Ajabu ya uteuzi wa Waziri Mkuu wa Uingereza

Mkuu naomba nikuweke sawa kidogo kwenye hoja yako kuhusu mambo mawili.

1. Waziri mkuu wa Uingereza huchaguliwa na wananchi kupitia chama chake ambapo kikishinda uchaguzi na kuwa na idadi kubwa ya wabunge, kiongozi wake ndie huja kuwa waziri mkuu.

Hivyo basi, wananchi wa nchi hiyo huchagua waziri mkuu kupitia chama chake.

Ikitokea waziri mkuu anajiuzulu nafasi hiyo basi chama hufanya mchakato wa kutafuta kiongozi mwingine ambae akipitishwa huja kuwa kiongozi na pia waziri mkuu.

Moja ya mamlaka ya waziri mkuu ni kuitisha uchaguzi wa haraka ambao huitwa "snap election" ili kutafuta wingi zaidi wa wabunge ambao utamsaidia kupoitisha ajenda kadhaa bila kusumbuliwa. Hatua hii ni ina madhara kwani yahitaji waziri mkuu kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa atashinda.

Boris Johnson alifanya hivyo mwaka 2019 na akashinda uchaguzi kwa kishindo na kuwa na idadi kubwa ya wabunge na kwa kuwa yeye ni bingwa wa ushawishi alikonga nyoyo za waingereza wengi.

2. Malkia wa Uingereza hachagui waziri mkuu bali humuidhinisha rasmi baada ya chama chake kushinda uchaguzi na kumruhusu kuunda baraza lake la mawaziri. Pia Malkia ni lazima aidhinishe kujiuzulu kwa waziri mkuu ikiwa kiongozi huyo amelazimika kujiuzulu.

Na mwisho ni kwamba Malkia hajishughulishi na aina yoyote ya siasa za nchi hiyo na hata akisema kitu fulani (kuhusu siasa) basi Buckingham Palace huombwa kutoa ufafanuzi ili kuondoa dhana kwamba ana ushawishi juu ya mada fulani.
 
Si kweli, Kwenye Uchaguzi mkuu ambao huitwa kila baada ya miaka 5 Wananchi hupiga kura ya kumchagua Mbunge wa eneo lake tu.

Wabunge wakishaenda Bungeni hupatikana chama chenye Wabunge wengi, kisha mtukufu Malkia humteua/‘appoint’/humualika Mbunge mmoja toka chama chenye Wabunge wengi kuunda serikali, hapa huwa ni Kiongozi wa chama hicho. Kwa mtiririko huo Waingereza wao humchagua Mbunge tu. Waziri Mkuu hutokana na Chama chenye Wabunge wengi ambaye huwa ‘appointed’ na Mtukufu Malkia kama sehemu ya mamlaka yake.

Na pia tovuti ya Bunge la Uingereza umeweka wazi nini hutokea wakati wa Uchaguzi mkuu.

Ikitokea waziri mkuu anajiuzulu nafasi hiyo basi chama hufanya mchakato wa kutafuta kiongozi mwingine ambae akipitishwa huja kuwa kiongozi na pia waziri mkuu.

Naam, ni kweli kabisa.

Kweli kabisa.

Nadhani tunapishana lugha tu, kiprotokali Baada ya Uchaguzi mkuu Malkia humwita Kiongozi wa chama chenye Wabunge wengi na kumuagiza/kumuomba kuunda serikali, hapo ndipo anateuliwa kuwa Waziri Mkuu.

Ama kwa maneno mengine ni kwamba, Malkia ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Waziri Mkuu, lakini uteuzi huo haufanyi kwa utashi wake, ila huongozwa kufanya hivyo kwa kufuata vigezo na moja ya kigezo hiko ni mtu huyo atakayemteua ni lazima awe na wafuasi wengi Bungeni.

Na mwisho ni kwamba Malkia hajishughulishi na aina yoyote ya siasa za nchi hiyo na hata akisema kitu fulani (kuhusu siasa) basi Buckingham Palace huombwa kutoa ufafanuzi ili kuondoa dhana kwamba ana ushawishi juu ya mada fulani.

Ni sahihi kabisa kwa maana Malkia anapaswa kuwa nembo ya Muungano kitaifa hivyo hajihusishi na mivutank yeyote ya kisiasa.
 
Mkuu, mimi nimeishi Uingereza (kama miaka 3 na ushei hivi)na nimepiga kura nikiwa raia wa Jumuiya ya Madola.

Raia wa Jumuiya hiyo wanaruhusiwa kupiga kura.

Hivyo ni jambo la hekima kunifahamu.

Pale wapiga kura yako, mbunge unaemchagua ndiyo wakichagua chama chake kwenda bungeni.

Chama chenye wabunge wengi walochaguliwa ndicho hushinda uchaguzi.

Wao watumia mfumo wa "First Past The Post" yaani mwenye wingi wa kura ndio mshindi hata kama mgombea apata chini ya asilimia 50 jambo linoweza kutokea iwapo kuna wagombea wawili maarufu. Mfumo huu huvisaidia vyama ambavyo vina wafuasi wengi katika maeneo makubwa.

Kwa mfano chama cha wahafidhina uchaguzi wa 2019 kilishinda kwa kura nyingi maeneo ya katikati ya nchi (Midlands) na kaskazini, kwasababu wazungu wengi wasopenda wageni nchini humo walipenda Boris Johnson awe waziri mkuu ili tu kutimiliza ajenda yao ya Brexit yaani kutoka kwenye Umoja wa Ulaya.

Hivyo Boris Johnson akaenda kupata wabunge wengi Bungeni yaani "majority" na mambo mengi yakapitishwa bungeni kwa kuzingatia kuwa yeye ana dhamana (mandate) alopewa na wananchi.
 
Nashukuru kufahamu, vipi maisha kule Uingereza? Natamani kuzuru siku moja.

Ila kama nilivyosema, tunapishana lugha tu,
Ila ngoja twende sawa, kwenye ‘Ballot paper’ kuna chaguzi ya kumchagua Waziri mkuu kama ilivyo huku kwetu kwa upande wa rais?
 
Maisha ya pale UK ni magumu kama hujajiandaa kwa maana ya aina ya ukaazi wako.

Lakini kama uko poa kifedha na kikazi waweza kwenda pale kutembea. Waweza jiandaa kwenda kushuhudia uchaguzi unokuja.

Ila Uingereza kwenye uchaguzi huwekwa wagombea wa vyama na utaratibu ni kuchagua wabunge ambao ndo huenda bungeni na kura hiyohiyo huchagua waziri mkuu.
 
Ile nchi ya kipuuzi sana familia iyo moja tokea mwaka 1066 inatawala tuu nchi mpaka leo alafu wao wamekalia kuzisema royal family nyingine kwamba hazina Democrasia na wakati wao pia hawana democrasia...
Vip mifumo ya nchi Yao ni kama ya kwetu? Au Iko imara sana
 
Hata Mimi namshangaa. Skendo ya kuwa mtoa habari wa Russia ndiyo iliyomvuruga zaidi na kuonekana hafai hata ndani ya chama chake
Jamaa Wana mifumo imara sana ya taasisi zake.

Wananchi wake wanajielewa sana. Ndo maana ukileta shida tu unaondolewa chapu. Hawataki upuuzi. Angalia upuuzi unafanywa na viongozi wetu. Wao ni miungu watu na Wala hawahitaji kukosolewa kama aliyeondoka
 
Yaani uko sawa asilimia 101.
 
Sasa malikia kazi zake hasa ni zipi ndani ya taifa?
 
Ile nchi ya kipuuzi sana familia iyo moja tokea mwaka 1066 inatawala tuu nchi mpaka leo alafu wao wamekalia kuzisema royal family nyingine kwamba hazina Democrasia na wakati wao pia hawana democrasia...

Hili jambo tutaliangaziq siku moja.
 
Oh sawa sawa.
 
Andiko langu nimelipa jina ‘Ajabu ya uteuzi wa waziri mkuu wa Uingereza’ .

Hakuna pahali nimesema SIO YA KIDEMOKRASIA.

Tafadhali soma tena kisha karibu kwa mjadala juu ya upatikanaji wake, kama unaona nimekosea kueleza ama kufafanua karibu kukosoa.

Halafu wakati mwingine tujadili AINA YA DEMOKRASIA mada unayoonekana unapenda sana kuijadili.

Karibu Mkuu.
 
Ile nchi ya kipuuzi sana familia iyo moja tokea mwaka 1066 inatawala tuu nchi mpaka leo alafu wao wamekalia kuzisema royal family nyingine kwamba hazina Democrasia na wakati wao pia hawana democrasia...
Wao wqnajiheshimu na kuheshimu wenhine,sisi tunajiina miungu watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…