Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mkuu naomba nikuweke sawa kidogo kwenye hoja yako kuhusu mambo mawili.AJABU YA UTEUZI WA WAZIRI MKUU UINGEREZA 🇬🇧
Na JumaKilumbi,
05.09.2022
Uingereza ni nchi ya kidemokrasia, Demokrasia iliyokomaa hasa, ila ina Malkia mwenye mamlaka ambayo huizidi katiba kwa sehemu.
Kuna mengi ya kuuliza kuhusu ‘Demokrasia’ yao ila leo tuzungumze kuhusu kupatikana kwa Waziri Mkuu wao.
WAZIRI MKUU NI NANI HASA?
Ni kiongozi wa Serikali mwenye mamlaka ya teuzi zote za juu; Teuzi za mabalozi, Teuzi za Baraza la mawaziri na Teuzi za maafisa wa Jeshi.
Pia ana mamlaka juu ya Utungaji wa sheria Utungaji wa sera na Utumaji Majeshi nje.
Muhimu ya yote ana sikio la Malkia, aweza mshauri kitu Malkia naye akafuata, kama vile Kuvunja Bunge!
WAINGEREZA 🇬🇧 HAWACHAGUI WAZIRI MKUU WAO
Tofauti na Tanzania 🇹🇿 ambapo huku kila baada ya miaka mitano tunapiga kura kumchagua kiongozi wa serikali, Rais, wao humchagua mtu mmoja tu, Mbunge.
Hao Wabunge wakienda Bungeni hujitazama, Chama kipi kitakuwa na Wabunge wengi?
Kama ni Labor basi Malkia atamteua kiongozi wa chama cha Labour kuwa Waziri Mkuu, na kama ni ‘Conservative’ vivyo hivyo.
Kwahiyo WAINGEREZA HAWCHAGUI WAZIRI MKUU!
SAKATA LA KUANGUKA KWA BORIS JOHNSON!
NB: Boris Johnson = BJ
BJ Alimteua bwana Pincher kuwa Mnadhimu wa chama chake cha Conservative. June 29, 2022 Picher alienda klabu alilewa sana akaanza kubambia wanaume wawili. Ikazuka skendo kubwa na nyingine kumhusu zilizowahi tokea huko nyuma. Watu wakasema ndiyo tabia yake.
- SKENDO YA CHRIS PINCHER
Alipoulizwa BJ akadai hajui chochote kuhusu tabia za Mnadhimu Pincher, lakini watu wakazidi kusema kuwa BJ alikuwa anajua fika.
Baadae BJ alikiri kuwa alikua anajua tabia ya mnadhimu wake na akaomba radhi kumteua. Hili likamtafuna polepole.
Hili lilikuwa zito, si unaikumbuka Covid-19? Lockdown je? Basi ilipozuka Uviko-19 BJ na serikali yake wakaweka katazo la watu kuchangamana ili kuepusha kusambaa kwa virusi.
- ‘PARTYGATE SCANDAL’
👉 Mwezi may 2020 walifanya ‘party’ kwenye bustani iliyopo Downing street (makazi ya Waziri Mkuu) na BJ alikuwepo.
👉 Mwezi Juni 2020 BJ alienda kwenye sherehe ya ‘birthday’ yake, ambapo ilisemekana kanuni za ‘Lockdown’ zilivunjwa.
Yote ilikuwa siri lakini Novemba 2021 gazeti la ‘Daily Mirror’ likaripoti matukio haya, ripoti nyingi zaidi zikafuata ila alipoulizwa BJ alisema kanuni za ‘social distancing’ zilifuatwa! Na uongozi wa Makazi ya ‘Downing Street’ (makazi na ofisi za Waziri Mkuu) walisema hakukuwa na ‘party’ yoyote.
Wiki moja baadae Video ikasambaa mtandaoni kumuonesha mkuu wa kitengo cha habari na mwenzie wakifanya mzaha kuhusu kanuni za ‘lockdown’. Shughuli ikaanzia hapo, Bunge likaunda kamati kuchunguza nini hasa kilitokea.
Miezi ikapita Januari 2022 ripoti ikatoka ikieleza kinaga ubaga kuwa sheria za ‘lockdown’ zilivunjwa kwenye ‘party’ ya mwezi mei 2020. BJ akajitokeza kukiri kuwani kweli alienda kwenye ‘party’ na kuomba radhi.
Iliposambaa ile video ya mkuu wa kitengo cha habari BJ aliunda chombo cha kuchunguza ambacho kilitoa ripoti mwezi mei 2022 ambayo ilieleza kuwa Watu walilewa sana kwenye ‘party’ hiyo na wengine walifanya vitendo vya dharau kwa wafanyakazi za usafi na ulinzi jengoni hapo.
ATHARI ZA SKENDO
Baada ya mambo kuwa dhahiri BJ akapoteza uungwaji wa wananchi wengi, Wabunge wa Upinzani na chama chake wakataka ajiuzulu. Wakafikia kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae, BJ akashinda kura hiyo.
Lakini tarehe 7 Julai 2022 BJ akatangaza kujiuzulu nafasi ya Kiongozi wa chama chake cha ‘Conservative’ na Uwaziri Mkuu, lakini ataendelea kuwa Waziri Mkuu mpaka atakapopatikana mrithi wake.
KILICHOFUATA
Basi chama chenye serikali kiliendesha mchakato wa kupiga kura kumchagua Kiongozi mpya wa chama hicho, ambaye moja kwa moja ndiye atakaekuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.
Mchakato ulimalizika kwa Bi. Liz Truss kushinda nafasi hiyo na 6.09.2022 alienda Scotland kwenye kasri la Balmoral alipokuwa Malkia Elizabeth II kuagizwa kuunda serikali, Maana Malkia ndiye humtafuta mtu wa kuunda Serikali .
KWAHIYO WAZIRI MKUU ANAPATIKANAJE?
Malkia ndiye anateua Waziri Mkuu, na moja ya sifa za mtu huyo ni awe na wafuasi wengi Bungeni, kwa kesi hii mtu toka chama cha Conservative ndiye mwenye wafuasi wengi Bungeni. Hivyo Mchakato wa wanachama 160,000 wa ‘Conservative’ kupiga kura kumchagua Kiongozi wao mpya ndiyo kumechagua Waziri Mkuu mpya wa Uingereza yenye watu Milioni 67.
View attachment 2348993
1. Waziri mkuu wa Uingereza huchaguliwa na wananchi kupitia chama chake ambapo kikishinda uchaguzi na kuwa na idadi kubwa ya wabunge, kiongozi wake ndie huja kuwa waziri mkuu.
Hivyo basi, wananchi wa nchi hiyo huchagua waziri mkuu kupitia chama chake.
Ikitokea waziri mkuu anajiuzulu nafasi hiyo basi chama hufanya mchakato wa kutafuta kiongozi mwingine ambae akipitishwa huja kuwa kiongozi na pia waziri mkuu.
Moja ya mamlaka ya waziri mkuu ni kuitisha uchaguzi wa haraka ambao huitwa "snap election" ili kutafuta wingi zaidi wa wabunge ambao utamsaidia kupoitisha ajenda kadhaa bila kusumbuliwa. Hatua hii ni ina madhara kwani yahitaji waziri mkuu kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa atashinda.
Boris Johnson alifanya hivyo mwaka 2019 na akashinda uchaguzi kwa kishindo na kuwa na idadi kubwa ya wabunge na kwa kuwa yeye ni bingwa wa ushawishi alikonga nyoyo za waingereza wengi.
2. Malkia wa Uingereza hachagui waziri mkuu bali humuidhinisha rasmi baada ya chama chake kushinda uchaguzi na kumruhusu kuunda baraza lake la mawaziri. Pia Malkia ni lazima aidhinishe kujiuzulu kwa waziri mkuu ikiwa kiongozi huyo amelazimika kujiuzulu.
Na mwisho ni kwamba Malkia hajishughulishi na aina yoyote ya siasa za nchi hiyo na hata akisema kitu fulani (kuhusu siasa) basi Buckingham Palace huombwa kutoa ufafanuzi ili kuondoa dhana kwamba ana ushawishi juu ya mada fulani.