama 160,000 wa ‘Conservative’ kupiga kura kumchagua Kiongozi wao mpya ndiyo kumechagua Waziri Mkuu mpya wa Uingereza yenye watu Milioni 67.

- SKENDO YA CHRIS PINCHER
Alipoulizwa BJ akadai hajui chochote kuhusu tabia za Mnadhimu Pincher, lakini watu wakazidi kusema kuwa BJ alikuwa anajua fika.
Baadae BJ alikiri kuwa alikua anajua tabia ya mnadhimu wake na akaomba radhi kumteua. Hili likamtafuna polepole.
- ‘PARTYGATE SCANDAL’
👉 Mwezi may 2020 walifanya ‘party’ kwenye bustani iliyopo Downing street (makazi ya Waziri Mkuu) na BJ alikuwepo.
👉 Mwezi Juni 2020 BJ alienda kwenye sherehe ya ‘birthday’ yake, ambapo ilisemekana kanuni za ‘Lockdown’ zilivunjwa.
Yote ilikuwa siri lakini Novemba 2021 gazeti la ‘Daily Mirror’ likaripoti matukio haya, ripoti nyingi zaidi zikafuata ila alipoulizwa BJ alisema kanuni za ‘social distancing’ zilifuatwa! Na uongozi wa Makazi ya ‘Downing Street’ (makazi na ofisi za Waziri Mkuu) walisema hakukuwa na ‘party’ yoyote.
Wiki moja baadae Video ikasambaa mtandaoni kumuonesha mkuu wa kitengo cha habari na mwenzie wakifanya mzaha kuhusu kanuni za ‘lockdown’. Shughuli ikaanzia hapo, Bunge likaunda kamati kuchunguza nini hasa kilitokea.
Miezi ikapita Januari 2022 ripoti ikatoka ikieleza kinaga ubaga kuwa sheria za ‘lockdown’ zilivunjwa kwenye ‘party’ ya mwezi mei 2020. BJ akajitokeza kukiri kuwani kweli alienda kwenye ‘party’ na kuomba radhi.
Iliposambaa ile video ya mkuu wa kitengo cha habari BJ aliunda chombo cha kuchunguza ambacho kilitoa ripoti mwezi mei 2022 ambayo ilieleza kuwa Watu walilewa sana kwenye ‘party’ hiyo na wengine walifanya vitendo vya dharau kwa wafanyakazi za usafi na ulinzi jengoni hapo.
- SKENDO YA KUKUTANA NA AFISA WA ZAMANI WA KGB